Rais Magufuli apiga Marufuku kuingiza Sukari toka Nje

Kwani nyinyi msipokunywa chai kwa mwaka mzima kwa ajili ya maendeleo ya nchi yenu kuna tatizo! Sasa watakunywa wakina mama Na watoto sawa!? Wanaume tutasubiri hiyo gap tuifidie!,nafikiri tumeelewana! Just a joke but Rais wa sasa amafuatilia kwa karibu mambo si kukurupuka , kama hamjui yaliokuwa yanafanyika kwenye biashara ya sukari mkae kimya ,! Fanyeni utafiti kabla hamjamkosoa mtu
 
Ni kweli tuna upungufu wa sukari hasa kuanzia Feb had June kila mwaka na kwa nia nzuri serikali na wadau was sukari kupitia board ya sukari waliruhusu sukari iingizwe kucover gap hilo.shida imekuja vibali vinatolewa mpaka vinazidi mbaya wakatokea wengine wanapitisha uchochoroni bila kulipia kodi matokeo yake viwanda vinashindwa kuuza kabisa Rais ana nia nzuri kwamba vibali vithibitiwe ili viwanda vyetu vizalishe na kutoa ajira na kwa sasa hamna Jinsi lazima vibali vitoke kwani mpaka sasa viwanda vimefunga uzalishaji mpka june .Uganda nao walikuwa na shida kama yetu lakini kutokana na mikakati mizuri sasa wanazalisha mpaka ziada na wanauza nje kwa nini sisi tusiweze
Sukari kama bidhaa wewe unadhani umuhimu wake ni uwepo wa kiwanda cha sukari tu na ajira au bidhaa yenyewe kuwafikia watumiaji wengi zaidi kwa kutumia vigezo vya kipato cha wengi zaidi.

GNI ya mtanzania kwa mwaka ni $2510 kuna asilimia kubwa wanaishi chini ya kipato hicho tena hao ni waajiriwa wenye familia kwa maana hiyo serikari makini kuna bidhaa basics lazima ihakikishe zinabaki chini hili watu waweze lisha familia zao sukari ni mojawapo; hawa wazalishaji wa ndani ni walanguzi siku zote na sisi wengine tumechoka kulanguliwa kwa ulinzi wa serikari in the name of uzalendo kwa watu wasio wabunifu watu walio na kipato kidogo could not care less who imports the sugar any more all they care for is value prices.

Hivi sukari ikizalishwa Tanzania ikifika kilo sh/5000 bado tuendelee kutumia vigezo vya uzalendo tu wakati kuna watu labda wanauwezo wa kuiagiza na kuuza kwa shillingi sh/2500 huku sasa ndio kutozingatia hali za maisha ya wengine na limitations za mifuko yao.

Muhimu hapa serikari lazima iangalie kwanini inayoingia ni rahisi na yetu ghali na kupambana na mazingira hayo kwanza ya uzalishaji kabla ya kutubebesha gharama zingine wengine atuishi kwa mishahara inayofanana na posho zao.
 
Hatua ya kwanza ni kukidhi soko la ndani baada ya hapo sasa ndiyo wanaweza kuuza nje au pia wanweza kufanya vyote kwa pmj maadamu tu sukari isikosekane hapa nyumbani!
kwan waliokua wanaingiza ni kina nani kuna watu ilikua biashara yao hiyo na wapo serikalin ngj tuone
 
21/2/2016.--BEI YA LEO YA SUKARI KWA ZANZIBAR----->>1600/- cash.
ZAMBIA----->>900/-a/c in tshs.
MALAWI---->>1100/- a/c in tshs.
 
kwan waliokua wanaingiza ni kina nani kuna watu ilikua biashara yao hiyo na wapo serikalin ngj tuone

Hivi wewe unaelewa kwanza maana ya kuwa Raisi wa JMTZ? Mimi nafikiri hivi vyama vyenu vimewapumbaza sana kiasi kwamba hata mnasahau ni nini maana ya kuwa Raisi wa JMTZ, kwa kukumbusha tu Raisi wa JMTZ ndiyo kila kitu na anachosema hakipingwi na yoyote na popote pale ndani ya ardhi ya TanZania, isipokuwa kinatekelezwa tu!
Raisi akisema fisadi huyu apigwe risasi anachukuliwa na kupigwa risasi mara moja hiyo ndiyo nguvu ya Raisi wa JMTZ sasa nakushangaa unapohoji eti ni nani atatekeleza Amri ya Raisi, ndugu acha kabisa Raisi ni mtu mwingine kabisa TanZania!
 
