Rais Museveni anachochea chuki baina ya Tanzania na Kenya

Kimsingi mimi sikatai hilo dili ninachokataa ni kutaka 'kusacrifice' uhuru na heshma ya Tanzania ili kupata dili la kibiashara. Kuna watu wapo humu wanapendekeza kuwe na 'kickbacks' kwa wajumbe wa Uganda. Haya ni maadili ya Kitanzania? Mbona tunataka kupotoka, kama ipo ipo tu, kama Muumba anataka biashara iwe yetu tutaipata tu, lakini sio kuilazimisha hata kwa kukiuka maadili. Sasa kama mtu anapendekeza tufanye biashara kinyume na baadhi ya watu wanashabikia, hilo halikubaliki na huo si uzalendo!
Kama ni offer za wazi kwa masllahi ya Serikali ya Uganda wala si kuuza uzalendo, mbaya ni kutoa rushwa kwa mtu binafsi hilo hata mm sipendi kuskia kabisa.
But kama ni kutoa offer let's say kutolipa ushuru kwa mwaka hilo nalo utasema ni kuuza utu?

Usiku mwema mkuu!
 
Mzee kwenye maadili huwa hakuna kumung'unya maneno chochote kinachofanyika kinyume na sheria au taratibu zalizowekwa ni ukosefu wa maadili. Hayo hayo ndiyo yaliyotufikisha hapa tulipo kiasi kwamba unashindwa kuelewa ni akili gani iliyofikiria katika kufanya maamuzi. Tizama sasa, hata wewe unashauri nchi itoe rushwa, na mwingine nae akipokea mshiko kwenye shughuli zake za utendaji wa kila siku utamlaumu?
 
M7 ana haki ya kutafuta the best deal kwa raslimali yake kwa kuangalia mambo mbalimbali; nafikiri hili swala tusilibebe kisiasa sana, ni la kibiashara na kiuchumi zaidi; na kwa jinsi siasa za ndani kule Kenya ya Kenyatta zinavyokwenda; tanganyika bado tuna nafasi ya kuukwaa mradi huo; leo hii wabunge wa county ya Turkana kuliko na mafuta wameapa bomba hilo halipiti ng'o! Tutumie soft power badala ya kashfa na matusi kwa kaka M7; kwani mwenye chake muungwana!
Mkuu, ninakuelewa vizuri.

Ni kweli Rais Museveni ana haki na uhuru wa kufanya maamuzi yake na serikali yake kama anavyoona ina manufaa kwake na nchi yake.

Kinachonishangaza ni hii aina ya kutafuta biashara anayofanya Rais Museveni na serikali yake. Ninaamini inajenga ufa na chuki ndani ya EAC.

Muda ni mwalimu mzuri. Muda utatoa majibu.
 
Hakuna kitu kibaya kama kulazimisha biashara. Upo uwezekano mkubwa wa kusacrifice hata utu na heshima yetu ili kupata hii biashara ya Kupitisha Bomba la Mafuta. Tusifikie hapo, ifike mahala nasi tumpe ukweli huyu mnafiki ili ajue analotaka kulifanya halikubaliki na halina mashiko. Kama alishaanza makubaliano na Kenya na wamefika katika hatua nzuri za utekelezaji ni vyema akaendelea nao.
Tukumbuke huyu M7 ni mnafiki anaweza kutugeuka kama alivyoweza kuwageuka jirani zetu. Tusilishabikie hili suala bila kuangalia udugu wetu, heshima yetu, uhuru wetu na fikra zetu na majirani wanaotuzunguka. Huyu M7 ni mnafiki ni bora kumtolea nje ili ajifunze kuishi vizuri na majirani zake. Kumbukeni leo mwenzako kesho kwako.
Well said Mkuu.

You just hit the nail on the head.
 
