Rais Magufuli asema anaweza kubadilisha noti kudhibiti wanaoficha hela...

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,862
12,099
Nimepata tetesi kuwa kuna uwezekano serikali ya Magufuli kubadili noti ya sh 10,000. Sababu ni kuhakikisha wale walioficha mapesa ya rushwa na wizi kwenye ndoo na magunia tokea enzi za JK majumbani wakose kwa kuyapeleka.

======

UPDATE:

Sept 01, 2016


Rais John Magufuli leo ametishia kubadilisha noti kama njia ya kuwadhibiti watu wanaodaiwa kuficha fedha majumbani.

Katika kile kinachoonekana kutaka kuwadhibiti watu wanaodaiwa kuficha fedha, Rais John Magufuli amesema kwa mamlaka aliyonayo anaweza kuamua kubadili fedha ili zile zinazofichwa na watu hao wakose mahali pa kuzipeleka.

Akizungumza katika mkutano wa 14 wa mwaka wa wahandisi uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City leo mchana mjini hapa, Magufuli amesisitiza kuwa kauli hiyo ni mahsusi kwa watu walioficha fedha katika majumba yao na kuwataka kuachana na tabia hiyo mara moja ili fedha hizo ziingie katika mzunguko.

Huku akisisitiza kuwa katika utawala wake fedha za bure hazitakuwepo kwa sababu zilizokuwepo awali zilitokana na fedha za wizi kutoka serikalini ambazo kwa sasa zimedhibitiwa, alisema kwa mwendo anaokwenda nao sasa ni ngumu kwa mwananchi kupata fedha bila kufanya kazi.

Hisani: Mwananchi
 
Ni ngumu kubadili pesa nyingi kama unazo nyumbani, ata watu wa benki yako watashangaa utakopokuwa na pesa taslimu nyingi kuliko zilizo kwenye akaunti yako.
Kama watu wanazo nyingi hawajabadilisha mpaka sasa, akimua kubadilisha itakula kwao,
Ukitaka kujua kama serikali ikiamu kitu, nenda kariakoo sasa unanunue kitu kama radio au friji bila risiti, hautafika mbali bila kukamatwa sasa hivi, ni noma tu.
 
Back
Top Bottom