Hivi mnajua figisufigisu ya wenye viwanda vya sukar na wafanyabiashara,tutegemee mfumuko wa bei mkubwa wa bidhaa hii,chai mtaan na vinywaj vingine vitumiavyo sukar vitapanda iwapo serikali haijajipenga na matamko haya ya jukwaan.Tayar wenye pesa zao wameanza kununua sukar iliyopo sokon na kuificha,wengine wameanza kuficha sukar badala ya kuiuza.Tayar wafanyabiashara wameanza kuwasiliana na wafanyabiashara maarum watakaokuwa wakinunua sukar na kuwazibia wafanyabiashara wengine,ili ionekane sukar inayozalishwa ni kidogo hivyo kupandisha bei ya sukar.Serikali isiishie kutoa matamko tu wazijue mbinu za kibepari.Watu wa sasa waelewe haya mambo yalikuwepo enz za nyerere,watu wenye pesa walinunua bidhaa na kuificha,bidhaa ilipoadimika waliileta sokon kwa bei ya juu.
 
Kila mwaka tunakuwa na upungufu wa zaidi ya tani laki moja na elfu themanini, ndipo serikali inatoa vibali vya kuagiza sukari bila ushuru, na pia waagizaji wanapangiwa kuuza sukari hiyo kwa bei iliyopangwa na serikali.
 
Watu ni mazuzu ngoja sukari ifikie 3000/ kwa kilo watu watarudi humu kulalamika, tatizo akili hakuna,
Je viwanda vya ndani vinatosheleza mahitaji?
Sukari ilikuwa inaagizwa nje na bado bei ni kubwa sasa vipi ispo agizwa?

Tunajuaje hawa wawekezaji kama hawatapunguza production ili kupandisha bei?
Tatizo ni uhuni wa wahindi kwenye supply,ndo maana cement ya Pakistan ni cheap kuliko yetu,serikali iwabane wauzaj waache ulanguzi

Hapa kwetu, vitu vinavyozalishwa na viwanda vyetu ni ghali kuliko kuagiza kutoka njee ni kwa sababu hapa kwetu gharama za uzalishaji (umeme, bureaucracy, red tape n.k), inafanya tusisonge mbele, na inakuwa rahisi kuagiza kutoka nje
 
Sukari yenyewe ni kujiongezea magonjwa na afya mbaya na kunenepa tu...mie siifagilii kabisa naweza kuishi bila kuwa nayo.

Jifunzeni kuacha kutumia sukari.
 
General speaking kuhusu hoja yako ya kulinda soko la ndani la chuma pia nadhani kama serikari itafanya hivyo itakuwa inaendelea makosa yale yale ya kuwalemaza wafanya biashara na kukimbia changamoto halisi ya kukuza uchumi so far ukipitia OEC - Tanzania (TZA) Exports, Imports, and Trade Partners tanzania ndio kwanza ina import hizo bidhaa not over $300m dollar sasa hapo unalinda soko gani?
...Kiukweli si kulinda soko la ndani as such, bali ku build internal capacity and to nurture it, sasa tukifika hapo ndio tutajadili kulinda/kuviwezesha viwanda. Maana hatuna uzalishaji wa chuma ghafi. Ila, tuna deposit za chuma.

...Nimeipata hoja yako!

Nchi yenyewe ndio kwanza ina middle class ya 12% (if you ask me I think the percentage is even lesser but then that is another debate looking at different facts), on housing alone dar in shortage ya 3 million homes kwa mantiki hiyo nani atafidia hizo idadi walau kuchangamsha soko? Considering asilimia kubwa ya wajenzi privately ni middle class tena ujenzi wenyewe watu wanadunduliza kwa miaka ina maana bado kuna asilimia kubwa sana baina yetu wasio na uwezo given the estimator of the group in building activity.
...Tunadunduliza kwa sababu hatuna house finance system ya nafuu na inayolengwa kuhakikisha wenye uwezo wa kumiki nyumba wanahudumiwa at competitive prices.

