Uchaguzi 2020 Rais Magufuli atakavyowageuka CCM, Ndugai hatarudi, nawaambia mnielewe!

Tila-lila2

JF-Expert Member
Oct 20, 2019
653
1,058
Ninavyomjua Dkt. JPM ni mtu mwenye huruma na pia hupenda kupendwa na kusifiwa. Magufuli hapendi atokeze mtu hata mmoja ambaye huonesha kutopendezwa naye. Ndiyo maana ukimwomba msamaha mnamalizana. Kwangu mimi ukisikiliza sana wote walio upinzani utagundua hata Mbowe mwenyewe hajawahi kumshambulia JPM personally kama JPM bali mara chache huongelea taasisi ya URais - hivyo basi nina uhakika JPM hamchukii Mbowe kivile kama Ndugai na wafuasi wake vigeugeu kama akina Silinde na Juakali wanavyoamini. Mbowe ni mwanasiasa anayefanya siasa za kistaarabu na anajua kuna maisha pia baada ya siasa - pamoja na kuonewa kote kule. Jeshi la Polisi pia limeonesha uonezi wa waziwazi jana baada ya kutoa taarifa ya HOVYO kuliko zote ambazo wamewahi kuzitoa wakiunda maneno ya akina Ndugai, Silinde na Juakali kuwa taarifa ya Polisi. Ukweli wananchi tunaangalia tu.

Kina Silinde , Juakali na Team Jipendekeza wamejenga chuki kubwa sana miongoni mwa wanasiasa. Wameonesha ni vigeu geu sana. Wenzao wameitwa TAKUKURU kwa sababu yao. Hebu tutafute tu kwa ukweli wa mioyo yetu ni kitu gani kibaya Mbowe binafsi au CHADEMA waliwatenda hao watu? Uamuzi wa kuwazuia wasiingie bungeni ndiyo kweli umeleta mambo yote hayo? Hata kama ulikuwa ni uamuzi mbaya ndiyo kweli ulete maneno yote yale? Kweli? Ninaamini leo hii hata watoto wao hawawezi kuja jivunia yale waliyokuwa wakiyasema hawa watu pale bungeni - tena kulia lia kwa Juakali ndiyo hovyo kabisa!

Kikubwa ninachoweza kuwahakikishia mijadala hiyo kwa JPM najua hajaichukulia kivilee kama wanavyofikiri. Uropokaji wa Ndugai akiungwa mkono na hao watu tayari umeshamfadhaisha mno Magu. Ameshaona hawa mabwana wamefanya kuliko vile ilivyotarajiwa, wamezidisha chumvi. Ndugai ana maagizo ya kudhibiti upinzani lakini sio kuangamiza upinzani. Ana maagizo ya kuwafanya wapinzani wampende JPM lakini sio kuwaongezea chuki zaidi dhidi ya JPM. Ukweli JPM hapendi kuchukiwa au kupingwa lakini hata wale wanaompinga iwapo wanampinga kwa upendo yeye hana tatizo kabisa. Kina Ndugai wamesababisha baadhi ya wapinzani wampinge JPM kwa nguvu sababu ya kuchochewa naye kama Spika na watu kama kina Silinde na akina Mollel sijui. Hawa watu waliotoka upinzani wamezidi kiwango cha maagizo. Na hawa waliohama juzi ndiyo wametumia nguvu zaidi bila kujua kuwa wanajichora tu na hawatapata kitu tena CCM - ndiyo kwishney hao!

Wakati wa Kampeni JPM anajua tayari anazo kura za CCM baadhi hivyo atazitaka kura za wapinzani. Kumbuka hapendi kutopendwa na atataka awapendezeshe hao ambao ni wachache wanaompinga ambao ni upinzani. JPM ataomba kura zao dhidi ya Tundu Lisu, Zito Kabwe au mwingine yeyote atayewekwa na upinzani. Atajisimamia mwenyewe ataona heri yeye apate kura nyingi kuliko hata wabunge wake. Mwaka 2015 kama mtakumbuka aliomba kura za wapinzani. Mwaka huu atafanya zaidi kwa sababu hana cha kupoteza - ni muda wake wa mwisho huu - atakuwa makini sehemu ambazo zina upinzani sana atajishusha apate kura zao. JPM ni mtu wa mahesabu, anajua atafanya nini.

