Rais Kikwete, Viongozi na wananchi wakati wa kuaga miili ya wanajeshi wa JWTZ

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,536
2,264

Rais Jakaya Kikwete, mkewe Mama Salma, wakitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza yenye miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan Julai 13, 2013 kutokana na shambulizi la ghafla, wakati wa zoezi la kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza yenye miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan Julai 13, 2013 kutokana na shambulizi la ghafla, wakati wa zoezi la kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akitia saini katika Kitabu cha Maombolezo ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla, wakati Rais na viobgozi wengine walipofika kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika Kitabu cha Maombolezo ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla, wakati Makamu na viobgozi wengine walipofika kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, akitia saini katika Kitabu cha Maombolezo ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla, wakati walipofika kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wafiwa baada ya kutoa heshima za mwisho kwa miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan Julai 13, 2013 kutokana na shambulizi la ghafla, wakati wa zoezi la kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd, akiwafariji wafiwa baada ya kutoa heshima za mwisho kwa miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan Julai 13, 2013 kutokana na shambulizi la ghafla, wakati wa zoezi la kutoka heshima zao za mwisho kuaga miili ya askari hao leo katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Regnard Mengi, akiwa na baadhi ya viongozi, wakitoa heshima za mwisho mbele ya Majeneza yenye miili ya Askari wa kulinda Amani, wa jeshi la Ulinzi la Tanzania, waliokufa huko Darfur Julai 13, 2013, wakati wa zoezi la kuagwa miili hiyo lililofanyika leo kwenye Uwanja wa Wizara ya Ulinzi, Upanga jijini Dar.

Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake, Dkt. Bilal, na viongozi wengine wakiwa katika shughuli hiyo ya kuagwa miili ya askari hao leo kwenye Uwanja wa Wizara ya Ulinzi Upanga Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, John Nchimbi akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, wakati wakiwa katika shughuli hiyo ya kuaga miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla. Kulia ni Katibu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Majeneza yenye miili yakiwa eneo la tukio tayari kuagwa.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati wa zoezi hilo.
Mkuu wa Majeshi,Jenerali Davis Mwamunyange, akizungumza wakati wa zoezi hilo.

Baadhi ya wafiwa wakiwa na huzuni huku wengine wakilia kwa uchungu wakati wa kuagwa miili hiyo.

Baadhi ya wafiwa wakiwa na huzuni huku wengine wakilia kwa uchungu wakati wa kuagwa miili hiyo.

Baadhi ya Askari pia wakiwa na nyuso za huzuni.PICHA NA OMR.





[h=3]*ASKARI WALIOKUFA DARFUR WAKILINDA AMANI HAWA HAPA-MUNGU ZILAZE ROHO ZAO PEMA PEPONI AMINA[/h]


MT 97024 PTE Fortunatus Wilbard Msofe- 36 KJ

MT 80581 CPL Mohamed Juma Ally- DFHQ AU

MT 72032 CPL Mohamed Chukilizo 41KJ

MT 87085 PTE Rodney Gido Ndunguru 92 KJ

MT 88860 PTE Peter Muhiri Werema 44KJ

MT 72121 SGT Shaibu Shehe Othman DFH-AU

MT 75028 CPL Osward Paul Chaula 431 KJ.
 
Binadamu wote tunapita hapa duniani.

Katika kitabu cha Mwanzo 3:19 kinasema,
"Kwa maana wewe ni mavumbi na mavumbini utarudi".

( For you are dust, and to dust you will return )

Surat Al – Imraan, 185
"Kila Nafsi itaonja mauti na bila shaka mtapewa ujira wenu kamili siku ya kiyama, na aliyewekwa mbali na moto na akaingizwa peponi, basi amefuzu, na maisha ya Dunia hii ni starehe idanganyayo".

(Every soul shall taste death. You shall receive your full reward for everything which you have striven for, on the Day of Resurrection. Whoever is spared from the fire and is admitted into paradise will have attained the objective of this worldly life; for the life of this world is nothing but an illusory enjoyment.)​
 
Sasa kama mnajua binadamu wote tunapita tu hapa duniani kwanini msiache demokrasia ifanye kazi yake? Kwanini mtumie majeshi kuzuia haki ya wananchi? Kwanini muue na kutesa watu ili hali mnajua wote tunapita? Acheni hizo hii dunia hamna mtu mwenye ubia nayo! Badala ya kutoa hoja zenye kuisaidia tanzania iendelee mmekalia majungu ya kuvidhoofisha vyama pinzani. Mnasahau kuwa hata wapinzani ni raia wa tanzania wenye kuhitaji kila haki ktk nchi yao. Hata hao askali waliouwawa unaweza kukuta wengi wao hawana hata vibanda vya kuishi walikuwa wanaishi kwenye nyumba mbovu za serikali. Badilisheni maisha ya watanzania na kufanya siasa safi
binadamu wote tunapita hapa duniani.

Katika kitabu cha mwanzo 3:19 kinasema,
"kwa maana wewe ni mavumbi na mavumbini utarudi".
( for you are dust, and to dust you will return )​
 
Sasa kama mnajua binadamu wote tunapita tu hapa duniani kwanini msiache demokrasia ifanye kazi yake? Kwanini mtumie majeshi kuzuia haki ya wananchi? Kwanini muue na kutesa watu ili hali mnajua wote tunapita? Acheni hizo hii dunia hamna mtu mwenye ubia nayo! Badala ya kutoa hoja zenye kuisaidia tanzania iendelee mmekalia majungu ya kuvidhoofisha vyama pinzani. Mnasahau kuwa hata wapinzani ni raia wa tanzania wenye kuhitaji kila haki ktk nchi yao. Hata hao askali waliouwawa unaweza kukuta wengi wao hawana hata vibanda vya kuishi walikuwa wanaishi kwenye nyumba mbovu za serikali. Badilisheni maisha ya watanzania na kufanya siasa safi

"The way we see the problem is the problem." by Steven Covey.

Mitazamo huwa ina taswira tatu. Huu ni mtazamo wako kati ya taswira tatu.
 
Inasikitisha sana na inatia hasira pia!wajihami zaidi na silaha nzito!na wasiwaamini hata raia wanajitokeza barabarani kuomba msaada!
 
Vipi kuhusu familia za hawa marehemu, wajane na Yatima, Serikali itawatunza na kuwasomesha?
 
Back
Top Bottom