Rais Kikwete: Nabii asiyekubalika nyumbani kwake?

Ndugu SMU Heshima mbele
Kutunukiwa Degree ya heshima sio garantee ya kufanya mema kwa Kikwete ndani ya nchi yake. Martin Luther Kinng aliwahi kusema nanukuu
"The ultimate measure of a man is not where he stands in moments of comfort and convenience, but where he stands at times of challenge and controversy."
Msimamo wa Mheshimiwa JK kwenye ufisadi ni upi hasa? Nchi imeyumba utafikiri hatuna Rais. Ni yapi mazuri aliyoyafanya zaidi ya uchumi wa nchi kuporomoka, mfumuko wa bei kuwa juu na madeni kuongezeka?

Obi,
Hizo degree nilitolea kama mfano tu wa jinsi watu wa nje ya Tz wanavyomtizama JK.

Kuna wakati anasifiwa na watu wa nje (mf Bush, Obama) mpaka unajiuliza kama kweli wanamaanisha au ni sisi ndo hatuoni mazuri yake.

Lakini kama watu mbalimbali walivyochangia mada, ni wazi kuna mazuri amefanya hata kama hayawezi ku outweigh mabaya yake.
 
umejitaidi kumtafutia vya kumsifia lakini jambo moja tu hujalitaja na ndio la msingi, hakuna nchi yoyote duniani iliyoendelea bila strong MANUFACTURING INDUSTRY, tiger ecenomies, china zote zimeendelea kwa strong manufacturing industry, na hapo ndio capitalist powers wame hold their advantage na hawatakubali waingilie, tunataka rais wa kuendeleza manufacturing industry badala ya kua taifa la wachuuzi, dream ya kila kijana nchi hii nowdays ni kupata frem pale kariakoo akalete makorokoro kule dubai aje auze, hatutaendelea milele, wala sio average, this guy is the worst of all kwani anayoyafanya ndio yanaumiza majority ya watanzania, kwa mfano he couldnt find new source of revenue instead when the budget reach deficit he rush to print more money( you need know someone in the inner circle to know this) as a result wananchi suffer from inflation of basic need e.g food prices are almost three times that when at the time he took office! democracy, freedom of press, road construction etc are vocabulalry not familiar to majority of tanzanian as they do not touch their daily lives, foods touch people daily lives!
 
Just a question for the JK apologists, Hivi JK alichaguliwa kuwa raisi ili afanye nini? Na so far aliyotakiwa kuyafanya yametekelezeka kwa % ngapi??

Usihangaike na kuwauliza wanaomtetea hata ukimuuliza yeye mwenyewe hajui alichaguliwa afanye nini alifikiri ni sifa kuwa rais aliona kama Mwanyi kawa rais basi na yeye naweza hakuwa na vision yeyote mbali ya kuuza sura angekuwa na busara angepumzika lakini asivyo atataka tena kipindi kingine na mambo ndiyo yata develop from bad to worse.
 
obi,
hizo degree nilitolea kama mfano tu wa jinsi watu wa nje ya tz wanavyomtizama jk.

Kuna wakati anasifiwa na watu wa nje (mf bush, obama) mpaka unajiuliza kama kweli wanamaanisha au ni sisi ndo hatuoni mazuri yake.

Lakini kama watu mbalimbali walivyochangia mada, ni wazi kuna mazuri amefanya hata kama hayawezi ku outweigh mabaya yake.

aliyevaa kiatu ndiye anajuwa kinapombana!
 
sio kwamba jamii haioni jambo zuri lililofanywa na kikwete mfano uhuru wa habari lakini tunategemea kiongozi au rais ambae atafanya mazuri zaidi ya yaliyofanyika kwa mfano azuie wazungu wasiibe rasilimali zetu, asiuze ardhi yetu kwa mwarabu(loliondo) , asicheke na mafisadi na pia awe mkweli pindi makosa yanapofanyika, si kwamba yeye asifanye kosa lolote,
 
Kwa hali ilivyo ni ngumu sana kuwakandamiza watu wasitoe maoni na dukuduku zao kwa faida ya ujenzi wa nchi yao.
 
Amefanya na kuanzisha UDOM na kufanya watu wake wame na cha kusemea na kupiga kelele nyingi sana juu ya hilo
 
Asante Kasheshe umetusaidia ku focus zaidi:
1. Elimu ya Sekondari kwa wote... (Shule za Kata)... soon will be there!
Wazo la sekondari za kata ni zuri lakini wameboronga sana kwenye implementation. Hawakujipanga na pia walilichukulia suala zima kisiasa zaidi. Ndio hapo unaona tuna shule nyingi (majengo) lakini hazina walimu na vifaa vya kufundishia. Pengine wangeweza kumerge baadhi hizi shule na kutumia resources ndogo za walimu walionao huku wakijiandaa kuongeza idadi ya walimu wenye sifa na kuwa motivate waliopo.
Kwa mtazamo wako hapa ume credit kama 20%
Asante Kasheshe umetusaidia ku focus zaidi:
2. Road constructions + (however few new surveyed and designed)
Nakumbuka hili suala liliwahi kuzua mtafaruku bungeni. Kuna mbunge mmoja alisema serikali ya JK haijajenga/tengeneza barabara hata moja. Project zote imerithi tu kutoka kwa serikali iliyotangulia. Baadae nakumbuka mbunge huyohuyo alimshukuru mtgeule wa JK, Bw Chenge kwa kusaidia kufanikisha ujenzi wa moja ya barabara katika jimbo lake.

