Rais Magufuli amsimamisha kazi Mkurugenzi Muhimbili

Hao watu siyo wakuonea huruma, nayeye hadi masimamishe kunavitu kaviona viko hovyo
Wapewe funzo maana haohao ndo wanamaduka ya dawa lakn eti hospital hazipo, ukiendekeza sana vitu vya kipuuzi kwa viongozi wananchi ndo tunaumia.

Maamuzi ya kukurupuka. utumishi wa umma sio hvyo! Taratibu rais wangu. usijefanya kama enzi za samaki wa magufuli, leo hii ni maumivu kwa serikali!
Kila unayeona anatetea maovu yanayofanyika kwenye idara za serekali,ujuwe yeye yuko kazini na tabia zake ndio hizo.Kama mumo kwenye maovu jirekebisheni,wananchi tunapata tabu,wakati mumekubali kufanyakazi,na unalipwa kwa ajili yetu,lakini hamtupi huduma nzuri.Asante Rais wetu,kura yangu haikupotea bure.
 
Bora JK kuliko Lowassa, naona hata akiitisha maandamano hakuna atakayekwenda, Magufuli amenoga ile mbaya. Ndo maana JK alisema Magufuli akishinda atalala usingizi
Usiusemee moyo. Plus, hatujapiga hatua kwenye safari ya miaka mitano. Tusishangilie kona tukidhani ni goli. Counter-attack moja tu itakuwa vilio. Tusubiri huku kila mtu akifanya lake limpasalo.
 
Amempa fursa ya kujieleza? Ikitokea kuwa serikali ndio haikupeleka fungu, atamrudisha kazini? Utawala bora hauko hivyo.

wimeota kuwa utetezi wake mkurugenzi atasema barua toka katibu mkuu ilielekeza pesa ziende kwenye kampeni zake! Apa ndo atakaa chini
 
Rais wa Jamhruri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Pombe Magufuli ameifuta BODY YA AFYA MUHIMBILI na kumsimamisha kazi MKURUGENZI MKUU wa HOSPITALI hiyo
Source ITV.
 
hii fukuzafukuza bila utaratibu inanipa hofu. kuna hatar likiwa kama lile la meli ya uvuvi bahari ya hindi. ni vizuri maelezo yakatolewa kisa cha kusimamishwa huyo mkurugenzi...
 
No one is condemned unheard! Je kama alitaarifu mamlaka za juu kuhusu tatizo hilo akaambiwa asubiri fedha hazipo kwa sasa Hazina? Katibu Mkuu hazina alipaswa kuulizwa kama ana taarifa juu ya jambo hilo na jee ombi la fedha kwa matengenezo na ununuzi wa vifaa lilifika kunakohusika? Sasa akitembelea hospital za Mikoani si atafukuza Madakatari wa kuu wa Mikoa yote kwa kosa hilo? Dr
Pombe ameanza vizuri sana ila asaidiwe ili akimuwajibisha mtu awe ni muhusika!

Ili kupusha uchunguzi wa tatizo alilo liona Pombe, that's why amemsimamisha kazi mkurugenzi wa muhimbili. Hajamfukuza kazi, hapa naona wadau wengi wanachanganya mambo kati ya kusimamishwa na kufukuzwa kazi
 
Rais Dk.Magufuli amefuta bodi ya afya Muhimbili na kumsimamisha kazi mkurugenzi mkuu wa Hospitali hiyo. Kitendo hicho kimekuja baada ya kuzuru gafla Hospitali kuu ya Taifa Muhimbili hii leo.

Tunashukuru kwa taarifa mkuu. Ila mbona huja ainisha sababu zilizopelekea Magufuli kufuta bodi ya afya Muhimbili?
 
Mnaongea as if kuna vimrija vimekatwa sasa ndio mnahaha. JPM hajamfukuza kazi Bali amemsimamisha kazi ili kupisha uchunguzi, Kama hana kosa atarudishwa kazini asap! Msitake kujifanya vichwa maji wakati akili mnazo.

Mkuu nadhani unanituhumu bure tuu huku ukiwa hujui nini mtoa mada kaandika, hebu rudia kusoma post kuu then uje usome na niliyoandika halafu uangaliw na ulivyoquote kwa hasira kali.

Kaka Tanzania ni yetu sote, tuweke uchama kando utaona inchi itavyosonga, hatuwezi jadili mambo ya msingi ya nchi kiushabiki na mihemuko.
 
Anawasimamisha kazi bila kujua makosa anayoyaona yametokana na serekali aliyokua anaitumikia. mfano ni budget ndogo na mishahara midogo, ule mgomo ndio athari anazoziona sasa, na atathimini ni watz wangapi wamekufa kwa makosa ya serekali aliyokua anaitumikia, Kuwafukuza ni kuwaonea, inabidi afukuze serekali nzima mpaka yeye mwenyewe kwani barabara alizojenga zina mashimo kwa muda mfupi tu. hio ni danganya toto tunataka ajenge mifumo mizuri ya kisheria na uwajibikaji ili watu wazembe waondolewe na mifumo na sheria sio kukimbiza mtu mmoja mmoja kama unawinda.
 
Watu wamesahau kwamba lowasa Mzee wa kusikiliza watu alishawahi kumfukuza kazi bila kumpa nafasi ya kujieleza enginer mkuu wa jiji pale jengo lilipoanguka changombe 2006
 
Kwa wakazi wa bandari na tanesco upepo unaweza kuvuma kuelekea upande huo hivyo wakazi wa maeneo hayo mnashauriwa mkae macho pepo zinasafiri km 300 kwa saa.Ahsante kutoka mamlaka ya hali ya hewa.
 
Rais Dk.Magufuli amefuta bodi ya afya Muhimbili na kumsimamisha kazi mkurugenzi mkuu wa Hospitali hiyo. Kitendo hicho kimekuja baada ya kuzuru gafla Hospitali kuu ya Taifa Muhimbili hii leo.
Duh Kwa Kasi Hii. Mkuu tuko Nyuma yako Watanzania wazalendo wote. Najua soon utaanza kupata hujuma kwani kuna ukoo wa Panya uop mwingi sana Nchii Hii. Na Hawatakubali kwenda na Kasi yako so watajipanga wakuhujumu.
Mkuu bado Kikosi Cha Usalama Barabarani kwani wanapokea rushwa kama wamekula kiapo.
 
Mkuu jiongeze basi kidogo. Wizara alizopita RAIS MAGUFULI huko nyuma are enough to test a MAN. Na alivuka with perfection.
mabua hayo, ngoja aanze kupata changamoto za maana atatulia tuli, kama sauti ilivyokata wakati anaanza kampen, alikuwa abaongea taratibu kama na wanae vile wakati wa kampen, Tusubiri tuone
 
Back
Top Bottom