Rais Magufuli katumia barabara kutoka Dar kwenda Dodoma

Haya yote alikuwa hayaoni wala hayajui akiwa waziri kwa miaka 20? Real?

Kuna utofauti wa muda na cheo, ulikuwa waziri sio rais, ulikuwa muda uliopita ila msafara ni current, inamaana changamoto zitakuwa tofauti kwa kigezo cha muda na uwezo wa kuzishughuliki nao ni tofauti kwa kigezo cha mamlaka aliyokuwa nayo.
 
Bora angepanda train sasa Barbara zetu hizi haiwezi speed na misafara watumiaji ni wengi mpaka wanyama
 
hiiii nchi sijui aliye iroga Alisha kufa mie sielewi kabisaaaaa. yaaani napata taabu haya majibizano yangekuwa face to face pangechimbika tuuuu hapa.
Rais anapofanya kitu tumsifie jamani huuu mda sio wa campaign ulishaisha siku nyingi kimebaki ni Kazi tuuu. nawashauri team lowasa tulie Dawa ilishawaingia tuuu hakuna namna msilete ushabiki mwingine ambao hauna maana huuu mda ni Wa kijenga nchi.
Hiki kitendo cha rais kutumua gari kutoka dar hadi Dom ni cha kizarendo sana hata kama ni Mimi sikubali kutumia gari wakati Chopa zipo Rais sio mjinga kama mnavyomfikiria nyie anamaana yake kufanya hivyo tuheshimu maamuzi haya ndugu zangu.
 
Kuna kitu nakiona hapa hii mishitukizo ya Magufuli wengi hawakuitarajia, Na mbaya zaidi wengi wao huenda ni waathirika kwa haya maamuzi ya Magufuli.

Sio kwamba wanapinga kwa sababu Magufuli anakosea hapana... Wanapinga ili kulinda tabiri zao!

Kwa hali hii Magufuli atawaacha mataa kwa kila hatua!
 
Tangu ajAli ya sokoine .kitengo cha ulinzi wa viongozi idara ya usalama sijawahi kusikia wakichukua option ya kumsafirisha Rais ,Makam au Pm kwa barabara ukiacha wakati wa kampeni ya kuomba kuchaguliwa Tena ...
Ni risk kumtembeza Rais wa Nchi kilometers 600 ...kwa gari wakati tunazo Ndege ...helicopter kwa kazi Hio ..pia ni gharama kubwa ,usumbufu na Muda ...
 
Kusafiri na gari si mabadiliko ni taratibu tu za kawaida. Alipokuwa katika kampeni alisafiri kwa gari pia

Mabadiliko tunayosema ni ya mfumo mzima wa utawala. Kule ZNZ chama chake kimegomea matokeo.

Mabadiliko yalikuwa kuanza kuwaasa wahafidhina wa znz wakubaliane na maamuzi ya wananchi

Mabadiliko si peremende jamani, huyu ana wiki 2 tayari mnaamini anaanza na mabadiliko!

Tumeyaona kwa JK alipotembelea masoko, ameondoka masoko ni mabovu kuliko alipotembelea

Alienda magereza tukaambiwa ni nguvu mpya, hadi leo miaka 10 tunasubiri nguvu mpya

Ipo mifano mingi, hoja hapa ni kuwa hili lisiwe tukio la maana sana tukijua kuna mambo muhimu sana

Tusiwe watu wa kulishwa peremende na kusahau mambo yanayoligusa taifa.

Hakuna mabadiliko kama taifa limegawanyika tena katika misingi mibaya sana

Hakuna kiongozi anayefanikiwa akiwa mwenyewe, akiwa na Taifa lisilo na umoja wala maridhiano

Hatuzungumzii kwanini tumefika mahali watu wanatoana roho kwa siasa.

Yaani siasa imetufikisha hapo hatuoni kama tatizo. Hatuoni kuwa ni tatizo kubwa sana katika jamii

Tunaona mabadiliko ni mtu kusafiri kwa gari! please lazima tuone umbali mrefu zaidi ya piua zetu

Hili si tukio la kuthibitisha mabadiliko, ni sehemu tu ya majukumu ya kawaida akienda na kutoka kazini

umechoka mzee, ishia zako mzee umekuwa mtoto unaivishwa pampers.
unataka kila kitu kiwe kime kamilika ndani ya wiki mbili tu? kwenye miaka 5 hoja hizi yeyote utakaye mpekekea lazima atakudharau atajua kabiswa unaongozwa na siasa za chuki fitina hinda, na kila ovu.
 
Nimeskia ana matatizo ya moyo kupenda nchi take na wananchi wake, akipanda ndege hovyo na kulitia hasara Taifa atateseka sana.

