Rais Magufuli afuta sherehe za maazimisho ya siku ya UKIMWI, fedha zinunue dawa...

nashangaa sana Rais Magufuli kufuta siku ya Ukimwi inayo adhimishwa duniani kote kila tarehe moja December.
hakuna mantiki yoyote Ukimwi bado ni janga la Dunia naomba Rais wetu punguza ubabe hausaidii sana na una madhara mengi sana hapo baadaye
mngeruhusu siku iadhimishswe bila kuwepo gharama zozote kama sherehe
naomba tutupia macho mambo haya kwa makini
 
Acha uongo wako hapa! leo nilikuwa singida,maadhimisho hayo yamefanyika viwanja vya peoples.Labda ungesema Magufuli ameshindwa kuhudhuria.Ila chakushangaza walijaza tu wanafunzi wa sekondari.

Siku ya ukimwi huwa ni tarehe ngapi bro??
 
We ni mjinga,sasa mbona ukimwi bado inashika kasi? Na isitoshe wengine wanaupatia hapo hapo kwenye maadhimisho.
Jiongeze.
 
siku ya ukimwi ipo ila imefutwa sherehe ambayo ingetumia pesa nyingi....

pesa hizo zimeelekezwa kununua dawa za ARV...jambo ambalo sio baya...
 
Huyu mtu anatakiwa atiwe governor na bunge au washauri wake (.. ila sidhan hata kama anashaurika). Hayo ni maadhimisho ya dunia/UN kwa ajili ya awareness, siyo SHEREHE.

Miaka yote mmekuwa mmeazimisha...kama ni awareness tayari tumeipata. Sasa mnataka nini? Pesa tunaenda kununua ARV....hakuna posho, hakuna T shirts wala gharama za upambaji...mlikuwa mkipiga sana hela za walipa kodi vilaza nyinyi.
 
Kinachofutwa sio maadhimisho...Ni sherehe ambazo zinaambatana na matumizi makubwa sana ya fedha...Bajeti zake zinatisha...Watu wamekuwa wakizitumia sherehe hizi kuvuna mapesa kwenye zabuni za fulana...Kofia...Matangazo...Maandalizi n.k

Kipi bora...Kufanya sherehe za gharama kubwa ama kutumia fedha hizo kununua dawa...

Tunaweza kiadhimisha hata kwa Rais kuhutubia kupitia TV na Radio

Hii siku ni muhimu kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu ukimwi... ukitoa elimu utakuwa umeokoa maisha ya watu wengi kuliko kuwapelekea dawa!
 
wavivu watamuona magufuli hafai katika maamuzi yake eti udicteta

poleni wavivu hapa kazi tu...
 
nashangaa sana Rais Magufuli kufuta siku ya Ukimwi inayo adhimishwa duniani kote kila tarehe moja December.
hakuna mantiki yoyote Ukimwi bado ni janga la Dunia naomba Rais wetu punguza ubabe hausaidii sana na una madhara mengi sana hapo baadaye
mngeruhusu siku iadhimishswe bila kuwepo gharama zozote kama sherehe
naomba tutupia macho mambo haya kwa makini

Hivi toka tumeanza kuadhimisha the so called World Aids Day Ukimwi umepungua ama umeongezeka??..

Watu wameugeuza UKIMWI kuwa mradi wa kuchuma pesa...Kuanzia serikalini mpaka kwenye NGOs watu wanatafuna fedha za Ukimwi bila huruma...Bado serikali inatumia fedha nyingi kweli kuandaa na kuendesha hayo maadhimisho...Ni mara kumi fedha hizo zikatumika kununua Condoms na ARVs badala ya hizo shereheza kila mwaka zisizokuwa na tija...
 
Acha uongo wako hapa! leo nilikuwa singida,maadhimisho hayo yamefanyika viwanja vya peoples.Labda ungesema Magufuli ameshindwa kuhudhuria.Ila chakushangaza walijaza tu wanafunzi wa sekondari.

Ule umeona ni ufunguzi yenyewe huwa Dec moja kaka.
 
Hajafuta imeahairishwa tu mwaka huu isiadhimishwe ,lkn pengine hazina watu wamekausha huwezi jua,pengine miaka mingine atasonga mana ni yakidunia.
 
Sawa.. ila ni kwamba uwingi wa dawa ni dawa.. ukisema madawa siyo sahihi.

Nimefurahi kwa comment hii. Wengi siku hizi Kiswahili kinawapiga kumbo. Kwa mfano utasikia wanasema: MASAA, Uwingi wa saa ni SAA Halafu utasikia wanasema: HUWA NAKWENDAGA, TUNAKULAGA CHAKULA...TUNACHEZAGA N.K. yaani waandishi wa habari ndio wenyewe kwa kuharibu Kiswahili.
 
Back
Top Bottom