...Tunahitaji hiyo system/infrastructure sasa!
 
...Kiukweli si kulinda soko la ndani as such, bali ku build internal capacity and to nurture it, sasa tukifika hapo ndio tutajadili kulinda/kuviwezesha viwanda. Maana hatuna uzalishaji wa chuma ghafi. Ila, tuna deposit za chuma.

...Nimeipata hoja yako!
I dont know where you see the potential exactly; to me it seems like mission impossible to nature an industry where the segment which is supposed to propel its growth are struggling with the finances to do so. That leaves the government investment as the main consumer; by the way which is the next fact even if you look at NBS data government expenditure on construction is almost twice to that of real estate. Tells you something about home building in Tanzania its not that people are not interested in home ownership rather the finances restricts them not solely on salaries but higher loan rates and government fiscal approach.

We cant compete on international level if we are not willing to invest in modern technology which makes those products cheap elsewhere; this is a country were labour is cheap, primary resources are available locally, that leaves capital investment and sensible business approach which aims to matching the pocket size of the market; challenges which are not a priority nor addressed whenever people talk of protectionism.

Given those circumstance restricting importation of cheap products is not in the interest of the majority of consumers only a few megalomaniac with nationalism interest but then they forgo the realism of many Tanzania income capacity.

...Tunadunduliza kwa sababu hatuna house finance system ya nafuu na inayolengwa kuhakikisha wenye uwezo wa kumiki nyumba wanahudumiwa at competitive prices.

...Tunahitaji hiyo system/infrastructure sasa!
Bila ya kusikia plan na sera za kufanya hivyo mazingira yatabaki kama ilivyo tu huo ndio ukweli wenyewe.

Haya mambo yalikuwa yakisemwa toka enzi za marehemu Mgimwa sijui kwanini ayafanyiwi kazi either huko wanapojadiliana na donors hakuna argument zinazoweza kuwa-convince situation inaweza badilika kwa sera za ndani au vipi lakini kwa sasa ni tatizo ambalo sioni likichukuliwa hatua leo au kesho.

Undeniably i can see the other side of the arguments too reducing bank interest in the country where it currency is not stable could prove to be a disaster in the long run for banks thus they need that margin of safety, bear in mind most of inter-banking loaning is done in dollars.
 
I dont know where you see the potential exactly; to me it seems like mission impossible to nature an industry where the segment which is supposed to propel its growth are struggling with the finances to do so. That leaves the government investment as the main consumer; by the way which is the next fact even if you look at NBS data government expenditure on construction is almost twice to that of real estate. Tells you something about home building in Tanzania its not that people are not interested in home ownership rather the finances restricts them not solely on salaries but higher loan rates and government fiscal approach.
...Nadhani utakubaliana nami kwamba, potential iko kwenye hiyo miradi ya ujenzi ya serikali, sekta binafsi, na kwa kiasi kidogo kwa wananchi binafsi. I mean, kama tunaweza fedha ya most crucial inputs kwenye hiyo miradi ibaki hapa.

...Kuna miradi kadhaa ya miundo mbinu ambayo inapaswa kufanywa, na itahitaji sementi na vyuma vingi tu. Sasa, kiwanda kimoja cha chuma kitaweza kupata soko kwa kuanzia, hapa nyumbani, halafu jingine litapatikana nchi jirani. My point being, kama tunategemea kukua kwa 7% y/y, au na ukiniuliza nitakwambia, tukiweka mambo sawa, we can even go to 10% growth kwa kama 5 yrs in a row.

We cant compete on international level if we are not willing to invest in modern technology which makes those products cheap elsewhere; this is a country were labour is cheap, primary resources are available locally, that leaves capital investment and sensible business approach which aims to matching the pocket size of the market; challenges which are not a priority nor addressed whenever people talk of protectionism.
...Huko wala siendi kwasasa!

...I will not advocate protectionism, but will propose incentives and deliberate actions to see construction materials sector establish a firm hold.

Given those circumstance restricting importation of cheap products is not in the interest of the majority of consumers only a few megalomaniac with nationalism interest but then they forgo the realism of many Tanzania income capacity.
...On the same page with you.

