Los técnicos
JF-Expert Member
- Sep 14, 2014
- 3,010
- 2,604
1. Unaenjoy maisha ya ulaya kwa sababu ya democrasia yao.Sielewi tatizo lako ni nini? Kama inakupendeza kunuita mimi mshenzi basi endelea kujiridhisha ni uhuru wako na nchi yako. Tukubaliane kwa hilo! Sawa?
Look! Mimi nilifikiri tunamjadili Tundu Lissu kuhusiana na sifa zake za kugombea Urais, kitu ambcho sikujua, naona sasa tatizo liko kati yangu na watanzania wanao dhulumiwa na serikali ya Magufuli, si ndiyo?
Sikiliza mkuu mimi huwa sipendi kukwaruzana na watu au vijana kwenye mitandao ambao kwa sababu yoyote ile hawaja weza pata bahati kama yangu. Kulingana na status yangu sioni kama kuna haja ya kukwaruzana na wewe, kwani naona kuna tatizo ambalo wewe na mimi hatutaweza litatua kwa matusi kwa vile hatuna kitu chochote in common.
Kama nitakuwa nimekukwaza wewe binafsi au familia na ndugu zako basi naomba niwie radhi. Sina malengo ya kuwakwaza watu ambao wanahangaika kutafuta riziki zao kwa shida.
Kwa kukujibu swali lako la kwanza, mimi nilienda Ulaya kwenye miaka ya late 80's kusoma baada ya kufaulu vizuri masomo ya Science. Sasa sielewi mwenzangu umesomea nini?
Nilivyokuwa masomoni Ulaya of course kila mtu anayafurahia maisha ya huko. Kila kitu unakiona kizuri kwa sababu tumelelewa kuamini hivyo. Baadae ukisha anza kazi na kuyazoea mazingira na pesa kidogo ya uhakika, ni kweli uko right, mtu unapotea na kujisahau kabisa. Maisha ya watu wa kwenu huyafikirii tena na unajiona wewe nawe ni mzungu kama wao.
Kwa kukuthibitishia tu hata hivyo mimi bado ni mtanzania na wala sikubadili uraia wangu. Nina miaka saba toka nirudi na Rais Magufuli ama kwa uhakika nilimpigia kura mwaka 2015 na nitampigia tena kura Oktober 28 2020.
My Moto is "No Time for Change and No Time for Experiment". Nataka Magufuli amalize mambo aliyo yaanza kwanza, ndipo tufanye majaribio.
Advantage niliyo nayo dhidi yako ni kwamba mimi nina uwezo wa kwenda Europe mda wowote ule ninao taka, kwani nina unlimited visus na watoto wangu na mjukuu wako huko. Utanisamehe kwa hili, kwani tumejifunza kwenye methali zetu kuwa bahati ya mwenzio, usiilalie mlango wazi.
Fanya bidii na wewe milango yako ifunguliwe, kwani kukaa gizani kwa mda mrefu sioni ajabu kama mtu anakuwa na frustrations za kupofuka macho.
Ungejua jinsi gani nimewapigania vijana na watu wa Bongo kwenye mada yangu, nadhani nisinge kuwa mkimbizi kwenye nchi ya mababu zangu. Ama kweli kusoma kunafungua akili.
2. Anayeishi nje hawezi kuzielewa changamoto za watumishi hapa nyumbani
Elimu yako nzuri uliyonayo haijawahi kukusaidia kufanya utafiti kuelewa kwa nini wengi wa watanzania kwa sasa wapo namna unavyowaona, Kwa kuwa wewe unashiba huko ulaya kwa wenye sera makini juu ya wastaafu, watumishi wa umma na maslahi yao kiasi kwamba hao wazee wanaostaafu hawawi mizigo.
Hawa wa kwetu wanakuwa ni mzigo kwa sisi vijana badala walipwe pesa zao ziwasaidie uzeeni, serikali imetumia fedha zao katika jenzi za madaraja, vijana mishahara yetu midogo isiyotosha bado tugawane na wazee wanaodhulumiwa na mifuko iliyofilisiwa na serikali.
Kwa kuwa hujafanya utafiti kamwe hutauelewa ushenzi ulioubeba kwa mujibu wa madai yangu.
Sina muda wa kukujibu tena, endelea kuinvest elimu yako ulaya huna haja ya kutupigia kelele kodi yako iko ulaya, binafsi na wenzangu kodi zetu ziko hapa nchini na tunanyanyaswa na Rais Magufuli