Magufuli kishaona wanaomhariabia ni waliomo ndani ya CCM kwenyewe - Ndugai anamharibia sana. Mfano jana alivyoshindwa kabisa kumlinda yule mbunge Yosepha Komba. Yaani uonevu wa wazi wazi. JPM hata yeye kama kaangalia kamjadala kale nina uhakika ameona Ndugai alivyofanya uonevu. Yule mbunge ni kweli kaonewa sana sana. Nina uhakika pengine walimdharau ama kwa umri wake ama kwa kuwa ni wa upinzani. Ndugai ama haelewei kama ana nguvu kubwa sana ama hajiamini km bado hajampendezesha Rais kwa hiyo anazidi kuua tu mende kwa bunduki. Hayupo rational hata kidogo. Kessy alivyoongea kuhusu Rais kuongezewa muda Ndugai akaruka ruka na kumhakikishia kuwa hiyo hoja ailete bunge lijalo la 12. Kazi kweli kweli! Kessy mwenyewe hatarudi tena. Mtaniambia!

Kwa hekima za JPM najua ataacha mambo yaende kama kawaida, amemhakikishia Ndugai ubunge lakini kwenye USpika nina uhakika Ndugai harudi na kwenye ubunge nina uhakika Lijuakali na Silinde hawarudi. Watabaki makapi very soon. Kwenye ubunge Mbowe atarudi akiwa imara zaidi na ninaamini kuna maajabu Rais atayafanya CCM hawataamini. Wananchi wake hata kama ni wapinzani wake kisiasa Rais anawafahamu kuwa hawana roho mbaya kama ambayo Ndugai na vibaraka wake wanataka kuonesha. Rais anachukua sana ushauri wa wapinzani na kusikiliza mijadala yao na kuifanyia kazi na anajua anayafanya yale mema ya upinzani na ndiyo yanamfanya apendwe zaidi na kuonekana anafanya vizuri. Hachukii upinzani kama Ndugai na watendaji wengine wa Serikali wanavyofikiri

Karibuni Idukilo tunywe kahawa Kijiweni!
 
Tumeipenda Wenyewe Wala Hatukuandikiwa Barua Acha Ituue!!
Potelea Pwete.
 
Mbunge anayeshindwa kumtii spika na kuanzisha ligi kwa kutozima mike yake huku akijua ni kosa huku akisema mama huyu nita deal naye nje.

Hivi huyu naekaonewa?

FB_IMG_1591479815656.jpeg
 
Ikiwa Ndugai atawania ubunge na akashinda ni wazi atapewa uspika. Ndugai amekuwa mwaminifu na mtiifu kwa Raisi,ni wazi Raisi atapendelea kuwa na Ndugai mtu anaemuelewa kama spika kuliko mtu mpya.
 
kila kitu kwenye siasa either uwe chama tawala ua upinzani, kurudi kwa Mbunge yoyote inategemea mtazamo na mawazo ya magufuli.
 
Bahati mbaya sana siwezi kuwa Rais Magufuli, ila kama ni mimi ningrfanya yafutayo ambayo yataacha funzo na kumbukumbu takatifu kwa vizazi vijavyo;.

Kwanza nisingemrudisha kiumbe yoyote aliyekimbia upinzani kwa kisingizio cha kuunga mkono juhudi za Rais..watu hawa kwanza kama hiyo ndio hoja yao maana yake hawana maono yoyote yale, kuanzia mwaka 2015 walishindwa nini kuona dira ya Rais Magufuli kuanzia hotuba ya kwanza tu ndani ya Bunge wasubirie mwaka 1,miezi michache kuelekea uchaguzi mkuu? Jibu hawa ni wahuni wa kisiasa na kama Rais atalijua hili awapige chini watakuwa hawana cha kusema na kama atatokea mmoja wao akalalamika Rais Magufuli atakuwa na jibu fupi mno(KUMBE MMEFUATA VYEO NA NYINYI NI BORA KULIKO WENGINE?)

Pili; Rais Magufuli aisuke CCM mpya kwa kuwapa nafasi watendaji na waliojitoa kwa chama chake bila kuwabughudhi wapinzani na kutupilia mbali CCM mazoea wanaojiona bila wao Chama hakiendi, hapa ataepukana na wanasiasia njaa ambao ubunifu wao upo kwenye kuushambulia upinzani ila wasijue jinsi ya kumsaidia yeye kama Rais.

Kama Rais atayafanya hayo atakuwa salama kabisa kwani wengi wao hawawezi hata kwa dawa kurudi upinznai kwani washaharibu huko na hawaaminiki Tena hivyo watabaki ndani ya CCM bila kutaka na pia wengi wao ni mafisadi watahofia kwenda upinzani kama Upinzani nao watakuwa na akili ndogo kurudia makosa ya 2015 kupokea waganga njaa.
 
Apatea ajali kutokana na starehe zake aagize misukule yake isingizie serikali afu useme hajawahi kumattack Magufuli!? Serikali inajiongoza enh? hizi mambo zinachukiza sana.
 
Back
Top Bottom