Rais kuingilia utendaji wa NHC si sahihi

Rais Kikwete mmemkaa kooni, kila atachosema, atachofanya, atachofanya hata kama ni chema kwenu ni kibaya. Sababu zinajulikana wala msidhani hatuzijui, yanajirudia yaliyomkuta Mwinyi.
 
njia mbadala ni ipi hiyo kama watu wanadaiwa yapata miaka 3 mpaka 4 hawajalipa hakika kwenye miti hakuna wajenzi,ila matumaini yapo tutapata kiongozi wa juu ambae yeye safu yake ya utendaji ni watu aina ya nehemia mchechu na wakina john pombe magufuri ambao wapo tayari kusimamia utawala wa sheria na sio kufundisha jamii kukwepa sheria.tunako kwenda watendaji wengi wa serikali na hatimae umma utaanza kupuuza sheria halali na hatimae tumeanza kuona jinsi raia wanavyojichukulia sheria mikononi na mwisho wake viongozi na familia zao ndio watakao pima ubaya wa kulea matumizi mabaya ya kupuuza utawala wa sheria kwa kuwa umma umetunga sheria lakini aliyepaswa kusimia sheria na kuona haki inapatikana kesha amua kukaa pembeni na kuacha kanuni ya mbugani au msituni [jungle's law] kuendelea kutumika na sio utawala wa haki na sheria kwa faida ya walio wengi.

mwisho wa siku polisi lawamani...........
 
rais kikwete mmemkaa kooni, kila atachosema, atachofanya, atachofanya hata kama ni chema kwenu ni kibaya. Sababu zinajulikana wala msidhani hatuzijui, yanajirudia yaliyomkuta mwinyi.

ff ndo matokeo ya kuwa critical thinker at...........
 
Jk mwenyewe aliingia ikulu kupitia njia mbadala, ndo maana kila kitu kwake suluhisho ni matumizi ya njia mbadala
 
hayo mawizara hela za posho za vikao na safari zipo, za kulipa kodi hawana? na mkuu wa kaya anawatetea! tatizo huyo mkurugenzi hathubutu ku-resign kwa kuingiliwa madaraka,manake atakosa mtama. kazi ipo!
 
Nimesoma habari katika Tanzania Daima yenye kichwa cha habari" NHC yarudisha funguo za wazazi ccm" NHC yarejesha funguo za wazazi CCM katika habari hiyo inaelezwa kuwa Rais ameliambia shiraka hilo kutafuta njia mbadala ya kudai madeni badala ya sasa ambayo inaathiri sana wizara. Mi naona hii si safi hata kidogo. Ndio yale ya Magufuli alipoambiwa aangalie utu/uungwana badala ya sheria katika bomoa bomoa, kwa hali hii tutafika kweli?

Hivi mdaiwa ukimbembeleza atakulipa kweli?
Dawa ni kutumia nguvu hamisha vitu nje aache nyumba wazi aje mpangaji mwingine
 
Rais Kikwete mmemkaa kooni, kila atachosema, atachofanya, atachofanya hata kama ni chema kwenu ni kibaya. Sababu zinajulikana wala msidhani hatuzijui, yanajirudia yaliyomkuta Mwinyi.

Hivi unafikiri kwanini mashirika mengi ya umma yalifilisika? Ni hali hii hii, kutokufuata sheria na kanuni za utendaji.

Wizara huwa inapeleka makadirio ya bajeti yake kila mwaka wa fedha unapokaribia, katika makadirio hayo kodi huwa ndani yake. Sasa kama wakipewa fedha ndogo kuliko walivyohitaji ni kosa la Serikali(Mfano tumeuona kwenye bunge lililopita, serikali inatenga fedha kiduchu kulinganisha na fedha iliyoombwa na wizara). Hata wakipata hiyo fedha ndogo, kodi ni kipaumbele, mambo ya walsha na posho za vikao visivyoisha ni ya baadae kama si kufutwa kabisa.
Hasa hasa serikali inahitaji kukuza mapato yake, iboreshe sheria za kodi kwenye madini, na kwenye uwekezaji mwingine. Mianya ya ukwepaji kodi izibwe.
Yaani kiufupi ni kuwa serikali haifanyi kazi ipasavyo, kila sehemu imeoza. Ndiyo maana tunamuandama mkuu wa serikali.
 
Kama kweli tunaheshimu sheria hapa hakuna cha njia mbadala kinachotakiwa ni kulipa madeni yote. kwani hizo pesa si walipewa kulipia kodi za nyumba wamezipeleka wapi. Hivi ni lini jk ataacha sheria ifuta mkondo wake?. dawa ya deni ni kulipa tu hakuna njia mbadala hapo
 
Nimesoma habari katika Tanzania Daima yenye kichwa cha habari" NHC yarudisha funguo za wazazi ccm" NHC yarejesha funguo za wazazi CCM katika habari hiyo inaelezwa kuwa Rais ameliambia shiraka hilo kutafuta njia mbadala ya kudai madeni badala ya sasa ambayo inaathiri sana wizara. Mi naona hii si safi hata kidogo. Ndio yale ya Magufuli alipoambiwa aangalie utu/uungwana badala ya sheria katika bomoa bomoa, kwa hali hii tutafika kweli?