Hivi kweli kuna Mtanzania with good and sound mind ambaye anaamini kabisa kuwa East Africa Dream ni ukweli? Kwamba tutaungana baadaye tuwe nchi moja kwa msaada wa EU ambayo sasa hivi inazungumzia Brexit? Tanzania na Kenya zinashindania opportunities za land locked neighbours. Mtu ambaye hauoni huo ushindani, anajidanganya sana.
Kinachofanyika kwenye hii biashara ya kupitisha bomba la mafuta kinatoa angalizo la hatima ya EAC.
 
Sometimes Do Nothing may be another Alternative to solve Problems we have.
Fursa za kibiashara ndani ya nchi washirika wa EAC isije ikawa ni sababu za
utengano au hujuma za kuvunjana nguvu.
Si vyema mtu mmoja akawa-drive watu wawili eti kwa sababu tu yeye ana fursa
fulani ya uchumi.

Kwa niavyo kama hali hii itaendelea ni dhihili kabisa jumuiya hii haitakuwa
na uhai mrefu.(rejea historia ya EAC).

Katika hili yatupasa kuwa makini kama watanzania kwani yawezekana
ubeberu tayari umepitia mlango wa mafuta kutuvurugia utawala wetu.

Wenye mamlaka ya uchunguzi na wachunguze hili suala kwa makini sana
maana kukaa madarakani kwa muda mrefu kwa baadhi ya marais/viongozi wa ki-Afrika ni kutekeleza maelekezo ya mabeberu,lakini pia nina imani kuwa shetani huyu kama yupo
na akashindwe kabisa kwa jina la aliye juu ya yote.
Kwa kiasi kikubwa ninakubaliana na hoja yako lakini nimeshindwa kuelewa una maana gani unaposema, ubeberu tayari umepitia mlango wa mafuta kutuvurugia utawala wetu.
 
PK ndo wa kwanza kabisa kurudi kundini... kama utakumbuka; PK alikuja Dar mwaka jana na kila kitu kilikamilika wakati ule. Tanzania na Rwanda wameunda kitu kama agency ambayo itahusika na ujenzi wa reli Dar-Kigali na tenda imetangazwa tangu August mwaka jana na Shirika la Reli ya Rwanda ndilo linasimamia show.

Issue inaonekana kama imefanyika kimya kimya kv wakati haya yanafanyika ilikuwa ni kati kati ya joto la uchaguzi manake ilikuwa ni between July to August!
Pk alishamwona Uhuru ana guts za kitapeli na nchi yake ni landlocked so akaachana nae
 
Mzee kwenye maadili huwa hakuna kumung'unya maneno chochote kinachofanyika kinyume na sheria au taratibu zalizowekwa ni ukosefu wa maadili. Hayo hayo ndiyo yaliyotufikisha hapa tulipo kiasi kwamba unashindwa kuelewa ni akili gani iliyofikiria katika kufanya maamuzi. Tizama sasa, hata wewe unashauri nchi itoe rushwa, na mwingine nae akipokea mshiko kwenye shughuli zake za utendaji wa kila siku utamlaumu?
Offer ni kitu tofauti na rushwa,
Rushwa ni kwa kitu ambacho ni haki yako
Kibiashara ni offer na ni jambo la kawaida,
Waganda wasiporidhia kupitisha bomba Tz tutalalamika? wapi?
Kama mimi na wewe tunafanya biashara ya ving'amuzi halafu mimi nikatoa offer ili kupata wateja wapya wengi ntakuwa nimetoa rushwa?
Otherwise sijui maana ya neno rushwa.
 
Unajua tanzania tumechelewa kuamka katika. Mambo mengi sana kwahiyo kuamka kwetu sisi kusiwe kwa kulupuka hadi ikasababisha tukakosana na majirani zetu wakenya. Kwasababu ya wametushinda kimaendeleo.

Nikiangalia historia ya makufuri ni mkulupukaji akiwa na waziri amewahi kufanya makosa mengi yaliyo isababishia serikali ikapata hasara. Na huenda museveni aliliona hilo mapema na akasema yule kwangu ni mrahisi. Lakini swali linakuja mveni anafanya yote haya ili apate faida gani? Na ilikuweje nayeye makufuri akamkubalia? Kiurahisi namna hiyo na akijua wakenya tayari wameisha aanza kutekeleza mkataba walio ingia na uganda? Siku zote rais inahitaji busara na maono ya mbali na kujifunza kutokana na makosa.
 
