Rais Mwinyi wa Zanzibar naye atakuwa anamuachia Mama awe anaenda Safari zake kama Mama afanyavyo Kwake?

EeenHeee, mada hizi!

Wengine tuna'admire' guts alizo nazo mama.

Naona mwana mama ni kama alikuwa amejiandaa kwenye nafasi hii.

Atawachokonoa wenye roho hadi zitapasuka, na hakuna mtakachoweza kufanya!

Mkiropoka, VUNJA!! Hapo mama na kundi lake watakuwa wametimiza lengo.

Sasa 'mta DO?
 
Uwe na adabu mkuu....

Hamkumpangia majukumu VP kipindi cha hayati JPM.....basi mnampangia Rais leo hata wa kumtuma kumuwakilisha ?!!! Khaaaa

Pathetic
Hapana.

Kama ni "Pathetic", wewe inakuhusu sana, kwa sababu umefumba akili , macho na kila kitu, usiweze kuelewa chochote!

Sema, kama ameamua kuvunja utaratibu wa mpangilio wa uongozi chini ya Jamhuri ya Muungano..., basi afanye hivyo kwa kujua anavunja utaratibu huo kwa maksudi.

Hilo haliwafanyi wanaohoji kuwa "Pathetic."
 
Na ukiona nimeanzisha Uzi jua kuna ' nilichokibaini ' na nakiona ama hakija kaa sawa au kina ' Ulakini ' hivyo ' nawachokozeni ' tu Great Thinkers ninaowapendeni ( JF Members ) ili tujadili na kwa marefu na mapana yake. Ubunifu huu ' Mama ' nahisi utaanza ( au umeshaanza ) kuzaa ' Visununu ' kwa upande wa Tanzania Bara na najua akina Mpango ( VP ) na Majaliwa ( PM ) linawauma mno ila ' wanajikausha ' tu.
Huu ni mfano dhahiri kuwa nchi bado inaongozwa bila kufuata kanuni tulizojiwekea na ni msisitizo kuwa bila katiba mpya tunaweza kurudi tulikotoka.
 
Mwingine yupo SADC mwingine yupo ana cheza na panya SUA, Kazi iendelee il karma hatari inaweza kukutafuna hata kaburini, Mwendezake alimpuuza leo ndio Namba moja
 
Yeye Mama aliwaambia Urais hautaki 2025? Hivi kwa Afrika hii uijuayo Wewe kuna Mtu ' akiuonja ' tu ' Urais ' atatamani Kuondoka mapema Madarakani na Kumkabidhi Mtu mwingine ' Kiurahisi ' tu kama msemavyo?
Yule mama alikataa kugombea Zanzibar mwaka 2020 akisema hiyo itakuwa ni demotion kwake!
 
Hapo maza anaharibu wasijisahaulishe wao wako milioni moja na nusu tu, wanapotaka fursa sawa wajue wengi ndio tunaoamua hatma ya Muungano feki unaowanufaisha Zanzibar kuliko Tanganyika Mbona magufuli alimwagiza sana Makamu wa Rais na Waziri Mkuu kuliko mwingine yoyote,
Kuna Siri gani kati ya Samia na Hussein?
 
Kama ulivyo Muungano unavyofikirisha ndivyo ilivyo kwa Rais wa JMT wa Tanzania kuwakilishwa nje ya nchi na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Kwa Katiba ya JMT (1977), Rais Mwinyi ni mjumbe wa Baraza la Mawaziri Serikali ya JMT, lakini kwa Katiba hiyo hiyo, Baraza la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, japo Zanzibar ni sehemu ya nchi ya Tanzania. Hii ina maana maamuzi yanayogusa masuala ya Muungano yaweza kufanyiwa maamuzi bila upande wa pili wa Muungano (Tanzania bara) kuwakilishwa. Ingefaa Waziri anayeshughulikia masuala ya muungano, kama siyo Waziri Mkuu, awakilishe Serikali ya Muungano.

Nukuu ya Ibara husika za Katiba ya JMT (1977):

54.-(1) Kutakuwa na Baraza la Mawaziri ambalo wajumbe wake watakuwa ni Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais wa Zanzibar na Mawaziri wote.
(2) Rais atahudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri na ndiye atakayeongoza mikutano hiyo. Na endapo Rais hayupo basi mikutano itaongozwa na Makamu wa Rais na kama wote wawili Rais na Makamu wa Rais hawapo Waziri Mkuu ndiye ataongoza
Mikutano hiyo.


Kwa msingi huo wa Ibara ya 54.-(2) Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kumwakilisha Rais wa JMT kiKatiba inafikirisha.

105.-(1) Kutakuwa na Baraza la Mapinduzi la Zanzibar litakalokuwa na wajumbe wafuatao:
(a) Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi;
(b) Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar;
(c) Mawaziri wote wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar;
(d) Wajumbe wengine watakaoteuliwa na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa mujibu wa masharti ya Katiba ya Zanzibar.


Kwa Ibara hiyo ni dhahiri maamuzi ya Baraza yanakuwa hayana baraka za uongozi wa Serikali ya JMT. Yawezekana hii ndio ikawa kiini cha migogoro ya Muungano kwa kuwa yanayoamriwa katika hilo Baraza hayapingwi mahala popote.

Nukuu ya Katiba ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (1984), Toleo la 1995:

1. Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
...
4. Katiba hii ni Katiba ya Zanzibar na itakuwa na nguvu za kisheria nchini kote na isipokuwa kutokana na kifungu 80 ikiwa sheria yo yote inatofautiana na Katiba hii, basi Kaliba hii ndiyo itayokuwa na nguvu na sheria hiyo itakuwa batili kwa kiwango kile ambacho kinahitilafiana.

