Rais Magufuli: Kama umesoma 'private school' atakayekupa mkopo ni kichaa

Kuna Wanafunzi wanasoma shule za private kwa sponsorship Katika level za secondary, sasa ukimnyima loans utakuwa hujamtendea haki kabisa. Kwa mtazamo huo wa ankle Magu wengi wataisikia tu Elimu ya Juu. Bila kuifikia.

Sent from my TECNO H6 using JamiiForums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Au mzazi kastaafu na hana kipato tena.
Hivi anayewaambia mzazi akistaafu anakuwa maskini ni nani?Hiyo ilikuwa zamani sio leo,kwa leo labda kama mzazi mipango yake ni mibovu.Mtu upate take home 180m,halafu kila mwezi laki nane halafu bado ubaki maskini,utakuwa kibwetere.
 
Huyu Rais, hajielewi kbsa! Mbona yeye alisomea Private school na bado akapewa udhamini wa Serikali kusoma chuo!? Haya mazee ya zamani inabidi Mungu ayapoteze, tubaki wenyewe wa kizazi hiki ili tuiongoze Nchi kwa mtindo wa Karne hii la sivyo, yatatufanya tuishi km masokwe msituni! Weledi wao ni finyu ktk kuiongoza Nchi, wkt wenzetu wanapiga hatua kusonga mbele, sisi tunarudi nyuma
Huyu mtu ni hatari, kinachosaidia Lisu alisema tusinyamaze tuseme, vinginevyo tungelikuwa na mass graves!
 
Nafikiri wazazi wanaosomesha watoto wao private schools na kodi wasilipe maana ni UKICHAA kulipa kodi halafu mtoto wako anabaguliwa....
Na ikumbukwe si kweli kwamba wazazi wanaosomesha watoto wao shule za private ndo wanapesa!!!
Binafsi nlisoma private school toka Form one hadi form Six na babangu ni mkulima. sasa hiyo inapelekea kuwa mzee wangu ana uwezo sana kwa hiyo serikali isimsaidie? Tena sio kumsaidia maana mtoto anakopeshwa kwa kodi za baba yake1 Kwa nini kuwe na makundi? Why wasiangalie ufaulu.
 
Binafsi huwa namkubali sana Rais Magufuli, lakini sometimes kauli zake huwa zinanisononesha sana, yaani huwa naona hata aibu kum-support nikiwa mbele za watu.

Katika hili Mheshimiwa Rais umekosea sana. Serikali itoe mikopo kwa kila mwanafunzi mwenye vigezo vya ufaulu bila kujali shule aliyosoma.
 
Wekeni akiba za kusomesha watoto wenu, msikae mnasubiria waje kujisomeshe kwa kukopa elimu. Wee mzazi unaejipanga mtoto wako aje kusoma kwa mkopo maanake unakimbia jukumu lako la kumsomesha maana huo mkopo hutolipa wewe atalipa mwenyewe. Kwanini umtie mwanao kwenye madeni wakati uwezo wa kumsomesha unao.

Wabongo tuna shida kweli, tulipoambiwa elimu ya msingi na sekondari itagharamiwa na serikali. Tukasema hatuwezi kupeleka watoto wetu huko maana hiyo so elimu. Ila chuo usipogharamiwa na serikali unaona umenyimwa elimu.
Nakubaliana na wewe kwenye kutokukubaliana, Statement yako ningeilewa kama serikali ingekuwa haitoi mkopo kwa mwanafunzi yeyote! Lakini kama inatoa mikopo kwa nini wengine wabaguliwe? Wazazi wao sio watanzania? Sio walipa kodi? Kwani mkopo ni hisani?
 
Asilimia kubwa ya Watanzania tuko wajinga, wacha maCCM yatuumize mpaka tuisome namba. Tena Mimi naapa namsaidia mama yangu mzazi, wengine sisaidii ng'o. Mitanzania mijinga sana
,,,,,,,,,,,,, nakaribia kukubaliana na ww tunaujinga wa kikondoo kwann viongozi hawataki mijadala ya kitaifa kwa mambo yanayowahusu wananchi wenyewe.

Tunaruhusu maamuzi ya MTU mmoja kufikiri isivyo kwa niaba ya UMMA.

Jana inatoka taarifa ya kituo cha mabasi yaendayo kasi kuwa kuna mabasi zaidi ya ishirini yameharibika kwa maji.

Inaonekana ni jambo la kawaida, wakati ni ufisadi mbaya usiopimika, nani? Hajui eneo lile ni hatarishi.

Haohao wamekataa kuipa kibali Yanga kujenga uwanja kwa Maelezo kuwa ni eneo la bahari KUPUMULIA ,haohao wanajenga stand kubwa .

Hivi ni nani? Katuloga.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Kauli ya Mh. Raisi Dr. John Pombe Joseph Magufuli kuwa waliosoma shule za private wasipewe mikopo inaleta ukakasi kwa sababu inajulikana watoto wake wamesoma/wanasoma shule za binafsi. Yupo mmoja yule aliyepata umaarufu akiwa UDOM ajulikanaye kwa jina la Jesca huyu alisoma St. Methew's Secondary iliyoko Kongowe nje kidogo ya Dsm kuelekea Mkuranga.

Swali la kujiuliza huyu alipokuwa chuoni hakupewa mkopo? Au yeye Magufuli anataka watoto wa wenzake wasipewe mkopo ila wa kwake wapewe?
 
Vilaza walifukuzwa UDOM yeye alibaki.
 
Shule za Kata Kwanza, hutaki hama nchi!
 
Back
Top Bottom