Bila ya kusikia plan na sera za kufanya hivyo mazingira yatabaki kama ilivyo tu huo ndio ukweli wenyewe.

Haya mambo yalikuwa yakisemwa toka enzi za marehemu Mgimwa sijui kwanini ayafanyiwi kazi either huko wanapojadiliana na donors hakuna argument zinazoweza kuwa-convince situation inaweza badilika kwa sera za ndani au vipi lakini kwa sasa ni tatizo ambalo sioni likichukuliwa hatua leo au kesho.
...Ni kweli hatujatekeleza mipango kadhaa up to date. Hope this Admin. will do most of them.

Undeniably i can see the other side of the arguments too reducing bank interest in the country where it currency is not stable could prove to be a disaster in the long run for banks thus they need that margin of safety, bear in mind most of inter-banking loaning is done in dollars.
...I would prefer the market to be left alone. We have regulations in place.
 
...Nadhani utakubaliana nami kwamba, potential iko kwenye hiyo miradi ya ujenzi ya serikali, sekta binafsi, na kwa kiasi kidogo kwa wananchi binafsi. I mean, kama tunaweza fedha ya most crucial inputs kwenye hiyo miradi ibaki hapa.

...Kuna miradi kadhaa ya miundo mbinu ambayo inapaswa kufanywa, na itahitaji sementi na vyuma vingi tu. Sasa, kiwanda kimoja cha chuma kitaweza kupata soko kwa kuanzia, hapa nyumbani, halafu jingine litapatikana nchi jirani. My point being, kama tunategemea kukua kwa 7% y/y, au na ukiniuliza nitakwambia, tukiweka mambo sawa, we can even go to 10% growth kwa kama 5 yrs in a row.
Potential hiko wazi ila kama umepitia kuangalia contribution ya michango baina ya sector kwenye hiyo link http://www.nbs.go.tz/nbs/takwimu/na/QNA_Third_Quarter_2015.pdf potential unayoizungumzia inazuiwa na uwezo na hapa ndio hoja yangu ilipo.

Ndio maana nikaweka facts za chuma tunayo import kuwa only $300m in other words hakuna industry kwa hali ya sasa; kama utaangalia vigezo kupitia potential unayotumia construction yenye mchango mkubwa ambayo ni everything minus non-residential properties wanasema inakuwa kwa asilimia 17.6, mchango wake kwenye GDP ni average ya 12.8% rough estimate with the estimation of tzs/89.1 trillion GDP ina maana mchango wake kwa mwaka ni tzs/11.4 trillioni. kati hizo toa hela za miradi ya barabara, kinachobaki ndio kiasi kilichotumika kujenga madaraja, majengo mingine yenye tija za chuma na hawa ni big spenders kama serikari au wafanya biashara wakubwa.

Housing sector mchango wake kwenye GDP ndio kwanza 2.3% which equates to roughly 2 trillion; katika hizi wachangiaji wakubwa ni raia wanaodunduliza mishaharara yao, wabadhirifu chini ya awamu iliyopita au mashirika yanayojenga sasa kama utaangalia kila mtu source zake za finance utakuta hayo mashirika yana mikopo au rent kwa hivyo hoja ya value unaona ilipo hili kuchochea sector lazima serikari ijaribu kufanya bidhaa ziwe cheaper zaidi kwa sababu Dar tu kuna uhaba wa nyumba 3m nini tatizo uwezo wa kujenga.

Mwisho ukiangalia source of finance mikopo iliyotolewa kwa ujumla ndio kwanza ni 14.3 trillioni kiasi gani unadhani kimeenda serikarini, kwa wafanyabiashara na raia kwenye kujenga au mashirika yanayojenga; tunarudi pale pale uwezo sasa kipi priority ya serikari 'watu kujenga' au 'kulinda industry' ukisema unalinda viwanda vya ndani ambavyo avina biashara yenye mikakati ya value ina maana kutokana na mifuko ya watu chances ni kwamba huo mchango wa ujenzi kwenye GDP utapungua ali kadhalika ukiwaacha bidhaa za bei chee ziingie ndio zitaua viwanda vyetu lakini watu watapata unafuu wa kujenga au kupunguza gharama za maisha. Surely katika mazingira haya serikari inatakiwa kufikiria kuweka mazingira ya biashara kuweza kushindana na nchi zingine ili mtanzania afaidike na ndio sera yenye tija kwa uchumi mkubwa.

