Rais Magufuli: Nilipokuwa waziri niliwahi kuteua mtu wa darasa la 7 kuwa meneja wa mkoa

Ameamua kuwawashia taa ya njano wasomi ambao alikua ana waamini. Inaonekana anafikiria kupiga u-uturn
Anashindwa kujua kuwa wasomi wengi ni kama yeye? Kuwa kama alivyo pata yeye PhD ndivyo na baadhi ya wengine nao wamepata! Kwa sababu hata hesabu za korosho zilivyo buma zimedhibitisha maandishi ya kijana Bs8 aliyetoweshwa baada ya kuandika maandishi hayo
 
Safi sana kumbe hata Ildephonce Bilohe (darasa la saba aliyegombea urais mwaka 2015) huenda akala shavu
 
Kuna wakati jiwe akili huwa zinarejea. Huwa zikirejea anaongea point sana,ingawa kwa hili inaweza kuwa mbinu ya kumbeba Daud Albert Bashite. Lkn ukweli kuhusu performance ya chochote haitegemei sana elimu ya vyeti,Kwa sababu hata elimu yenyewe ya darasani nao ni ubunifu. Yaani aliyegundua maandishi hakuwa Msomi.
 
Kusoma sana siyo kuwa na uwezo wa kuongoza...........Walimu wa UPE kwa asilimia kubwa ya wasomi nyuma ya 2005 ndiyo waliowafundisha Elimu ya shule ya msingi
 
I second, ukisoma kama haujaelimika ni bure kabisa. Wapo watu wana elimu lakini hawakubahatika kuhudhuria formal education. KAMA UNABISHA ANDAMANA
Kama ni hivyo; ni kwa nini kuna zoezi kubwa a la ghrama nyingi la uhakiki wa vyeti na siyo uzoefu? Manesi na madakitari wazoefu sana wameondolewa kwa kukosa vyeti vya form 4 ilihali vya class seven wanavyo? Is it rational?
 
Tatizo watanzania tumefanywa masoko, sisi wenyewe tunashindwa kutengeneza soko si tu la nje ya mipaka yetu hata la ndani , vitu vyote vinatoka nje ya nchi , labda chakula tu , Elimu nyingi zinazotoka nje, zinakuja kama biashara na si kutuelimisha, ndio maana kuongoza wa Tz , ni pasua kichwa kwelikweli , tumegeuzwa bidhaa za wenzetu , tunanunua vya wenzetu , tunasifia vya wenzetu, anaejaribu kutatua matatizo yetu atatukanwa sana , na ataambiwa hajasoma.
 
Sasa uhakiki wote serikalini uliowaondoa mpaka madereva wazuri ambao hawakuwa na vyeti vya kumaliza madarasa makubwa zaidi ya yanayotakiwa kujua kazi ya udereva ulikuwa wa nini?

Magufuli anaji contradict.
 
Kama ni hivyo; ni kwa nini kuna zoezi kubwa a la ghrama nyingi la uhakiki wa vyeti na siyo uzoefu? Manesi na madakitari wazoefu sana wameondolewa kwa kukosa vyeti vya form 4 ilihali vya class seven wanavyo? Is it rational?
Hapa jombaa umechanganya issues, ajira zinataka formal qualifications, kama hauna kaput. Ndiyo maana hilo zoezi liliendeshwa. Hoja ni kwamba wapo watu wamelimika bila ya kuwa na formal education ila siyo qualification ya kupata ajira ambazo formal qualification is a requirement.
 
Back
Top Bottom