80.-(1) Kwa masharti ya kifungu hiki Baraza la Wawakilishi linaweza
kubadilisha kifungu chochote katika Kaliba hii.


Kimsingi maamuzi ya Baraza la Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi, ambayo hayana mwakilishi wa Serikali ya Muungano yanaweza kuathiri shughuli za Muungano na ustawi wake.

43.-( 1) Kutakuwa na Baraza la Mapinduzi ambalo litajumuisha Rais, Waziri Kiongozi, Mawaziri pamoja na Wajumbe wengine kama Rais atavyoona inafaa.
...
(5) Baraza la Mapinduzi kwa pamoja litawajibika kwa Baraza la Wawakilishi p.unoja na watu kwa ujumla kuhusiana ua mambo yate yaliyotenowa na au kwa amri ya Rais au Waziri Kiongozi au Waziri mwengine kalika utekelezaji wa shughuli zake za kazi.


Vifungu hivyo vya Katiba vinalipa Baraza la Mapinduzi, ambalo halina mwakilishi kutoka upande wa pili wa Muungano, kufanya maamuzi, km kwa kifungu cha 80.-(1) ambayo yanaweza kuathiri afya ya muungano.

Yafuatayo ni majumuisho yangu kwa mtazamo wangu binafsi. Awali Rais wa JMT kutoka Zanzibar alikuwa Ali Hasani Mwinyi. Pamoja kwamba mwanzilishi wa muungano, Baba wa Taifa, Mwl Nyerere, alikuwa bado hai, aliweza kuvunja Azimio la Arusha na kuruhusu Katiba ya Serikali ya Mapinduzi kufanyiwa marekebisho yaliyotambua Zanzibar kama nchi na Taifa kiasi cha kuwa na wimbo na bendera. Nanukuu hiyo Katiba (2) Serika.li ya Mapinduzi ya Zanzibar itakuwa na uwezo wa kuweka kitu chochote kitakachokuwa kielelezo cha Serikali kama itavyokubaliwa na sheria iliotungwa na Baraza la Wawakilishi ambalo halina mwakilishi kutoka Tanzania bara kama ilivyo kwa Bunge la JMT

Sasa Serikali ya JMT inaongozwa na Mzanzibari tutegemee mabadiliko makubwa ya Kijamii, Kisiasa na Kiuchumi kwa faida ya Zanzibar.
Kwahiyo 'Mama' anakosea au anapatia?
 
Ni walakini mkubwa sana; kama anapenda Zanzibar isikikike zaidi, basi ateuwe Waziri wa mambio ya nje kutoka Zanzibar ndiye awe anamwakilisha, kama ambavyo Mwinyi alikuwa amemuweka Hassan Diria. Lakini kumtumia Rais wa Zanzibar kumwakilisisha Rais wa Jamhuri ya Muungano ni kosa kubwa na ni uvunjaji mkubwa wa katiba. Mama asilewe madaraka kupita kiasi!
Nashukuru kwa wengi kuona Tatizo hili.
 
Huyu mother Theresa aambiwe ukweli aache ujanja wake wa kuipa fursa zenji, kwenye mambo ya msingi ya JMT.
Binti tulia hebu.

Haya mambo usiyaangalie tu juu na wala usiwe kichwa mchunga. Karibu kiembe samaki kwa Butros upate urojo uliokwenda shule.
 
EeenHeee, mada hizi!

Wengine tuna'admire' guts alizo nazo mama.

Naona mwana mama ni kama alikuwa amejiandaa kwenye nafasi hii.

Atawachokonoa wenye roho hadi zitapasuka, na hakuna mtakachoweza kufanya!

Mkiropoka, VUNJA!! Hapo mama na kundi lake watakuwa wametimiza lengo.

Sasa 'mta DO?
Una uhakika Kichwani Kwako zimetimia?
 
Mtaalamu, inawezekana umeupenda huo utaratibu ila ukasahau muundo wa serikali ya JMT.

Hussein Mwinyi ni nani katika serikali ya JMT?

WaZNZ wameshaona fursa ya kushika hatamu, SMZ haina kiti popote isipokuwa EAC, raisi wa SMZ hawezi kumuwakilisha raisi wa JMT.

Anamuwakilisha kwenye yale mambo 22 ya Muungano?

Raisi wa SMZ hawezi kuendesha Baraza la mawaziri mbele ya VP kama raisi wa JMT hayupo, iweje awakilishwe na naye nje? Protokali hapa imekaaje?

Nafasi ya raisi wa SMZ kuwa VP kwenye JMT ilishaondolewa kwa kuzingatia mkanganyiko wake, viongozi wakubwa 3 wa JMT wanapaswa kuwa juu ya raisi wa SMZ, sasa inawezekana vipi? Msaidizi wa raisi wa JMT ni VP, kwanini amtume raisi wa SMZ?

Kazi iendelee.
Kwa maana hiyo rais kavunja katiba ?
 
Hapana.

Kama ni "Pathetic", wewe inakuhusu sana, kwa sababu umefumba akili , macho na kila kitu, usiweze kuelewa chochote!

Sema, kama ameamua kuvunja utaratibu wa mpangilio wa uongozi chini ya Jamhuri ya Muungano..., basi afanye hivyo kwa kujua anavunja utaratibu huo kwa maksudi.

Hilo haliwafanyi wanaohoji kuwa "Pathetic."
Ninakubaliana nawe ' Mama ' anakosea.
 
Back
Top Bottom