Ifike wakati tuseme hawa wafanya biashara watanzania wawe wabunifu na serikari iwache kuwalinda kwenye nchi maskini na mishahara isiyoweza mudu ugumu wa maisha, waje na sera za uchumi zinazoweza kushindana resources tunazo; yes nakubaliana na wewe potential hipo lakini kuonekana inataka kwanza iwekewe mazingira ya kuweza kushindana na dunia kuliko kutaka kuwafaidisha watu wachache ambao ni wafanyabiashara na mabenki kwa gharama za wananchi utaratibu usiofikiria ukuaji wa uchumi unaogusa maisha ya mtanzania.

...I would prefer the market to be left alone. We have regulations in place
I agree but if we want people to take more loans for housing purposes maana hapo ndio potential kubwa ilipo kwakuwa ardhi bado inapatikana. In order to encourage that rates have to be lowered and BoT should assure lenders on the stability of the currency ata kama unataka ushindani at 15%-20% interest atuwezi kwenda mbali; na hawa jamaa wana akili wanajua wateja wao wakubwa ni wafanya biashara na serikari kwa hivyo they're not worried na raia matokeo yake wengi wanabaki kudunduliza na kujenga swala ambalo linachukua miaka kwa mishahara ya leo sasa tena uwaondelee na unafuu wa bidhaa rahisi uo sasa ndio unyanyasaji wenyewe.
 
Potential hiko wazi ila kama umepitia kuangalia contribution ya michango baina ya sector kwenye hiyo link http://www.nbs.go.tz/nbs/takwimu/na/QNA_Third_Quarter_2015.pdf potential unayoizungumzia inazuiwa na uwezo na hapa ndio hoja yangu ilipo.
...Kwa uchumi na mazingira yetu, kama tunataka kuwa na maendeleo -of course na ku grow zaidi- na kukuza zaidi pato la taifa, itabidi serikali iinyanyue sekta ya chuma na kuongeza ujenzi wa miundombinu.

...Tuko nyuma kwenye miundombinu ambayo ni njia ya kukua na kuendelea zaidi. Kuna madaraja, barabara, na majengo kadhaa yanayohitajika kujengwa ili kufungua fulsa na kuboresha huduma za maeneo kadhaa nchini.

...Hii ni potential growth avenue na market for these products. Achilia mbali masoko yanayotuzunguka kama tutakuwa serious enough kuzalisha bidhaa bora zenye bei shindani.

Ndio maana nikaweka facts za chuma tunayo import kuwa only $300m in other words hakuna industry kwa hali ya sasa; kama utaangalia vigezo kupitia potential unayotumia construction yenye mchango mkubwa ambayo ni everything minus non-residential properties wanasema inakuwa kwa asilimia 17.6, mchango wake kwenye GDP ni average ya 12.8% rough estimate with the estimation of tzs/89.1 trillion GDP ina maana mchango wake kwa mwaka ni tzs/11.4 trillioni. kati hizo toa hela za miradi ya barabara, kinachobaki ndio kiasi kilichotumika kujenga madaraja, majengo mingine yenye tija za chuma na hawa ni big spenders kama serikari au wafanya biashara wakubwa.
...Uzuri uliopo ni malighafi ya kuzalisha chuma kuwapo kule Liganga. Hapa ndani, kuna viwanda vya bidhaa za chuma vinaongeza uzalishaji kwa kuwekeza kwenye upanuzi, meaning mahitaji yanaongezeka.

...I don't care that much about what amount we import and what we consume. What i do care about is the potential that remains untapped.

...Hatuwezi kuwa na uchumi wa maana, kama hatutakuwa na viwanda vya vyuma au kiwanda cha chuma cha uhakika! Wachina wanaotaka kuwekeza Liganga, wanategemea kuzalisha 3mil. mts/yr. Ukweli kwa kuanzia wanaweza kuvuta mpaka 1mil. mts/yr na hii wakitegemea soko nje. I would propose a goal of 500k mts/yr to start with, and then grow from there.