Offer ni kitu tofauti na rushwa,
Rushwa ni kwa kitu ambacho ni haki yako
Kibiashara ni offer na ni jambo la kawaida,
Waganda wasiporidhia kupitisha bomba Tz tutalalamika? wapi?
Kama mimi na wewe tunafanya biashara ya ving'amuzi halafu mimi nikatoa offer ili kupata wateja wapya wengi ntakuwa nimetoa rushwa?
Otherwise sijui maana ya neno rushwa.
Kwenye law of contract kuna kitu kinaitwa 'offer and acceptance' labda turudi huko ndipo tunaweza kuelewana. Au wewe unamaanisha nini? Au unamaanisha kufifisha masharti ya mkataba?
 
Binafsi PK nilimshangaa tangia mwanzo na hata hapa nilisema is like hawakufanya SWOT Analysis ya kutosha hususani kwenye sehemu ya THREAT! It's too risk nchi kutegemea reli inayopita kwenye nchi mbili tofauti. Rwanda walijisahau kwamba, kwa kutumia bandari ya Mombasa basi ili wao waweze kufanya biashara vizuri walohitaji stability ya nchi mbili (Kenya & Uganda) kwa pamoja wakati kutumia bandari ya Dar es salaam walichokuwa wanahitaji ni stability ya Tanzania peke yake. Good enough, kwa kuangalia historia hiyo moja yenyewe ndiyo inaonekana kuwa more stable not mentioning the stability of two countries ambazo stability zao hazina guarantee!
Lakini mkuu PK alikua na nia nzuri tu na Tanzania toka zamani, na mara kibao alishaomba sana ijengwe reli toka Tanga mpaka Kigali, ila si unajua tena nchi yako kwa mambo yake ya kiswahili, tulifanya upembuzi yakinifu mpaka jamaa alichoka akaamua enough is enough.

Ila baada ya kutengwa kidogo naona ndio mikakati ikaanza mpaka Sitta na Mkwerre wake wakaamua kuweka jiwe la msingi ujenzi wa reli(SGR).

Hii nchi inaongozwa na siasa za hovyo sana, kama tungeruhusu wataalamu washike nchi kama anavyofanya sasa JPM tungekuwa mbali sana aiseee
 
Kwa kiasi kikubwa ninakubaliana na hoja yako lakini nimeshindwa kuelewa una maana gani unaposema, ubeberu tayari umepitia mlango wa mafuta kutuvurugia utawala wetu.
Ubeberu ni mfumo wa kibepari ulioko
Kwa kiasi kikubwa ninakubaliana na hoja yako lakini nimeshindwa kuelewa una maana gani unaposema, ubeberu tayari umepitia mlango wa mafuta kutuvurugia utawala wetu.

Ubeberu ni Ubepari uliokomaa,na kamwe bepari hawezi kukubali kushindwa hivyo atafanya kila mbinu
ili tu yeye aonekane yuko juu yako either kwa kumtumia bepari mwenzake au mjamaa.

Maana halisi ni kuwa Tanzania ijayo ya Viwanda ni kikwazo kikubwa kwa mabepari hasa ukizingatia
kuwa viwanda vingi vitakuwa chini ya Umma/ubia,hivyo kwa nchi jirani ambazo mabepari wamewekeza
ni lazima uchumi wao utashuka kwa kasi.

Kwa maana nyingine ni kuwa kupitia Bomba la Mafuta + Gesi + Madini + Utalii + Uvuvi,Tanzania hii ya
leo ndani ya ndani ya miaka 20 ijayo itakuwa kama Canada.

