Rais Magufuli: Mshahara wangu kwa Mwezi ni Sh. Milioni 9.5. Nitatoa salary slip...

ujinga tu huo...hata mtoto mdogo huwezi mdanganya kilahisi hivyo!! haya siku ya wajinga itumieni vyema
 
ha ha ha nikisiaga matamko ya jpm nafurahi sana na ninashangaa pia....
yaan jpm anasema analipwa mil9.5 kweli??? yaan anataka kutuambia kuwa mbunge anamzid rais kwa mshahara maana mbunge analipwa mil11.5.....kweli tz ni nchi ya kipekee.....hongera jpm wa vijiwen watazid kukushangilia na kukuita malaika.......umeiteka media vizuri.
 
Hamuachi fitina!! Raisi kulipwa 9M huoni ni uzalendo? wakati wakuu wa taasisi wanalipwa 36M.
Uzalendo upi?wakuu wa mashirika wanatunzwa kama rais?unajua marupurupu ya rais kwa mwezi ni tsh ngapi?changa la macho,hata wabunge ukiwauliza mshahara watakwambia 2ml. Na salary slip utaoneshwa
 
Huo ni uongo kweupe...takwimu znaonesha east africa mstaafu jk ndio alikuwa anaongoza kwa kulipwa mshahara mkubwa kuliko marais wenzie sasa iweje yeye ashushe ad mil 9.5 wakat wakurugenz wanapokea mil 35 aliowateua yeye?sidhan kama inaingia akilini huo ni uzush ktk hilo
 
Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametaja mshahara wake kuwa ni Tsh mil 9.5, huku akiahidi atatoa Salary slip zake punde akitoka mapumzikoni Chato.

Hiyo imetokea wakati wa kipindi cha magazeti leo tarehe 01/04/2016 ambapo watangazaji walisoma habari iliyoandikwa na gazeti la nipashe kuwa Zitto na Lissu waomba ataje Mshahara wake na ukatwe kodi.

Wakiwa katika mjadala huo, walipokea taarifa kuwa Rais kawasikia na katuma taarifa ofisi za Clouds kujuza mshahara wake kuwa ni mil 9.5 na atatoa stakabadhi zake akirudi Dar.

Huo ndio mshahara alioukuta na hata Rais Kikwete alikuwa akilipwa kiasi hicho pia.

Chanzo: Clouds 360 Asubuhi hii.
Sawa Mshahara wake ni Huo ila kwa ushauri wangu suala la kusema mshahara wake na kutangazwa katika Kituo Cha Clouds ni kuipa chati kituo hicho kwanini asingepeleka taarifa hiyo TBC
 
Haimaye Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametangaza mshahara wake kupitia kituo cha clouds tv katika kipindi cha 360...........kwamba anapata kiasi chha shilingi za kitanzania 9500000 kwa mwezi.

Aoneshe pia na pay stub yake sio maneno tu
 
Lowassa asema atapunguza mshahara wa Rais toka milioni 400 kwa mwezi hadi milioni mbili

Katika hotuba yake amesema haingii ikulu kutafuta fedha anaenda ikulu kwa kazi moja tu ya kuhakikisha wananchi wanakuwa na maendeleo . Amesema dhamira yake ni kuona taifa linasonga mbele kwa kasi ya ajabu.

Amesema atapunguza mshahara wa Rais ambao analipwa hivi sasa dola 192,000 sawa na milioni mia nne kwa mwaka hadi kufikia milioni mbili kwa mwezi hivyo kumfanya mwaka mzima kutumia milioni 24 kama mshahara wake wa mwaka. Amesema kuna faida gani ya mtu kupokea mshahara wote huo ili hali wananchi wako hawana maji , zahanati hakuna dawa, pembejeo za kilimo zipo juu, wakulima wanakopwa mazao yao.

Amesema haendi ikulu kutafuta ela amesema anaenda ikulu kwa kazi moja tu ya kuondoa umaskini nchini hiyo ndiyo dhamira yake.

Amewashangaa wanaosema anafuata fedha ikulu na kuwaambia kama mtu umeshindwa kutafuta fedha ujanani halafu utegemee upate fedha uzeeni hiyo ni ngumu kwa sababu uzeeni ni muda wa kusaidia jamii kwa kile ulichochuma ujanani.

Amesema wakati wa mabadiliko ni sasa, na mabadiliko hayo yatapatikana nje ya CCM kwani ipo haja ya kubadilisha mfumo hodhi wa chama tawala kama kweli tunataka kusonga mbele sisi kama taifa. Amesema yapo baadhi ya mambo CCM hawawezi kuyabadilisha kwa kuhofia watu watafumbuka macho hivyo itatishia uhai wao.
 
kwa rais kulipwa hivyo naona sawa. ila najua marupurupu yataongeza hicho kiac. kuhuc viongoz wa mashirika umma na taasisi zingine aangilie kwa undan juu ya kupunguza mishahara hiyo. kwan wapo wengi wazuri wenye fani za pekee ktk taasisi za kimataifa wanaliopwa mishahara mikubwa tunawaomba wafanye kazi bongo. ss km mtu analipwa mil. 30 ww umlipe mil. 15 si sawa. tutawakosa wataalamu wa nje. kwa mfano gavana wa BOT na mkuu wa NHC walikotoka wanalipwa zaidi ya kile wanqchopata ss. nafikiri Raic aangalie sio kote kwa kupunguza salary
 
Kuna watu wa ajabu sana maana mtu anabisha wakati ukweli wenyewe haujui unasena hapokei hicho kiasi wakati yeye kasema anapokea haya basi na mtuambie nyie yeye hua anapokea bei gani ili tujue nani mwongo
 
wanachokifanya viongozi wa CCM ni kuweka sukari kwenye kinyesi...
vituko show,the comedy,futuhi..tumeona
step aside.
wengine bahili asili ndio maana hata maendeleo hawana..
footballers tu wapo wanaokula zaidi ya milioni 200 kwa mwezi..
 
Ya kweli haya?! yule jamaa yetu wa msoga yeye alikuwa anakunja 192m us dollar kwa mwaka sawa 36 m tsh kwa mwezi!. basi magufuli ni mzalendo

Hata mimi najuwa hivyo, kwahiyo Rais ukiingia madarakani mshahara unajipangia mwenyewe au ikoje hii mwingine alipe hii na mwingine hii?
 
Back
Top Bottom