Rais Magufuli: Kama umesoma 'private school' atakayekupa mkopo ni kichaa

Halafu mtu unapambana kujisomesha unaajiriwa bodi ya mkopo wanaanza kufyeka mshahara huku wewe si mnufaika huu ni upuuzi wa hali ya juu
 
Lazima atambue ya kwamba Hela hizo zinazopatikana kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa vyuo ni kodi za wananchi,sasa yeye anataka kujiamulia tu Hvi kuna watu wanashindwa kumshauri rais......naona Hata Bunge linashindwa kuingilia kati Suala hilo!

Ova
Sio kwa bunge hili la sasa ndugu. hakuna wa kunyanyua mdomo labda wapinzani watasema kdg lkn support ya wabunge wa ccm yaiwezi kuwepo kabisa. RIP Mh. S. Sitta.
 
Huwa nastaajabu sana naposikia viongozi wanalalamikia Elimu ya nchi hii, Ajabu ni kwamba ukiwatathimini wao ni wabovu kuliko Elimu yenyewe!!!!
 
Kauli ngumu kama hizi kutolewa na kiongozi mkubwa wa nchi ni hatari sana kwa taifa lletu!
 
Naunga mkono raisi,wacha wale waliosoma kwa shida ndo wawe kipaumbele kwanza,kama kuna pesa zitabaki ndo wapewe hao wa private
 
Mzazi anapomsomesha mtoto shule binafsi ni kwamba anatafuta msingi mzuri Wa elimu ya mwanae!! Ninaposema hili siyo kwamba shule za serikali hakuna msingi mzuri .tumeona shule za serikali sehemu nyingine zikifanya vizuri tu lakini sehemu nyingine ni shida kidogo!!
Ikumbukwe kuwa mzazi huyu anayempeleka mwanae private ana uwezo Fulani kwa wakati Fulani.wazazi Wa namna hii ndiyo walipaji kodi wazuri sana!huyu mzazi eidha ni Mwalimu,mfanyabiasha ,mwajiriwa sehemu mbali mbali,mjasiliamali au hata mkulima!!mzani anajitaidi amsomeshe mwanaye mpaka form six maana Yake mwisho Wa secondary education!! Kwa nini mzazi anaona mwanae sana aliyemaliza secondary education anapoanza tertiary education apate mkopo?
Kwanza mzazi huyu kajikamua vya kutosha na so kwamba ni tajiri sana!!
Pili mzazi huyu wakati mwingine umri umekwenda .anaona sasa ni vyema mwanae apate mkopo ili iwe ahuweni kwake!!kodi ambayo amekuwa akilipa basi imsaidie kumsomesha mtoto wake elimu ya juu japo si bure Bali ni mkopo ambao mtoto huyu atakuwa responsible kuurudisha!!
Mtoto anapokuwa chuo kikuu ni MTU mzima sasa.ndiyo maana hata maswala mengi ya kimaisha yanabadirika ,wengine wanaweza kutengeneza hata familia!!

Kuwabagua hawa watoto waliyosoma private kuwa wasipate mikopo siyo sahihi!! Ni kutengeneza minongono katika jamii!! Ningeshauri wasinyimwe Bali wapewe kiasi Fulani ili kumpunguzia mzazi mzigo Wa kumsomesha mtoto from primary secondary to university!! Kusema kuwa waliyosoma private wasipewe mikopo ni dhana mbaya kwa wazazi kuwa sasa watoto wote waende shule za serikali!!Hapa ni kuua sekta binafsi!!Hatujengi uchumi imara kwa kuua sekta binafsi!! Tunapotengeneza Sera tuwe tunajiangalia sisi ,jamii inayotuzunguka!!
Na linapokuja swala ambalo unaona jamii inalipigia kelele ujue hilo ni tatizo!!kaa chini utafakari how to solve it!! Huo ndiyo utawala bora wenye kusikiliza maoni ya tajiri na masikini yani kuwakumbatia tajiri na maskini!
 
Wote ni watanzania kigezo cha Mikopo ni ufaulu sio umesoma shule gani
1. Ulemavu sio kigezo
2. Kufiwa na wazazi na Uwe na cheti cha kifo sio kigezo
3. Kusoma private schools sio kigezo
N.k.
 
Wenzetu kigezo cha kwanza mtu kupata mkopo ni uwezo wa kusoma (akili), ndio maana wanawapa hata moyo wanafunzi kuwa anayepata alama za juu anapata ufadhili. Sisi vigezo vyetu ndio hivi, kupimana ujinga alafu eti tujenge viwanda!
 
Wote ni watanzania kigezo cha Mikopo ni ufaulu sio umesoma shule gani
1. Ulemavu sio kigezo
2. Kufiwa na wazazi na Uwe na cheti cha kifo sio kigezo
3. Kusoma private schools sio kigezo
N.k.
ni kweli, lakini cake ikiwa ndogo hula maharusi na wazazi na wapambe, cake ikiwa ndogo zaidi, na walaji hupungua mathalan hula maharusi na wazazi tu, cake inapokuwa kiduchu zaidi basi huliwa na bibi na bwana harusi, ..kwa hiyo mimi nadhani wanao andaa cake wanajuwa ukubwa wake kwahiyo ni namna tu ya kuwapunguza;
NOTE; Endapo MKOPO huu utatolewa kwa wanafunz wa govn na ukawa hautoshi kwa hawa kitaangaliwa kigezo kingine cha kuwapunguza tena, wanaweza sema Wasio na bikira hawatapata MKOPO,...Voice!!! katika utawala Wangu asiye na bikira asipewe MKOPO kwa sababu serikali haisomeshi makahaba!!!!
 
Wakisema wasio na bikra hawapati mkopo mbona walishasema serikali haisomeshi wanafunzi wazazi.
 
Wazazi wa private hebu amsheni masikio juu. Nendenu unicef mwonane na mkurugenzi mkazi awasaidie kupata scholorship za vyuo vikuu, Australia China Canada Sweden wanao mpango wa kusomesha watoto wenye uhitaji
 
Wote ni watanzania kigezo cha Mikopo ni ufaulu sio umesoma shule gani
1. Ulemavu sio kigezo
2. Kufiwa na wazazi na Uwe na cheti cha kifo sio kigezo
3. Kusoma private schools sio kigezo
N.k.

Numerically, ninafuu kusomesha mtoto katika baadhi ya private schools kuliko baadhi ya govenment schools
 
ni kweli, lakini cake ikiwa ndogo hula maharusi na wazazi na wapambe, cake ikiwa ndogo zaidi, na walaji hupungua mathalan hula maharusi na wazazi tu, cake inapokuwa kiduchu zaidi basi huliwa na bibi na bwana harusi, ..kwa hiyo mimi nadhani wanao andaa cake wanajuwa ukubwa wake kwahiyo ni namna tu ya kuwapunguza;
NOTE; Endapo MKOPO huu utatolewa kwa wanafunz wa govn na ukawa hautoshi kwa hawa kitaangaliwa kigezo kingine cha kuwapunguza tena, wanaweza sema Wasio na bikira hawatapata MKOPO,...Voice!!! katika utawala Wangu asiye na bikira asipewe MKOPO kwa sababu serikali haisomeshi makahaba!!!!
Wakisema wasio na bikira hawapati mkopo kwa Tanzania watasoma wavulana tu
 
Back
Top Bottom