Kwa nchi ambazo zimezoea kuwanyonya wengine
kwa kuwapa misaada na mikopo alafu zikaona namna tunavyopanga mipango kama hii ya maendeleo
yetu pasipo kuwategemea wao hakika watafanya kila wawezalo kutukwamisha.

Nina hakika kuwa bado kuna mirija ya ukoloni mamboleo ndani ya nafsi za viongozi wengi wa Afrika,
sisi Tanzania hayumkini tumeanza kujinasua taratibu ingawa wale jamaa wa IMF wamekwisha anza
kujipenyeza taratibu kuhakikisha kuwa tunaendelea kukopa ili tuzidi kudaiwa na hivyo kunaswa na mitego
ya ubeberu.
 
Naona mambo ya Unyumbu pembeni
Leo naunga Mkono hoja
Mambo ya kulialia Watanzania tuyaache
Hii fursa itakuwa aibu na hasara ikitupita kushoto
Ushamba wetu katika biashara za ushindani ndio una toa nafasi ya watu kuonyesha kama kuiogopa Kenya hivi,sasa Museveni kosa lake nini naye ana taka kupitisha mafuta yake apeleke sokoni na hawezi kupitishia hewani ni aidha Tanzania au Kenya,kisha naye ana wachumi wake na bila shaka wameona kupitia Tanzania kuna unafuu fulani na usalama,sasa mna letewa halua kwenye sinia mna ogopa kuila kwa kumhofia Jirani na jirani mwenyewe kesha tufanyia ufedhuli mara chungu nzima eti watu wame sahau,Tanzania now or Never.
 
M
Kwenye law of contract kuna kitu kinaitwa 'offer and acceptance' labda turudi huko ndipo tunaweza kuelewana. Au wewe unamaanisha nini? Au unamaanisha kufifisha masharti ya mkataba?

Mkataba hufungwa baada ya makubaliano yote,
mkataba ndio utadefine whether unanafuu kwa mwekezaji au la, lakini unafuu au ughali wa mkataba hutegemea matokeo ya mazungumzo ya awali,
kwa lugha rahisi na kwa faida ya wengi utakuwa umeelewa i hope
 
Binafsi PK nilimshangaa tangia mwanzo na hata hapa nilisema is like hawakufanya SWOT Analysis ya kutosha hususani kwenye sehemu ya THREAT! It's too risk nchi kutegemea reli inayopita kwenye nchi mbili tofauti.
...Walipoingia kwenye mazungumzo na UG na KE, walikuwa wanalijua hilo. They had no option, at least at that time.

...RW walionyesha interest kubwa kwenye reli ya kati, toka PK alipoingia madarakani. Lakini, kama unavyojua hali ya reli ya kati.

...They are still waiting for us. Ile ya kupitia UG na KE ni last resort, i mean they had to do something. Ndio maana kila mtu alitakiwa kujenga kipande chake.

Rwanda walijisahau kwamba, kwa kutumia bandari ya Mombasa basi ili wao waweze kufanya biashara vizuri walohitaji stability ya nchi mbili (Kenya & Uganda) kwa pamoja wakati kutumia bandari ya Dar es salaam walichokuwa wanahitaji ni stability ya Tanzania peke yake.
...They had no choice. Now their hopes are up.
 
...Walipoingia kwenye mazungumzo na UG na KE, walikuwa wanalijua hilo. They had no option, at least at that time.

...RW walionyesha interest kubwa kwenye reli ya kati, toka PK alipoingia madarakani. Lakini, kama unavyojua hali ya reli ya kati.

...They are still waiting for us. Ile ya kupitia UG na KE ni last resort, i mean they had to do something. Ndio maana kila mtu alitakiwa kujenga kipande chake.

...They had no choice. Now their hopes are up.

..kweli awamu iliyopita walikuwa very sluggish.

..yaani walikuwa wanachangamka kwenye ufisadi tu.

..mazingira hayo ndiyo yaliyosababisha Kagame akahamia kwa Uhuru Kenyatta na Museveni.

