Rais Magufuli amsimamisha kazi Mkurugenzi Muhimbili

Amempa fursa ya kujieleza? Ikitokea kuwa serikali ndio haikupeleka fungu, atamrudisha kazini? Utawala bora hauko hivyo.

Mara nyingi vitu kama hivyo keshafanya homework yake.

Fikiria wao wanakupa ambulance ili ukafanye kipimo sehemu fulani. Kama si 10% ni kitu gani. Hizo X-Ray na CT Scan za Muhimbili ndiyo vinaharika peke yake wakati kwenye hospital binafsi wafanyakazi ndiyo hao hao wa Muhimbili.
 
Mkuu nadhani unanituhumu bure tuu huku ukiwa hujui nini mtoa mada kaandika, hebu rudia kusoma post kuu then uje usome na niliyoandika halafu uangaliw na ulivyoquote kwa hasira kali.

Kaka Tanzania ni yetu sote, tuweke uchama kando utaona inchi itavyosonga, hatuwezi jadili mambo ya msingi ya nchi kiushabiki na mihemuko.

Hapa hakuna utetezi, Waziri/wizara ndio ilimtuma ashindwe kujiendesha kibiashara? Hawa watu ni wezi na hawana tofauti na bodi ya tanesco ya miaka ya 2006. Wapigwe chini! HAPA KAZI TU!
 
Haya matanzania bhana shida kweli hayohayo kulalamika huduma mbaya hospitali,sasa wahuska wameanza kuwajibishwa nayaona tena yanasema anakurupuka,uongozi bora hauko hivyo yaan sjui uyafanyie nn haya matanzania yakuelewe
 
Amempa fursa ya kujieleza? Ikitokea kuwa serikali ndio haikupeleka fungu, atamrudisha kazini? Utawala bora hauko hivyo.

Huyu ni raisi na anaelewa anacho fanya, nina uhakika kila jambo analo fanya analifahmi na kashapata maelezo ya kutosha. Labda awe raisi ambaye hajaenda shule...
 
Hilo tatizo la MRI na CT-scan kutofanya kazi lipo mara kwa mara hospitali za Serikali na ni miongoni mwa mambo yanayowafanya wananchi kuichukia serikali. Ni jambo jema kwa JPM kulivalia njuga.tunamuomba pia apige marufuku viongozi kwenda kutibiwa nje ili waboreshe hospital I za ndani.
 
Magufuli ameifuta bodi ya afya ya hospitali ya Muhimbili na kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Muhimbili baada ya kutembelea hospital hiyo na kukuta Vifaa/vipimo vya MRI na CT-Scan hazifanyi kazi kwa kipindi Cha miezi 2 wakati MRI na CT-Scan za hospital za watu binafsi zinafanya kazi.

Stay tuned for more details.

Kha, Kwa mwendo huu nimekwisha. sijui nitafute kazi nje au niende ukawa
 
Safi sana nchi ilijaa ufisadi kila sehemu Acha asafishe akitoka pale aelekee TANESCO, Bandari na TTCL Kikwete aliwalea sana.
 
Kuwa na akili. Akajieleze sasa tatizo ni mfumo au management yake. Acha ushabiki.
Matatizo ya Muhimbili yamesababishwa na mfumo wa nchi ni kukurupuka sana kama tunadhani mkurugenzi ana makosa , huwezi kutatua matatizo ya muhimbili kwa kumsimamisha mkurugenzi .
 
Haya matanzania bhana shida kweli hayohayo kulalamika huduma mbaya hospitali,sasa wahuska wameanza kuwajibishwa nayaona tena yanasema anakurupuka,uongozi bora hauko hivyo yaan sjui uyafanyie nn haya matanzania yakuelewe
Wala usishangae, mirija imekatwa so wanahaha kutafuta pa kutokea. Hapa kazi tu!
 
Mkuu ajieleze nini? Wewe huwajui wabongo kwa longolongo? Ukimruhusu kujieleza tu anachomoa!Na kumbuka huyu jamaa anaitwa Tingatinga, Sasa uliona wapi Tingatinga likija kubomoa Nyumba yako linakupa muda wa kujieleza? Mimi nasema aendelee tu hadi watu wakae kwenye mstari kwanza ndipo mambo ya kujieleza yatafuata baadae.

Ni kweli kabisa unalo sema, si muda wa kujieleza sasa hivi. Na kama si mkurugenzi nani awajibike sasa...
 
No one is condemned unheard! Je kama alitaarifu mamlaka za juu kuhusu tatizo hilo akaambiwa asubiri fedha hazipo kwa sasa Hazina? Katibu Mkuu hazina alipaswa kuulizwa kama ana taarifa juu ya jambo hilo na jee ombi la fedha kwa matengenezo na ununuzi wa vifaa lilifika kunakohusika? Sasa akitembelea hospital za Mikoani si atafukuza Madakatari wa kuu wa Mikoa yote kwa kosa hilo? Dr
Pombe ameanza vizuri sana ila asaidiwe ili akimuwajibisha mtu awe ni muhusika!

Kwa iyo wewe ndio unajua kuliko Magufuli? Yeye sio kichaa hayo unayosema alishayaona
 
Amempa fursa ya kujieleza? Ikitokea kuwa serikali ndio haikupeleka fungu, atamrudisha kazini? Utawala bora hauko hivyo.

Fungu la viazi?,kama wewe ni professional na mwajiri hataki kutengeneza vifaa acha kazi tu badala ya kula mshahara wa bure huku watu wanateseka
 
Sasa hamia tanapa, viwanja vya ndege na bandarini sababu kubwa ni kwamba tembo na faru wetu wanaisha
 
Tatizo letu Watz ni kufurahia mwingine kuguswa na misukosuko. Kamwachisha kazi, yeye ndiye kamwajiri?? Mkurugenzi huyo ana haki zake chungu nzima, unamwachisha tu ka Hg!!! Haya tungojee. Alisimamisha Makandarasi wangapi wa barabara bila mjadala. Wakamshinda mahakamani ka mtoto. Akalipa mihela ya kufa mtu. Hasara kwa taifa. Aliizuia meli ya Mvietnam, na samaki zake akagawa bure watu wale. Ati nitawashinda mahakamani. Amelipa meli mpya na samaki wapya kwa Dollar mpya za kimarekani. Hasara kuu kwa taifa.
Haya yoote, mlimsifia. Sitamsema vibaya rais wangu ila, Uongozi bora si hivyo. Yeye ni kiongozi, awaongoze wanaoongoza wafanye kazi ya viwango si kutimuana bila mpangilio. Ila kwa vile huwa hatuambiwi, mngekuja kutujuvya atakacho lipwa huyu mhusika baada ya kumbwaga mahakamani.


Kesi ya meli for your information, mafisadi walimzunguka. Wakala hela kwa wenye meli na kuhonga huko mbele. magufuli angefanya nini? Sasa yeye ndiyo top. Tuendelee kuona muziki wake hadi watu waingie kwenye mstari.
 
Tuombe apate mawaziri wenye imani na nchi Yao/yetu kama Mheshimiwa Raisi. Maana Raisi peke yake hawezi kuindesha nchi peke yake.
 
Back
Top Bottom