Rais Magufuli awateua Abdallah Bulembo na Prof. Palamagamba Kabudi kuwa Wabunge

Hii ni asante kwake kwa kumpigia campaini wakati akigombea urais. Ijapokuwa Ni haki yake kikatiba ILA busara ilitakiwa kuangaliwa kwanza. Ilikuwa si lazima amteue kuwa mbunge then uwaziri. Ninafikiri kuna tatizo kwa washauri wake au yeye anatatizo na washauri wake. imeleta taswira mbaya.
 
Kabudi mwanasheria wa kanisa la Anglican kwa askofu mokiwa na mshauri Mkuu wa sheria wa bwana yule.

Nadhani mwakyembe atapisha njia pale wizara ya sheria NA muda si mrefu mabadiliko ya Baraza la mawaziri yanakuja.

Kwa kuwa bwana yule pia watu wa madini na nishati wanamtikisa,anaweza pia kumuweka kabudi.

Pia anaweza kumwacha kabudi achuane na tundu lissu japo navyojua kabudi atataka uwaziri kwa kuwa huwa hakubali nafasi za chini.

Kabudi pia anaweza kuwekwa ofisi ya makamu wa rais mazingira na kumuondoa January makamba,ambae nadhani hayuko comfortable sana NA hii awamu,kabudi ni mtaalamu wa environmental laws na kwa kuwa masuala ya muungano ni ya kisheria zaidi NA kabudi ni mwanasheria

Nahisi nape atampisha bulembo
January ni mchakachuaji mkuu wa chama pia mtaalam wa fitna na kamati za Ufundi wa CCM,bila January leo hii mkulu asingekuwa ikulu ni vigumu kumwondoa tena sana sana January anaweza kupewa wizara yenye Ulaji, na mwakyembe ni rafiki mkubwa wa magu tokea zamani ni vigumu amtumbue hata akijisaidia ofisini hawezi kumtumbua.
 
Mh.kila siku unasisitiza usawa kwa Wote Lakini naona nitofauti na unachomanisha.
Leo hii familia moja inawabunge wawili tena Baba na Mwana bora Hata ingekuwa shemeji.
Watanzania tulikuwa tunapinga kitendo cha Chadema kupeana vyeo hivyo Hasa familia yangu Ndesamburo Kuwa Baba, Mama na mtoto Kuwa wabunge au Tundu Lissu na Dada yake Kuwa wabunge au Dr. Slaa na mke wake Kuwa wabunge.
Kwahiyo bungeni patakuwa familia ya bulembo.
Mh. Raisi Kama nafasi zilikuwa zimebaki ungeangalia Hata mtoto wa maskini aliyemaliza chuo kikuu Hata Kama ni kada WA chama chako, utakuwa umesaidia kuondoa umasikini katika familia ile.
Mh. Tafakari Sana katika hili umetuangusha Watanzania,kama ulikuwa na nia Ya kumpa kazi Mara mia Hata ungemteua ubalozi au ukurugenzi Lakini si kwa kitu ulichofanya Leo kwenye Watanzania milioni 50 umekosa kabisa....!!
Baada ya kuona katoto kanachepuka sana kule Bungeni Dodoma ndipo wamebuni mbinu ya kumpeleka baba amlee binti yake mpaka aoelewe na CCM wenzake asije kutumbukia kwa Wapinzani.
 
Rais anatakiwa aombewe tu,wananchi kazi yenu ni kumwombea rais tu zaidi ya hapo ni uchochezi.
Fasheni mpya ni kila RPC ,OCD kuchukua Ujiko kusaka vyeo kwa kupitia chadema,wanajua kuwa wakiwapiga mabomu chadema mkulu atawapa vyeo sana,hivyo wanachama wa chadema kuweni makini na polisi kwani chadema imekuwa njia ya know jipatia sifa na vyeo.
 
prof .kabudi
alikuwa na msimamo mkali sana juu ya katiba ya wananchi ya warioba ..
sasa hii ya kuteuliwa tuielewe kuwa mchawi mpe mtoto akulelee au mtoto akilia njaa mpe pipi atatulia hata sijui..
ila kwa uzoefu wangu tunaenda kumpoteza kabudi kama mtetezi wa katiba ya wananchi soon atapewa uwaziri na hio itakuwa mwisho wake kusimamia katiba ya wananchi
rejea.humphrey polepole.mzee warioba kapewa ukuu wa chuo.na sasa kabudi ataenda kupewa uwaziri
..hii ni kuizika kabisa katiba ya wananchi
 
Mpaka maghufuli amalize siasa zake 2020 UDSM itakua imepukutika yaani wanachukuliwa majembe yanaachwa vuvuzela akina Bunsen burner sorry Benson Bana.
mkuu
hii ni shida kweli.....mwishowe watu wote ambao ni potential watamalizika kibaya zaidi huko waendako hawaendi kuongeza tija yeyote zaidi ya kumpigis makofi mshereheshaji
 
Naiwaza KATIBA ya mzee Warioba tu hapa!
mkuu
tulie tu na kuombolezwa..kuna jitihada kubwa ya kuua nguvu ya wapishi wa katiba ys warioba..
ukianza na warioba mwenyew tang ateuliwe basi katiba kaitupa huko

huyu kijana humphrey polepole.tqng ateuliwe basi kaachqna na katiba zimebaki propaganda.mara ooh ntazungumza ndani ya chama oooh msimamo wang haujabadilika..very cheap


sasa na prof .kabudi nae ndo huyooo anaelekea huko hatua itayofuata ni kupewa uwaziri huko hutamsikia tena akipigania katiba hasa serikali 3
 
Back
Top Bottom