..reli ya rwanda-uganda-kenya ilikuwa hailipi kwa upande wa rwanda na hata wataalamu wa CoW walieleza ktk utafiti waliofanya.

..lakini hapo katikati Museveni akamgeuka Kagame kwa kuamua ku-extend reli kuelekea South-Sudan instead of Rwanda kwa maelezo kwamba reli ya kuelekea Rwanda hailipi na hana fedha za kujenga branch mbili[ya s-sudan na rwanda].

..kwa sasa hivi Kagame amerudi tena kwenye mradi wa awali wa Burundi, Rwanda, na Tanzania. Mradi huo umepewa jina la dikkm[dsm-isaka-keza-kigali-musongati]. Rwanda ndiyo imepewa jukumu la kushughulikia tender process ya mradi, ambapo so far wameshafanya short list ya wakandarasi 6 kama finalists nadhani.

..labda Magufuli atawachangamsha ili ujenzi wa mradi huu uanze mapema iwezekanavyo.

NB:

..bomba la mafuta ya uganda likija Tz maana yake mradi wa kenya wa lapsset utakuwa kama umekufa. Kwa upande wa kaskazini Ethiopia ameanza kujenga reli kuwaunganisha South Sudan na bandari ya Djibouti. Kuna fununu kwamba Ethiopia wana mpango wa kujenga bomba la mafuta ili South Sudan apitishe mafuta kwao kuelekea Djibouti. Ndiyo maana mnaona Kenya wamekuwa very desperate siku za karibuni.

cc chige
 
..kweli awamu iliyopita walikuwa very sluggish.

..yaani walikuwa wanachangamka kwenye ufisadi tu.

..mazingira hayo ndiyo yaliyosababisha Kagame akahamia kwa Uhuru Kenyatta na Museveni.

...Katika moja ya vitu vinavyonipa hasira at times ni reli ya kati.

..reli ya rwanda-uganda-kenya ilikuwa hailipi kwa upande wa rwanda na hata wataalamu wa CoW walieleza ktk utafiti waliofanya.

..lakini hapo katikati Museveni akamgeuka Kagame kwa kuamua ku-extend reli kuelekea South-Sudan instead of Rwanda kwa maelezo kwamba reli ya kuelekea Rwanda hailipi na hana fedha za kujenga branch mbili[ya s-sudan na rwanda].

...Actually, kama si rushwa na terrain katika ujenzi wa reli, gharama si kubwa kivile. Reli ya Mombasa-Nairobi inasemwa kuna hela inategenezwa, matata.

..kwa sasa hivi Kagame amerudi tena kwenye mradi wa awali wa Burundi, Rwanda, na Tanzania. Mradi huo umepewa jina la dikkm[dsm-isaka-keza-kigali-musongati]. Rwanda ndiyo imepewa jukumu la kushughulikia tender process ya mradi, ambapo so far wameshafanya short list ya wakandarasi 6 kama finalists nadhani.

..labda Magufuli atawachangamsha ili ujenzi wa mradi huu uanze mapema iwezekanavyo.

...This thing is long overdue.

...Nategemea afanye hivyo.

NB:

..bomba la mafuta ya uganda likija Tz maana yake mradi wa kenya wa lapsset utakuwa kama umekufa. Kwa upande wa kaskazini Ethiopia ameanza kujenga reli kuwaunganisha South Sudan na bandari ya Djibouti. Kuna fununu kwamba Ethiopia wana mpango wa kujenga bomba la mafuta ili South Sudan apitishe mafuta kwao kuelekea Djibouti. Ndiyo maana mnaona Kenya wamekuwa very desperate siku za karibuni.

cc chige
...That was my point, and why the Kenyans will not let go of this easily.

...Ethiopia wanaonekana kuwa na appetite ya kuwekeza miundo mbinu kuelekea Djibouti. Wana barabara na reli tayari. Meli zao zipo huko pia. It makes sense, but, many eggs in one basket.

...Wanategemea pia kuchimba mafuta. They've being very aggressive on that front of late.
 
Back
Top Bottom