Rais Magufuli: Wanafunzi UDOM waliofeli wakatafute vyuo vya saizi yao

NCHI HII BANA KILA CKU MOVI MOVI 2, AF ZOTE HAZIISHAJ. ZOTE NUSU NUSU TU
 
hata kama ni sahihi hatua walizochukua kuwaondoa kwa mpango mbovu ndio tatizo ninaloliona
 
Wrong! Tatizo siyo hao watoto wanaoitwa "vilaza". Tatizo ni serikali (TCU/Wizara ya Elimu, Bodi ya Mikopo, UDOM etc) waliowadahili hao watoto na kuwaingiza hapo chuoni, na kuwapa hiyo mikopo. Interestingly, Rais ametoa hiyo kauli mbele ya Kikwete, ambaye serikali yake ndo iliongoza taasisi zilizofanya hayo makosa, na alikuwepo pale anacheka.
 
Yaan waondoke haraka wakatafute wanapostahili kulingana na elimu yao .Mi huu upuuzi sikua naujua Niliujua lst yr baada ya anko wangu kwenda Snt Joseph ya Arusha .Hawana sifa wanapata special fucult alwnc kila mwaka .Jpm chapa ilale
 
Habari wana JF,

Leo ni siku ambayo nimejikuta nashindwa kumuelewa Rais pale alipoongelea sakata la wanafunzi wa UDOM wa stashahada maalum ya ualimu.

Mh. Rais wakati hawa vijana wanaondolewa chuoni tuliambiwa ni kwasababu ya walimu kugoma kuwafundisha kwa takribani wiki tatu kutokana na mkanganyiko juu ya malipo yao.

Leo umekuja na kauli mpya masikioni kwetu isiyokuwa na ukweli wowote. Hivi mh. Rais kwanini mna kauli mbili tofauti? Mh. Rais una uhakika kuwa hao wanafunzi wengi wao wamefeli? Mh. Rais hivi kufaulu ni division 1&2 pekee? Mh. Rais mbona hawa vijana matokeo yao yalipangwa kwa GPA lakini wewe umeongelea division?

Mh. Rais unaanza kunipa wasiwasi na serikali yako hii kuwa haiwezi kutufikisha popote kwa kuanza kuwa na ndimi mbili na kuongea vitu usivyokuwa na uhakika navyo. Wale vijana kuhusu ufaulu wao ni mzuri wala hauna mashaka kwa kuwa wengi wamefaulu masomo ya sayansi na matokeo yao yamepangwa kwa GPA. Sina uhakika kama utakuwa umepitia matokeo yao vizuri.

Mh. Rais vijana wa kidato cha sita wamemaliza mitihani yao muda mrefu lakini mpaka sasa hawajui watasoma program zipi katika vyuo mbalimbali kutokana na kutokuwepo TCU guidebook mpaka sasa hivi. Na hii yote inasemekana wahusika wameshindwa kutoa kitabu hicho kutokana na sintofahamu iliyopo juu ya minimum requirement iwe D au C.

Mh. Rais tafadhali usiturudishe kwenye udahili wa miaka ile ya chuo kikuu kimoja ukadhani kufaulu ni division 1&2 peke yake. Ilikuwa hivyo kwa sababu kulikuwa hakuna vyuo vya kutosha. Naimani watu wako wanaopitia mitandaoni watakupa maoni yangu.
Weeeeee acha kabisa hiyo kitu. Lazima turudi ujimani. Hakuna kunywa pombe mchanga!?
 
Huna hoja...nchi siyo ya vilaza tena hii
Kama sina hoja ungepangua nilichoandika.

Wewe ndiye huna hoja.

Umeshindwa kupangua nilichoandika kwa hoja.

Hujui collective responsibility, hujui breach of contract, hujui compassionate government.

Google those terms first.

Halafu uje kujibu hapa.
 
Kwa hali inavyoendelea unaweza kusema Rais John Pombe Magufuli si saizi ya UKAWA mpaka sasa. Wengi hawapendi kusikia hili, ila lazima lisemwe ili kutafuta dawa ya kumkabili kisiasa.

Amewazidi. Kila idara anaonyesha anaelewa masuala mengi zaidi ya UKAWA wanayofanya. Yanamezwa kwa sentensi moja anayoongea anapopewa muda wa kusema kitu. Anajibu kwa ushawishi wa hali ya juu. Wanashindwa washike wapi na hakuna chombo cha taarifa kisicho tangaza habari zake.

Naangalia sijui wiki ijayo UKAWA watakuja na nini, maana amemaliza leo katika hotuba yake ya UDSM.
 
Iliyo wa-enroll ni serikali ya CCM sawa,lakini ni ya Kikwete sio ya Magufuli.Jamani lazima tufike mahali tuseme ushenzi huu basi.Serikali haiwezi kufumbia macho tatizo ambalo imeshaliona,lazima ili confront head on.Taifa haliwezi kuwapa Diploma watu wasiostahili.Mfumo ni Kufaulu Form four na Div.I or II uende Form V than VI halafu chuo Kikuu or Certificate,Dip.than Chuo Kikuu not otherwise.Hatuwezi kukubali nchi iwe ya vilaza.

You're very right. Makosa lazima yasahihishwe ingawa yalijulikana tangu enzi hizo. Kuna wenzako hawataki Magufuli atenganishwe na CCM na Mwenyekiti wake Kikwete. Sijui kama watafurahi kukusikia ukiita yaliyofanywa na Kikwete kuwa ni "ushenzi huu".
 
Kama ukilaza kwa mujibu wa definition aliyotoa mkulu leo ni chin ya division one na two, basi vilaza nchi hii tuko wengi sana.
 
Nimemsikiliza vizuri Mh Rais kweli anania ya dhati ya kuikomboa elimu yetu ambayo kwa kiasi kikubwa ilikuwa inakwenda kombo; shida yangu ni pale mkuu wangu huyu anakauli ambazo mimi binafsi sizifurahii yeye kama kiongozi mkubwa kuzitamka kumuita mtuu "kilaza" ambayo ni lugha ya kebehi nadhani hii haijakaa vizuri, hao unaowaita vilaza hawajajipeleka wenyewe wamepelekwa na serikali alafu tena hao unaowaita vilaza ndiyo unaowategemea wakupigie kura .Naamini hii lugha inamisamiati ya kutosha unayoweza kuitumia ili kumsaidia mtu ambaye yupo nje ya system
Wa yudom hawajapewa pesa ya mkopo na hawajagoma, nawapongeza. Wangegoma tunawafukuza na wanakaa huko nyumbani miaka mitano yaani wakati wa uchaguzi ndio tunawakumbuka kwa ajili ya kura. Na hapo wengine washakuwa wazee.
Hii ni kauli ya mtu anaeitwa rais. Duh tulikotoka ni karibu, tunakoelekea ni mbali!!
 
miaka ya themanini mzee kenyata akiwa rais kenya aliwahi kumwambia rais wa tanzania wakati huo Julius nyerere weweeee julius unaongoza maiti kila tukio watu wapo kimya tu.
 
Nimesikia mkulu anasema walikuwa wanachukua degree ila nilikuwa nimesikia walikuwa wanachukua deiploma na ni special program. .. mwenye kujua plz...
 
Back
Top Bottom