Housing sector mchango wake kwenye GDP ndio kwanza 2.3% which equates to roughly 2 trillion; katika hizi wachangiaji wakubwa ni raia wanaodunduliza mishaharara yao, wabadhirifu chini ya awamu iliyopita au mashirika yanayojenga sasa kama utaangalia kila mtu source zake za finance utakuta hayo mashirika yana mikopo au rent kwa hivyo hoja ya value unaona ilipo hili kuchochea sector lazima serikari ijaribu kufanya bidhaa ziwe cheaper zaidi kwa sababu Dar tu kuna uhaba wa nyumba 3m nini tatizo uwezo wa kujenga.
...What about housing finance ya uhakika. Bei za bidhaa tuachie soko. Tukipanga kila bei au kuiingilia, we'll be misallocating resources.

...Usafirishaji bora, umeme wa uhakika, na ku review taxes zinazoihusu hii sekta kutasaidia

Mwisho ukiangalia source of finance mikopo iliyotolewa kwa ujumla ndio kwanza ni 14.3 trillioni kiasi gani unadhani kimeenda serikarini, kwa wafanyabiashara na raia kwenye kujenga au mashirika yanayojenga; tunarudi pale pale uwezo sasa kipi priority ya serikari 'watu kujenga' au 'kulinda industry' ukisema unalinda viwanda vya ndani ambavyo avina biashara yenye mikakati ya value ina maana kutokana na mifuko ya watu chances ni kwamba huo mchango wa ujenzi kwenye GDP utapungua ali kadhalika ukiwaacha bidhaa za bei chee ziingie ndio zitaua viwanda vyetu lakini watu watapata unafuu wa kujenga au kupunguza gharama za maisha. Surely katika mazingira haya serikari inatakiwa kufikiria kuweka mazingira ya biashara kuweza kushindana na nchi zingine ili mtanzania afaidike na ndio sera yenye tija kwa uchumi mkubwa.
...Kulinda viwanda bila malengo maalum na assessment za uhakika kila kipindi, haisaidii. Lakini, kuanzisha au kuwezesha uwepo wa kiwanda fulani strategic, lazima kuwe na mipango ya kukiangalia kinafanikiwa. I don't see it as protectionism. Emirates Airlines is case in point, pamoja na kwamba ipo sekta tafauti.

...Kama unaweza kuzalisha ndani at fair and competitive prices, usipochukua hatua ni uzembe wa hali ya juu. Hamna nchi inajengwa kwa kutegemea imports tu, hata kama ni rahisi kiasi gani. Tusipozalisha na sisi, wapi tutapata fedha za kununua bidhaa toka nje?

Ifike wakati tuseme hawa wafanya biashara watanzania wawe wabunifu na serikari iwache kuwalinda kwenye nchi maskini na mishahara isiyoweza mudu ugumu wa maisha, waje na sera za uchumi zinazoweza kushindana resources tunazo; yes nakubaliana na wewe potential hipo lakini kuonekana inataka kwanza iwekewe mazingira ya kuweza kushindana na dunia kuliko kutaka kuwafaidisha watu wachache ambao ni wafanyabiashara na mabenki kwa gharama za wananchi utaratibu usiofikiria ukuaji wa uchumi unaogusa maisha ya mtanzania.
...Sera zinawekwa, kusimamiwa na kutekelezwa na the establishment, wengine wanapanga wakitilia maanani uwepo wake.

...Kuna vitu lazima ulinde. Muulize mMarekani kuhusu aerospace industry.

I agree but if we want people to take more loans for housing purposes maana hapo ndio potential kubwa ilipo kwakuwa ardhi bado inapatikana. In order to encourage that rates have to be lowered and BoT should assure lenders on the stability of the currency ata kama unataka ushindani at 15%-20% interest atuwezi kwenda mbali; na hawa jamaa wana akili wanajua wateja wao wakubwa ni wafanya biashara na serikari kwa hivyo they're not worried na raia matokeo yake wengi wanabaki kudunduliza na kujenga swala ambalo linachukua miaka kwa mishahara ya leo sasa tena uwaondelee na unafuu wa bidhaa rahisi uo sasa ndio unyanyasaji wenyewe.
...Fundamentals will dictate that.