Kwani sihuyu Nehemia amekiri kama anafuata ilani ya CCM.... sasa atakoma kuringa... Raisi ndio menyekiti wa CCMna kinara wa utekelezaji wa hiyo ilani
 
Nimesoma habari katika Tanzania Daima yenye kichwa cha habari" NHC yarudisha funguo za wazazi ccm" NHC yarejesha funguo za wazazi CCM katika habari hiyo inaelezwa kuwa Rais ameliambia shiraka hilo kutafuta njia mbadala ya kudai madeni badala ya sasa ambayo inaathiri sana wizara. Mi naona hii si safi hata kidogo. Ndio yale ya Magufuli alipoambiwa aangalie utu/uungwana badala ya sheria katika bomoa bomoa, kwa hali hii tutafika kweli?

JK ni ndumilakuwili. napenda sana kuonekana mzuri kila upande!! Kwa maneno haya ina maana anjua kwanini wizara zake licha ya kuwa na bajeti kwanini hazilipi!! Labuda serikali imefilisika, kuna hela kwenye makaratasi lakini hard cash nehi!!!

Kwa hili si sahihi, alipaswa kuwaacha NHC wafanye kazi zake kibiashara ili kuleta ufanisi. Msechu atajuta kuacha CBA, kwenda kwenye makazi ya kisiasa!! Inabidi uwe poimbi tu, wa kutuliza ball!!!!
 
Rais Kikwete mmemkaa kooni, kila atachosema, atachofanya, atachofanya hata kama ni chema kwenu ni kibaya. Sababu zinajulikana wala msidhani hatuzijui, yanajirudia yaliyomkuta Mwinyi.

Sawa madam First lady. Lakini aache undumilakuwili.
 
Katika hili la NHC ni kwa nini Serikali ya Ccm iwe bado inazing'ang'ania nyumba ambazo zinahitajika hata kwa sasa hivi zirudishwe
kwa wenyewe waliotaifishwa wakati wa sera mbovu za ujamaa na kujitegemea. Na nyumba ambazo wahusika hawapo ziuzwe
Serikali ikumbuke kwamba nyumba hizo hazikujengwa na Serikali ya Tanu wala ya ccm, Bali zilitaifishwa kwa mpango maalum
wa kuwadhoofisha Raia kwa madhumuni ya kuwatawala kimabavu, kwa siasa ambayo ilishindwa kuwaongoza watanzanzia.
Na huu ni wakati mbadala wa kuzirudisha nyumba zote kwa wenyewe, Ikiwa Serikali waliuza nyumba zao kwa nini wazing'ang'-
anie hizo, Kwa hatua hiyo ya Serikali ya Ccm inatufanya Watanzania tuwe na maswali mengi ya kujiuliza ambayo bado yako
wazi.
 
Katika hili la NHC ni kwa nini Serikali ya Ccm iwe bado inazing'ang'ania nyumba ambazo zinahitajika hata kwa sasa hivi zirudishwe
kwa wenyewe waliotaifishwa wakati wa sera mbovu za ujamaa na kujitegemea. Na nyumba ambazo wahusika hawapo ziuzwe
Serikali ikumbuke kwamba nyumba hizo hazikujengwa na Serikali ya Tanu wala ya ccm, Bali zilitaifishwa kwa mpango maalum
wa kuwadhoofisha Raia kwa madhumuni ya kuwatawala kimabavu, kwa siasa ambayo ilishindwa kuwaongoza watanzanzia.
Na huu ni wakati mbadala wa kuzirudisha nyumba zote kwa wenyewe, Ikiwa Serikali waliuza nyumba zao kwa nini wazing'ang'-
anie hizo
, Kwa hatua hiyo ya Serikali ya Ccm inatufanya Watanzania tuwe na maswali mengi ya kujiuliza ambayo bado yako
wazi.

Mkuu hapo umenena japokuwa mimi na-declare interest kwamba ni mbaguzi wa rangi. Lakini kumbuka kuna nyumba zilijengwa na serikali na kuna zingine zilitaifishwa zikawekwa kwa msajili wa majumba. Hizi ambazo zilitaifishwa zikirudishwa kwa wenyewe zitarudi kwa wahindi ambao ndio wanaozikalia anyway. Ila kwa kuwa mimi ni mbaguzi wa rangi sipendi zirudishwe, hilo tu. Hoja yako ina mantiki. Kwa nini serikali iliuza nyumba zake lakini ing'ang'anie ambazo ilitaifisha toka kwa hao jamaa zenu?
 
Rais anayelalamikia umeme kama mwananchi wa kawaida, unategemea nini kwa swala nyeti kama hili? He is simply not my president anyway.!!!
 
Nimesoma habari katika Tanzania Daima yenye kichwa cha habari" NHC yarudisha funguo za wazazi ccm" NHC yarejesha funguo za wazazi CCM katika habari hiyo inaelezwa kuwa Rais ameliambia shiraka hilo kutafuta njia mbadala ya kudai madeni badala ya sasa ambayo inaathiri sana wizara. Mi naona hii si safi hata kidogo. Ndio yale ya Magufuli alipoambiwa aangalie utu/uungwana badala ya sheria katika bomoa bomoa, kwa hali hii tutafika kweli?

huyu mtu ndio anataka watendaji watafute suluhu kutokana na matatizo sugu? Sasa wafanye maamuzi gani tena zaidi ya kutekeleza yale yaliyoshindikana?
 
Back
Top Bottom