Rais Mwinyi amemuapisha mkurugenzi mkuu mpya wa ZAECA

Blasio Kachuchu

Senior Member
Sep 7, 2016
153
111
DSC_4805.JPG

DSC_4777.JPG


Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abduulla (kushoto) Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe.Khamis Ramadhan Abdalla na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Mkurugenzi Mkuu wa Zaeca Bw, Ali Abdalla Ali katika Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo.

Viongozi Wakuuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wakipiga saluti wakati Wimbo wa Taifa ukipigwa leo kabla ya kuapishwa Mkurugenzi Mkuu Mpya wa ZAECA Bw.Ali Abdalla Ali (kulia) hafla ya kiapo imefanyika Ukumbi wa Ikulu Jijini Zazibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akimkabidhi Hati ya kiapo Nd. Ali Abdalla Ali mara baada ya kumuapisha kuwa Mkurugenzi Mkuu wa ZAECA,hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) alipokuwa akizungumza na Viongozi mbali mbali (hawapo pichani) waliohudhuria katika hafla ya kumuapisha Nd. Ali Abdalla Ali kuwa Mkurugenzi Mkuu wa ZAECA,hafla iliyofanyika Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar pamoja na kutoa maelekezo maalum kwa Mkurugenzi huyo.
DSC_4897.JPG

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) alipokuwa akimkabidhi Vitabu Nd.Ali Abdalla Ali, ikiwa ni muongozo katika utekelezaji wa kazi zake mara baada ya kumuapisha kuwa Mkurugenzi Mkuu wa ZAECA,katika hafla iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
 
Sawa Aende Akachape Kazi Asirudie Yale Yale Ya Police Aliyefutwa Kazi
 
Back
Top Bottom