...Tungetegemea microfinance iokoe jahazi, lakini rates huko nazo ni kubwa. Swali ni kwanini? Sehemu ya jibu inawezapatikana kwenye gharama na risk inayohusiana na mikopo hiyo.
 
...Kwa uchumi na mazingira yetu, kama tunataka kuwa na maendeleo -of course na ku grow zaidi- na kukuza zaidi pato la taifa, itabidi serikali iinyanyue sekta ya chuma na kuongeza ujenzi wa miundombinu.

...Tuko nyuma kwenye miundombinu ambayo ni njia ya kukua na kuendelea zaidi. Kuna madaraja, barabara, na majengo kadhaa yanayohitajika kujengwa ili kufungua fulsa na kuboresha huduma za maeneo kadhaa nchini.
Mpaka hapa tunapoandika serikari na wafanya biashara ndio biggest contributors kwenye hivyo vitu ulivyotaja. Kupitia figures za mchango wa construction on the GDP and given the government budgetary capabilities, the sums which are contributed nadhani its fair to say their expenditure on the sector at the moment is limited by the tither considering other national obligations it has.

Wanunuzi wengine ni wafanyabiashara hawa nao kwa sera za sasa ni ngumu kuongeza volume zaidi ya ukuaji wa sasa unless kama ikitokea wanaokuja na mitaji yao kutoka nje ya nchi given the borrowing environment in Tanzania; wanachi kwenye ujenzi face even the worsen plight when it comes to improving the necessary housing sector leading to high demands of the product.

Kwakuwa hizi factors mbili ndio kwa sasa zinamchango mkubwa wa matumizi ya chuma ili azma yako ifikiwe inabidi wafanya biashara waongezeke na kulipa kodi, pato la serikari likuwa liweze kuongeza kasi ya utumiaji wa chuma.

On the outlook kwa mazingira ya sasaa kunahitajika FDI on new industries au sera rafiki za mikopo kufanya watu wafungue viwanda kwa pace kubwa zaidi. Tupo na catch-22 bila ya kukua kwa viwanda serikari aiwezi pata hela ya kuongeza miradi yake kwa speed zaidi na bila sera rafiki za mikopo wafanya biashara awawezi kukuwa kwa kasi ya kutumia chuma zaidi kwenye ujenzi wao; unless labda tuuze bidhaa kama gesi na madini mengine serikari ipate hicho kipato cha nyongeza hila kwa sasa elimu bure tu kasheshe kutokana na limited budget na ni jambo la msingi pia.

...Hii ni potential growth avenue na market for these products. Achilia mbali masoko yanayotuzunguka kama tutakuwa serious enough kuzalisha bidhaa bora zenye bei shindani.
Hapa ndio tunapokubaliana kipi kinatufaa na kuachana kipi kinahitaji kufanyika kwanza kufikia hayo malengo. Kwa mazingira ya sasa unless tuna matajiri wengi wenye billions to risk wakiwekeza kwa hela zao bidhaa zinaweza zikawa raisi na bei za kushindana; lakini kwa mtu anayekopa bank at 15%-20% awezi kushindana on prices kwa mtu anaekopa at lets say 7% or lower huko kwao hapo ndio competitive advantage inapopotea.

Wafanya biashara wanaoenda kuleta bidhaa huko wanajua watanzania kwa uwezo wao nikipeleka kwa bei chee na wanayopata sokoni kwao nitauza na nina faida. Unless labda wageni waje na mitaji yao ambayo ipo kwa riba chee huko walikoitoa ndio wanaweza zalisha na kuuza kwa ushindani wa import prices.

...Uzuri uliopo ni malighafi ya kuzalisha chuma kuwapo kule Liganga. Hapa ndani, kuna viwanda vya bidhaa za chuma vinaongeza uzalishaji kwa kuwekeza kwenye upanuzi, meaning mahitaji yanaongezeka.
Haya maswala ya resource waziri husika wa viwanda jana asubuhi kupitia star tv alikuwa akiyaongelea na yeye amekiri kuna tatizo la modern machinery to compete kwa unafuu lakini ameacha source muhimu zaidi mitaji ambayo ajaigusia. Hila wao kama wizara kwa sasa wako tayari kualika wawekezaji na amedai apewe mpaka mwezi wa nane tumpime amefikia wapi kwa hivyo sote tusuburi hila kwa maneno yake people are interested in investing in Tanzania sasa kama kwa soko la hapa au kwao tutajua when the time comes.

