Rais kwenda kwenye msiba wa msanii je ni sahii?

Hakutakiwa kwenda huko, Hana kazi za kufanya!!. Alikuwa wapi wakati anaumwa!!, Kama anasaidia wavuta unga alishindwa nini kumaidia huyu wakati anaumwa!!. Jibu ni No!.
 
Hiv jamani hatuna ya kujadili? Kwani kuna ubaya gani rais kwenda msibani? Yeye sio binadam? Kwan yeye hatazikwa? Mambo mengine!!
 
acheni hizo banaa... rasi naye ni msanii........au mmesahau???
 
Huyu mtu huwa anashangaza sana yeye na washauri wake dugu moja...Hivi kwa nini anakuwa mgumu wa kuelewa?? 2015 ifike hata kesho maana tumechoshwa na comedy za huyu mtu oh nilisahau kama naye ni msanii...mwenyekiti wa wasaniii tz.
 
Dhuki na ukosefu wa shughuli mbaya sana . mwishowe utafuatialia hadi rais kala au kavaa nini ...then utaishia kusema kodi zetu
 
Kama una elimu yako nzuri, ajira nzuri au uko busy na biashara zako sidhani kama utapata muda wa kufuatilia kisichokusaidia
 
Kwan wasanii si binadamu, na kuna ulazima wa raisi kuhudhuria misiba yote bila kujali majukumu aliyonayo na sehemu aliyopo????
 
Mime mwenyewe niliwaza hivyo hivyo kama wewe baadae nikapata jibu kuwa kule marekani raisi Obama ana protocol kali sana inayomzuia kuhudhuria vitu kihasara hasara kama raisi wetu hapa bongo. Inawezekana JK pia ana protocol ila sidhani kama anaifuatlia au anajiamulia mwenyewe akiamka aende wapi na kuacha shughuli za maana za kitaifa. Kwa msiba huu ilitosha alivotoa salamu za rambi rambi then agetuma mtu akamwakilishe kw ajina lake. Iko siku atapigwa kabari na wahuni shauri yake.

Ila tusisahau JK anapenda safari thats why kwa wiki lazima ahudhuria misiba haijalishi ni nani na uzito gani kwa taifa hili.
RIP Sajuki na pole sana Wastara:A S-cry:

Kwani kila wanachofanya ulaya au wazungu ndo sawa?! Mbona hamjiamini, hatuna maamuzi aina yetu
 
Kwani kila wanachofanya ulaya au wazungu ndo sawa?! Mbona hamjiamini, hatuna maamuzi aina yetu

Tungekuwa na maamuz yetu basi tungebakia zama za mawe kuishi mapangoni na kula mizizi maana ndio wazungu walivotukuta wakatuendeleza na kutuonyesha njia ya maendeleo na ndio kioo chetu sisi. Kila kitu tumeiga usikute hata hizo pamba ulizovaa hapo umeiga kwa wazungu, vaa magome ya mti ndio tujue kuwa hutaki kuiga uzungu...kinyume na hapo kuiga mazuri ya wazungu hakuepukiki....
 
Hawa wanasiasa wamezidi kutafuta publicity,haswa kwenye matukio ya msiba.
Wanatamani kila mwezi msanii afe,ili kampeni za kuelekea 013!
Sijamwona tu Lowasa,nahisi makanisani na misikitini kunalipa!
 
Rais na msafara wake gharama anazotumia ni kubwa sana. Alipawsa kutuma mwakilishi wake tu, pamoja na rambi rambi basi.


Sent from my BlackBerry 8900 using JamiiForums
 
Rais hapaswi kuhudhuria misiba ya watu wengine ambao sio ndugu zake. Hata wakati wa Mwalimu Nyerere watu walikuwa wanakufa na hakuwa yeye binafsi anakwenda misibani. Alikuwa anatuma wawakilishi inapobidi na marehemu Rashid Kawawa alikuwa sana anatumwa kumwakilisha Mwalimu pale inapobidi.

Alipofariki Waziri Mkuu Edward Sokoine Mwalimu alishiriki mwanzo mpaka mwisho kama Rais, na hata kwenye msiba wa marehemu Abeid Amani Karume Rais wa Zanzibar Mwalimu alishiriki kikamilifu. Alipofariki Samora Machel Rais wa Mozambique wakati Mwalimu ameshastaafu hakuhudhuria mazishi, ila Rais wa wakati huo Ali Mwinyi ndiye aliyewakilisha Tanzania. Kwa kuwa Samora alikuwa rafiki wa karibu wa Mwalimu, yeye na mama Maria Nyerere walikwenda kuhani kwa mjane wa Samora, Graca Machel baada ya mazishi.

Nchini Tanzania walikufa wasanii wengi katika kipindi hicho, wakiwemo wanamuziki kama wakina Mbaraka Mwinshehe na Salum Abdalla. Serikali iliwakilishwa na Waziri anayehusika wakati huo akiwa Waziri wa Utamaduni jina limenitoka.

Ukiona kiongozi wa nchi anahudhuria misiba ya wasanii basi uelewe ya kuwa hana kazi ya kufanya na pia anatafuta umaarufu (cheap popularity). Anaenda kuonyesha sura hasa kwa kuwa anajua vyombo vya habari vitakuwepo na sura yake itaonekana nchi nzima aweze kuwadanganya watu kama yeye ni mtu wa watu. Kama kweli anajali watu, basi aanze kushughulikia matatizo ya watu ya kila siku. Hospitali huduma mbovu ndizo zinazosababisha vifo vingi kwa watu kukosa huduma ya uhakika. kama kungekuwa na hududma za kutosha kwa nini watu (akiwemo huyo Sajuki) inabidi watumie pesa nyingi kupelekwa India kupata huduma miaka 51 baada ya Uhuru?

Mtu wa pwani anapolia njaa humpi samaki ale, unampa zana za kuvua samaki ili atatue matatizo yake avue samaki wa kula yeye, na wa kuuza apate pesa za kumsaidia.

JK kuonyesha sura yake misibani ni aibu ya kitaifa. Katiba mpya wekeni hicho kipengele kijulikane kisheria... anatia kichefuchefu!

Tema mate chini!

Tena kama hiyo haitoshi,binafsi nilitegemea kumuona Rais akiwa ameambatana na Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo katika shughuli nzima ya mazishi ya marehemu Sajuki,lakini hali haikuwa hivyo.Katika picha nyingi zilizoripotiwa kwenye vyombo vingi vya habari waziri husika haonekani,isipokuwa tu Rais,mkewe pamoja na baadhi ya wasanii wa filamu.This is SHAME to our nation.
 
Binafsi naona sio sahihi kwa Raisi kuhudhuria hii misiba ya wasanii. Kuna wa-Tanzania wengi tu wenye michango mikubwa kwa Taifa na hatusikii ushiriki wake kwenye misiba yao! Hii inajenga dhana kuwa anashiriki tu pale atakapoweza kuuza sura! Hili sio jambo jema kwa Uraisi kama Taasisi! Kibinadamu angaliweza kushiriki na familia husika kupitia uwakilishi - mke wake au mwanaye!

si kosa kwa MSANII KUHUDHURIA Msiba wa MSANII MWENZAKE!
 
Back
Top Bottom