Rais Magufuli anawaapisha Mabalozi na watendaji wa Serikali aliowateua hivi karibuni

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,138
RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI ALIOWATEUA - IKULU DSM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli awaapisha Viongozi mbalimbali aliowateua tarehe 20 Septemba, 2019

1.Bw. Loata Sanare kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro. Bw. Sanare anachukua nafasi ya Dkt. Kebwe Stephen Kebwe ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

2. Bw. Tixon Tuyangine Nzunda kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (anayeshughulikia Bunge na Waziri Mkuu). Kabla ya uteuzi huo Bw. Nzunda alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI (aliyekuwa akishughulikia Elimu)

3. Dkt. Ally Possi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Possi alikuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali.

4. Bw. Gabriel Pascal Malata kuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali. Kabla ya Uteuzi huo, Bw. Malata alikuwa Kamishna wa Kazi katika Ofisi ya Waziri Mkuu.

5. Bi. Mary Maganga kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango (anayeshughulikia Utawala). Kabla ya uteuzi huo, Bi. Maganga alikuwa Kamishna wa Bajeti wa Wizara ya Fedha na Mipango.

6. Mhandisi Anthony Damian Sanga kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji. Kabla ya uteuzi huo, Bw. Sanga alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira wa Jiji la Mwanza.

7. Bw. Alphayo J. Kidata kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara. Bw. Kidata anachukua nafasi ya Dkt. Jilly Elibariki Maleko ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.

8. Mhandisi Emmanuel Kalobelo kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro. Kabla ya uteuzi huo Bw. Kalobelo alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na anachukua nafasi ya Bw. Cliford Tandali ambaye amestaafu.

9. Dkt. Khatibu Kazungu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro. Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Kazungu alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na anachukua nafasi ya Mhandisi Aisha Amour ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.

10. Dkt. Mussa Julius Lulandala kuwa Balozi

11. Bw. Stephen Patrick Mbundi Kuwa Balozi

UHAMISHO.

Mhe. Rais Magufuli amefanya uhamisho wa Wakuu wa Wilaya wawili ambapo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mkoani Mara Mhandisi Charles Kabeho amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato Mkoani Geita,

na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato Mkoani Geita Mhandisi Mtemi Msafiri Simeoni amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mkoani Mara.

Mhe. Rais Magufuli amefanya uhamisho wa Naibu Makatibu Wakuu wawili ambapo aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Nicholaus Merinyo William Mkapa amehamishwa na kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Mathias Bazi Kabunduguru amehamishwa na kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, TAMISEMI (anayeshughulikia Elimu).

MABALOZI. Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Mabalozi 12 watakaoiwakilisha Tanzania katika vituo vya Abu Dhabi (Falme za Kiarabu), Bujumbura (Burundi), Brussels (Ubelgiji), Cairo (Misri), Harare (Zimbabwe), Kuwait City (Kuwait), Pretoria (Afrika Kusini), Riyadh (Saudi Arabia), Tokyo (Japan), Umoja wa Mataifa - Geneva (Switzerland), Umoja wa Mataifa – New York (Marekani) na Abuja (Nigeria).

Walioteuliwa kuwa Mabalozi kwa ajili ya vituo hivyo ni Bw. Mohammed Mtonga (Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali Mstaafu),

Bi. Jilly Elibariki Maleko (aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara),

Dkt. Benson Alfred Bana (ambaye ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam),

Meja Jenarali Mstaafu Anselm S. Bahati, Prof. Emmanuel D. Mbennah (ambaye ni Makamu Mkuu wa Chuo, Chuo Kikuu cha Mtakatifu John),

Bi. Maimuna Tarishi (Katibu Mkuu Mstaafu),

Meja Jenerali Mstaafu Gaudence Milanzi (Katibu Mkuu Mstaafu),

Bw. Ali Jabir Mwadini (ambaye ni Kansela Mkuu, Ubalozi Mdogo wa Tanzania-Dubai),

Dkt. Modestus Francis Kipilimba (Mkurugenzi Mkuu Mstaafu, Idara ya Usalama wa Taifa),

Bw. Jestas Abuok Nyamanga (Mkurugenzi wa Ulaya na Amerika, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki),

Prof. Kennedy Godfrey Gastorn (Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya Ushauri wa Kisheria wa Asia na Afrika - Asian-African Legal Consultative Organization) yenye Makao Makuu New Delhi, India.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli aliwapandisha vyeo na kuwateua Maafisa 3 kuwa Mabalozi.

Wateule hao ni Bw. Stephen Patrick Mbundi ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulinzi, Siasa na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,

Bw. Ali Sakila Bujiku ambaye ni Msaidizi wa Rais na Dkt. Mussa Lulandala ambaye ni Msaidizi wa Rais.

Mabalozi Wateule hao wataendelea kutekeleza majukumu yao hapahapa nchini na wataapishwa


Zoezi la kuapisha limekamilika

Mambo muhimu:
1. Rais Magufuli ameshtukia upigaji mkubwa uliotaka kufanyika katika ujenzi wa mandhari ya Coco beach ashangaa 14bilioni wanataka kujengea nini wakati sheria za ujenzi wa beach unajulikana.
Rais ameshangaa Meya kwenda kumkabidhi mradi mkandarasi na ameuliza meya na ukandarasi wapi na wapi?.....pia amehoji uwepo wa mkuu wa mkoa wakati yote haya yanatokea....."....na mkuu wa mkoa yupo anaangalia tu!!!" alishangaa Rais Magufuli.

2. Rais Magufuli ametoa ombi kwa mahakama kuwafikiria wahujumu uchumi ili wale watakaokiri makosa na kutubu warejeshe fedha walizofisadi na kusamehewa

3. Amewataka wateule wa mkoa wa Morogoro wakachape kazi kwani mkoa ule una changamoto nyingi sana
 
Karibu

Up dates;
Vipi usharudi kutoka mazishini mbeya?
tapatalk_1569129196473.jpeg
 
Back
Top Bottom