Hata alipokuwa minister ilikuwa nadra Sana kwenda nje ...mnajuwa kuna watu tu huwa na hofu ya Ndege ........Tena ukizingatia Tena lie helicopter ya jeshi ilivyowapindukia yeye ...makamu ,Rc na Kova wakati wa mafuriko

Wakati wa kampeni aliavoid Sana helicopter Pamoja na kuwa ccm walikuwa Nazo nyingi...

KUNA KITU NAMSIFU LOWASSA KWA USTAARABU ..PAMOJA NA KUYAJUA FIKA MATATIZO BINAFSI YA MAGUFULI HATA MARA MOJA HAKUWAHI KUTATUMIA AU KUWAPA CHADEMA DOZZIER WAZITUMIE ...INAONEKANA ANA MIIKO YA KIAPO
 
...Ni risk kumtembeza Rais wa Nchi kilometers 600 ...kwa gari wakati tunazo Ndege ...helicopter kwa kazi Hio ..pia ni gharama kubwa ,usumbufu na Muda ...
Nyinyi "wasomi" wa upinzani tangu Ukawa washindwe uchaguzi akili zenu zimetetereka sana. Kila kukicha mnazidi kujipunguzia heshima kwa watu tuliokuwa tunawaamini kwa mawazo yenu mbadala. Sawa tu, endeleeni hivyo hivyo.
 
Dr.JPJ Magufuli Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania,anaongoza kwa kuonesha mfano. Hii no kuonesha kwamba c lazima Sana ndege! Ikiwa no pamoja na kujionea hali halisi ya mahali anapopita na kuwashukuru wananchi kwa kumchagua.
 
Kuna utofauti wa muda na cheo, ulikuwa waziri sio rais, ulikuwa muda uliopita ila msafara ni current, inamaana changamoto zitakuwa tofauti kwa kigezo cha muda na uwezo wa kuzishughuliki nao ni tofauti kwa kigezo cha mamlaka aliyokuwa nayo.
Hapana! hoja si kushughulikia, tunaambiwa anapita kutazama na kujionea

Ina maana alikuwa hayajui hayo? Hapo ndipo hoja ilipo
 
Hakuna mwaka ukizitoa hizo week 2, assessment zipo za sina nyingi watu walitumia ya awali kumpa kura, hii wanauomsifia ni endelevu kwahyo usitumie mihemuko yako na chuki ambayo hukuondolea imani juu ya mtu usiyempenda.
Sasa kama ni endelevu mbona tunaambiwa ni mabadiliko? Mbona tunaambiwa anapita barabarani kujionea ubovu wa barabara na misitu inavyochomwa? Kuna kipi alikuwa hajui hapo

#Hapa hoja tu
 
Either way, akitumia ndege bado hayo magari ya raisi yatasafirishwa kwenda Dodoma ili kuzunguka nae. Nadhani amesev japo kila mpinzani anaonekana kuponda tu.

Ina maana huko Dodoma hakuna magari yanayoweza kutumiwa na rais?

Ikulu ya Chamwino haina magari?
 
Hapana, hatuwezi kudanganyika kirahisi. Alipaswa kuanza na mabilioni ya pesa za kwenda kutibu chunusi India. Kutumia barabara ni kuokoa pesa kiogo sana , pengine sawa na nauli ya mh mmoja kwenda London

Hizi ni stunt za kuamsha taifa baada ya kuona, kuna huzuni, kutoridhika, manung'uniko na taifa limegawanganyika

Anachotakiwa ni kuliunganisha taifa si kuanza na vitu vidogo vidogo vya kumjengea umaarufu wa haraka

Asimame na kuangalia taifa lilipo na ajiulize kama ndivyo wenzake walivyopokea nchi siku za nyuma

Asikimbie ukweli kuwa uchaguzi , kampeni, matokeo n.k. vimeacha makovu makubwa makuba sana katika umoja wa taifa

Huo ni ukweli anaotakiwa kukabiliana nao na si popularity ya vitu vidogo vidogo

Tatizo si spea wala vipuri, ni jinsi taifa lilivyogawanyika na changamoto ya kukosa kuungwa mkono na sehemu ya jamii

Ni jinsi wananchi wanavyoangaliana kwa misingi ya kubaguana, chuki n.k. Jinsi chuki ilivyobobea na kuleta yale ya Geita

Aunganishe taifa hili lililogawanyika kwanza ili aungwe mkono. Kinyuime chake kila jambo analofanya litakuwa Big G


Hilo taifa umeligawanya wewe?

Mtaisoma namba.
 
Nilimaanisha wasaidizi wake wengi wanatumia magari aina hiyo.

Hatutaki wala hatuna haja ya kujuwa ulichomaanisha.

Unachomaanisha/ulichomaanisha wewe kitatusaidia nini sisi zaidi ya wewe kujaribu kutujaza ujinga ulionao?

Tunataka ukweli.

Hivi wewe ni mwandishi wa habari za ukweli? Au udaku?

Wengine huwa hatudanganyiki.
 
Back
Top Bottom