Rais Magufuli: Wanafunzi UDOM waliofeli wakatafute vyuo vya saizi yao

Hakuna mtoto Wa mkubwa pale 98% watoto wamaskini but sema magu alishajua nyege zenu zipo wp kwhyo ni rahis kuwafikisha watu kama nyie
Kitu kama kuna mtoto wa magu pale alikuwa anasoma hesabu na IT ngoja niyachambue majina nitaanika kila kitu soon
 
Hii nchi mkanganyiko sana, serikali ilianzisha programme yenyewe, na ikafanya usahili yenyewe na wakijua fika wale vijana ni wa form four, wakawapatia nafasi leo hii mnawafukuza na kuwaita ni division 4 mara walipata zero, sasa mlipokuwa mnawafanyia usahili hamkujua hilo? serikali ingewaacha wakasoma hiyo course yao wakapata dip watakaofaulu vizuri wakaendelea na degree, sio sahihi kuwa mtu wa form four hawezi kusoma degree, kwani kunawatanzania wangapi wamemaliza form four wamekwenda Kenya kusoma degree?, ni wakenya wangapi wanaosoma nchi za nje tena vyuo vya maana kwa elimu ile ile ya kwao ya just form four tu wanajiunga na chuo na maisha yanakwenda? mistake kudanganya dunia kuwa elimu ya tz ni bora sana kuliko the rest of the world, kilichopo Tanzania ni utaratibu tu, culture kwamba chuo inatakiwa upitie form six kwanza, lakini sio lazima. Hapa serikali imekosea, imewapotea vijana muda na future zao, wajapan husema bila kujali wew umepita wapi ,umefikaje chuo, at the end we are looking for results only. Kama mtu wa form four kaenda chuo na kadeliver , kaajiliwa bado kadeliver vizuri that's all, mnataka nini tena? . Sawa utaratibu umekikwa lakini je nani kakiuka utaratibu huo? ni serikali au vijana hao, hataka ni watoto wa viongozi nani kawapeleka pale, hapa serikali ndo yenye makosa , lazima ikubali na iangalie jinsi ya kuwasaidia , na tuache kuwa na plan ya miaka miwili miwili, ni aibu ya karne taifa kubwa hatuna plan ya kudumu, kila siku tunakuja na plan za ajabu ajabu tu.

Mkuu umeongea point tupu! Kwanza rais amepishana kauli na waziri wake. Maana waziri kasems bungeni kwamba wanafunzi wale hawakufukuzwa kwasababu hawana vigezo..walifukuzwa kwasababu walimu wao walikua wamegoma. Yeye anakuja na kuwaita (in my opinion kuwatukana) vilaza! This from our president jamani!

In any case,hata kama ni kweli hawana vigezo..hivi ilikua ni busara kuwatimua kwa namna ile? Dodoma ile unawatimua wanafunzi elfu 7 ghafla vile waende wapi kwenye mji mdogo vile?

Halafu hao vijana elfu 7 ambao wanaitwa vilaza inamaana ndio basi tena? JPM anakosa busara ya kuona kwamba hata kama wameshindwa kupata hizo division 1 na 2..ile ni potential workforce kubwa sana kama watawezeshwa? Kweli kabisa hao wanakua dismissed kama takataka?

Dah..mie yangu macho. Mwaka wa kwanza hata haujaisha..sijui baada ya mitano tutakua tumefikishwa wapi.
 
safari bado ni ndefu mno kwa style hii. ili kuturidhisha wananchi, ni vyema wakaweka majina na alama walizopata mitihani ya form IV. kutuambia ni vilaza wakati walikua wanasoma masomo ya juu haituingii akilini.
Magu hataki kusema ukweli kuwa hayuko tayari kuona vijana wanatumia mabilioni ya pesa toka kwenye serikali yake. Aseme tu kuwa hizo hela zitaenda wapi badala yake.
 
Mkuu acha Magu atunyooshee elimu yetu, mchakatoa mzima wa kuchagua hawa vijana uliharibiwa na wajanja, watu walichomeka watoto na ndugu zao wasio na sifa ili tu wadake ajira. Wenye div 1 na 2 ni wachache, majority ni div 3 na 4 na hawa ndo anawaambia wakatafute vyuo vya size yao
Lakini kumbuka vigezo ni div. I, II, na III. Na wote waliochaguliwa wana sifa hizo. Kama yeye ni msema kweli aje na wale wenye four waliochomekwa, afanye kama alivyofanya kwenye sakata la wafanyakazi hewa shinyanga
 
Hebu tujiulize Magu ni mwalimu , je aliupenda au ndio yale ya BASHE ?
kWA KWELI JIBU anao Mheshimiwa ama mtu ambaye alisha wahi kumwambia kuhusu suala hilo (kama aliingia kwa kuupenda ama la). Lakini kwa kuangalia namna alivyo chaguliwa kuiunga na Kidato cha Tano, utaona kuwa alisoma mchepuo ulio kuwa na somo la tatu ambalo ni Ualimu. Mengine yalikuwa Kemia na Bayolojia.Inawezekana kuwa alipenda kuwa mwalimu tangu akiwa Vidato vya chini ama "alilazimika" kusomea Ualimu kutokana na Masomo aliyosoma Vidato vya juu na Diploma ya Ualimu mara tu baada ya kumaliza kidato cha Sita. Alisoma CB (Ed). Wengi wa waliosoma Kidato cha tanao na Sita na Kuunganisha Diploma ya Ualimu, wakati huo, walikuwa HAWANA Mchepuo "Uliokaa vizuri", Kwa Mfano wanafuzni wa CB (Ed), hawakuwa wamefaulu vizuri somo la Fizikia, nk.
 
Kabisa Mkuu miaka zaidi ya 14 kuanzia O level hadi Phd level ya kusoma kwa kiingereza halafu lugha haipandi. Tena si kiingereza tu bali hata Kiswahili chake ni kibovu. Ni kilaza wa kutupa.
Mkuuu taratibu taratibu, usije fikiri huyu ni baba mwanaacha mzee wa msoga. Vijana wake wakipita hapa wanalala mbele na wewe
 
pamoja na kwamba baadhi yao hawana sifa za kusoma program ile, bado sio sababu tosha ya kuwondoa kwa style ile. walipaswa kuondoka kwa utaratibu, maana sio wavamizi. waliwadahili wao wenyewe.
Kweli walitakiwa waondolewe kwa staha kidogo.
 
Kuna kitu watu hawaelewi. Leo nimemsikia Prof Mkumbo akifafanua ktk Azam tv kwamba wizara ndiyo iliamua kuchukua wanafunxi hata wa div 4, na waliwalazimisha tcu na chuo kuwapokea. Ni kwamba hii programu ilikuwa inafadhiliwa na benki ya dunia. Baadaye benki ya dunia ikajitoa. Sasa serikali imeshindwa kuendelea kuiendesha program hii. Mfano baada ya benki ya dunia kujitoa serikali imekuta ikudaiwa na wakufunxi karibu 9 bilioni. Ndio maana wakaamua kuwafukuza wanafunzi.
 
Back
Top Bottom