...I don't care that much about what amount we import and what we consume. What i do care about is the potential that remains untapped.
So do I but for people to consume or even tapping the potential they first need money.

...Hatuwezi kuwa na uchumi wa maana, kama hatutakuwa na viwanda vya vyuma au kiwanda cha chuma cha uhakika! Wachina wanaotaka kuwekeza Liganga, wanategemea kuzalisha 3mil. mts/yr. Ukweli kwa kuanzia wanaweza kuvuta mpaka 1mil. mts/yr na hii wakitegemea soko nje. I would propose a goal of 500k mts/yr to start with, and then grow from there.
Things have changed a lot since then wao wenyewe wana reserve kiasi kwamba wana dump Europe wameshaua viwanda viwili vya chuma UK na kuleta mzozo mkubwa kisiasa kisa importation hata wafanya biashara nchi za nje awajali nani anazalisha bali value pricing and quality of the product kwa hivyo ata kama sisi tutashindana inabidi value na quality iwe kigezo over uzalendo.

...What about housing finance ya uhakika. Bei za bidhaa tuachie soko. Tukipanga kila bei au kuiingilia, we'll be misallocating resources.
I agree but under the circumstances the government institution should focus on affordable homes not and taking the full advantage of the opportunity which the market offers.

...Usafirishaji bora, umeme wa uhakika, na ku review taxes zinazoihusu hii sekta kutasaidia
Hapa tuko pamoja 100%

...Kulinda viwanda bila malengo maalum na assessment za uhakika kila kipindi, haisaidii.
I agree 100%

Lakini, kuanzisha au kuwezesha uwepo wa kiwanda fulani strategic, lazima kuwe na mipango ya kukiangalia kinafanikiwa. I don't see it as protectionism. Emirates Airlines is case in point, pamoja na kwamba ipo sekta tafauti.
Kama hao tunaotaka kuwalinda bidhaa zao zingekuwa hazina price variation ya vile in terms of value kutetea uagizwaji wa bidhaa ni kama uhaini lakini kuwalinda watu ambao hawafikirii value hapo ni kutomtakia mema mtanzania kutokana na kipato chake. Kama na yeye anataka kujenga inabidi afikiriwe pia kulindwa hawa jamaa wanapenda bei za juu sana kwa bidhaa zinazozalishwa ndani hapo ndipo tatizo lilipo.

.
..Kama unaweza kuzalisha ndani at fair and competitive prices, usipochukua hatua ni uzembe wa hali ya juu. Hamna nchi inajengwa kwa kutegemea imports tu, hata kama ni rahisi kiasi gani. Tusipozalisha na sisi, wapi tutapata fedha za kununua bidhaa toka nje?
Ndio hoja yangu pia kama wapo sambamba sawa lakini mtu anaelalamika mwingine nafuu halafu anataka tumlinde yeye wakati yupo ghali sio tija kwa kigezo cha average income ya mtanzania.

...Tungetegemea microfinance iokoe jahazi, lakini rates huko nazo ni kubwa. Swali ni kwanini? Sehemu ya jibu inawezapatikana kwenye gharama na risk inayohusiana na mikopo hiyo.
Moja wapo ni kushuka kwa shillingi kwa hivyo people at BoT need to come up with effective measure to ensure the Tsh can be trusted before reinforcing lowering of the interest rates.
 
Baada ya malalamiko ya muda mrefu juu ya utoaji wa vibali vya kuingiza sukari nchini. Rais magufuli amepiga marufuku vibali hivyo kutolewa.

Rais amemwagiza Waziri Mkuu asitoe kibali chochote cha uingizaji wa sukari toka nje ili kukuza viwanda vya ndani na kuvutia wawekezaji wengine kufungua viwanda vya bidhaa hiyo.

Mzee Pinda enzi yake alivitoa kama njugu.
Hapa kuna HUJUMA???
 
Attachments

  • 1456378300622.jpg
    1456378300622.jpg
    9.9 KB · Views: 36
Back
Top Bottom