Rais Magufuli afanya kikao na Sekretarieti ya CCM

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,976
Hiki ni Kikao cha kwanza na wajumbe wa Sekretarieti ya CCM kwa Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa tokea alipochaguliwa na Mkutano Mkuu wa CCM.

Rais pia ameongea na wafanyakazi wote wa ofisi ya Makao Makuu ya CCM, Dodoma.

IMGL1649.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula alipowasili Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma

IMGL1652.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Zakia Hamdan Meghji.

IMGL1653.jpg

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka.

IMGL1654.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi, Seif Shaban Nasoro.

IMGL1655.jpg

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCMTaifa , Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu wa UWT, Amina Makilagi.

IMGL1656.jpg

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu UVCCM, Shaka Hamdu Shaka.

IMGL1660.jpg

Rais wa Jamhuri ya miingano na Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu wa Sekretarieti, Anamringi Macha.

IMGL1671.jpg

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt. John Pombe Magufuli baada ya Mwenyekiti kuwasili Makao Makuu ya CCM, leo. Kushoto ni Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa na Wapili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula.

IMGL1681.jpg

Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa , Dkt. John Magufuli akiwasili ukumbini, kuzungumza na Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM, Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma, Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula na Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Waziri Mkuu Majaliwa KassimMajaliwa, Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rajab Luhwavi na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
IMGL1691.jpg

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (aliyesimama) akitoa maneno ya utangulizi kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. John Pombe Magufuli kuzungumza na Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM, Makamo Makuu ya CCM mjini Dodoma.
c11-jpg.371957
Mwenyekiti wa CCM, Rais Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Sekretarieti ya CCM Taifa.
c13-jpg.371963

Mwenyekiti wa CCM, Rais Magufuli na sekretarieti ya CCM wakiwa katika picha ya pomoja na wafanyakazi wote wa ofisi ya Makao Makuu ya CCM, Dodoma.
 
...wewe jamaa nahisi utakuwa secretary wa Magu, ndio mana kutwa huishi kumsifu kwa mapambio!
 
Philip Japhet Mangula best politician, namkubali sana huyo mzee itabidi nimtafute tupigie nae stori kuna vitu vingi nitajifunza toka kwake
Waliokuwa wanajiita Wanamtandao walimfanyia figisufigisu na kumuondoa kwenye Ukatibu Mkuu halafu wakafanya kila linalowezekana ili asiweze kufurukuta ndani ya CCM.

Baada ya CCM kuanza kuzama kisiasa, Rais Kikwete akaona walifanya kosa la kiufundi na kuamua kumrudisha tena kama Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara.

The rest is history...
 
Waliokuwa wanajiita Wanamtandao walimfanyia figisufigisu na kumuondoa kwenye Ukatibu Mkuu halafu wakafanya kila linalowezekana ili asiweze kufurukuta ndani ya CCM.

Baada ya CCM kuanza kuzama kisiasa, Rais Kikwete akaona walifanya kosa la kiufundi na kuamua kumrudisha tena kama Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara.

The rest is history...
Mzee safi sana hana makuu kabisa mzee wa watu, si mwingi wa maneno ila vitendo anavijua itabidi awe mentor wangu huyu maana bila hivyo chama wataachiwa watu wa ovyo kweli
 
Bavichaaa kila siku walikuwa wanahubiri humu na kupiga ramli Magufuli hawezi kuwa mwenyekiti Wa ccm.

Haya ngoja tuone watahubiri nini tena baada ya kuumbuka vibaya.

Wanajifanya hawaipendi ccm lkn kila kukicha wanahubiri ya ccm na kuacha ya Sacco's UKUTA
 
Back
Top Bottom