Lakini kimsingi, bado hali ya barabara zetu ni mbaya sana. Mwezi Januari nilitembelea makao makuu ya nchi yetu (Dodoma). Hali ya barabara inasikitisha. Ukienda huko mikoani hali ni mbaya zaidi.
Kwa mtazamo wako hapa ume mcredit kama 40%

Asante Kasheshe umetusaidia ku focus zaidi:
3. University of Dodoma + (the biggest in East & Central Africa)
Kwa hili anastahili credit. Lakini issue siyo ukubwa tu (kama tunavyoona kwenye sekondari) waende zaidi kwenye quality. Unaweza kuwa na majengo mazuri lakini kama huna waalimu wa kutosha ni kazi bure. Utaishia kuwa na graduates vilaza tu.
Kwa mtazamo wako hapa ume mcredit kama 50%

4. Democracy and Freedom of Expression + (big plus)
Nimepitia posts mbalimbali naona baadhi wanajaribu kumdiscredit kwenye hili. Lakini kusema ukweli amejitahidi kuwa mstahimilivu. Ni kweli kuna baadhi ya magazeti yamewahi kufungiwa katika kipindi chake. Lakini hata hivyo ukiangalia namna waandishi wanavyoandiaka habari za kisiasa sasa na kipindi cha miaka sita nyuma kuna tofauti kubwa tu (wa sasa wanaandika kwa uhuhru mkubwa zaidi). Tujaribu kufuatilia front pages, kwa mfano tu, za gazeti la Mwanahalisi. Hata ile 'List of Shame' kwa kipindi cha Mkapa pengine ingekuwa ngumu kuitoa kwa namna ilivyotolewa.
Kwa mtazamo wako hapa umem credit kama 60%

5. National Stability (as a result of freedom of expression), if u despute this ask yourself if Six or Edo was the chairman of CCM during this period what could have happened?
6. Cammander in Chief - our Army got enough exposures - Somali, Comorro, Beirut et.
7. Health -- Campaigne against Aids, medicines are now found at health centres, now Malaria.
Nakubaliana na wewe. Kwenye afya infant/child mortality rate imeshuka kutoka around 73 (2006) hadi 69 (2009).
Kwa vile point zingine hujakubaliana nazo kwa mtazamo wako hapa ume mcredit kama 20%

Asante Kasheshe umetusaidia ku focus zaidi:
8. Habours --- eliminated monopoly of TICTS
9. Airports --- almost all big airports are under renovation or expansion.
14. TANESCO at list remain standstill but it was to be bankcrupt
15. Sports at least we managed to be "hawavumi lakini wamo"
17. Corruptions: He has done a lot, review of PCCB act, stregnthen the institution; election funding act etc etc
Bado anakazi kubwa sana ya kufanya. Tunatia aibu kwenye sekta hizo!
Kwa mtazamo wako hapa ume mcredit kama 15%

Asante Kasheshe umetusaidia ku focus zaidi:
10. Good governance: --- at least Tanzanians can see the difference btn parliament, judiciary.
11. Judiciary... appointed quite a big number of judges.
Hili linanipa shida kulikubali. Ukiangalia bunge letu bado ni 'kibaraka' wa serikali. Mahakama nazo ndo hivyo hazina sauti mbele ya serikali. Bado 'wanyonge' wanakosa haki zao mahakamani.
Kwa mtazamo wako hapa ume mcredit kama 10%

Asante Kasheshe umetusaidia ku focus zaidi:
12. Housing: Bill of mortgage passed etc.
13. Kilimo kwanza, coming
Too early to give any credit.
Kwenye kilimo suala la uozo kwenye vocha za mbolea ndo kwanza tu limeanza kufumuka. Tusubili mengine yanakuja.
Kwa mtazamo wako hapa ume mcredit kama 5%

Asante Kasheshe umetusaidia ku focus zaidi:
16. International Affairs: We have no "bifu" with anybody. he has done his part but Ni kweli amejitahidi.
Kwa mtazamo wako hapa ume mcredit kama 50%

Nimejiweka kama External Exam moderator nimejaribu kuzangalia point zako na kuzigrade kwa ujumla na hii naichukulia ni grade uliyompa JK kwa masuala uliyoyataja

Ukitafuta average ni sawa na kumpa JK 30% katika utendaji wake yaani

20%+40%+50%+60%+20%+15%+10%+5%+50%= 30%
 
Kwa hali ilivyo ni ngumu sana kuwakandamiza watu wasitoe maoni na dukuduku zao kwa faida ya ujenzi wa nchi yao.

kama rais akipenda anaweza kuwa mkandamizaji lakini utakuwa mwamzo wa mwisho wa mafanikio yake, kwa mfano tazama urusi kipindi cha putin
 
Ukitafuta average ni sawa na kumpa JK 30% katika utendaji wake yaani. 20%+40%+50%+60%+20%+15%+10%+5%+50%= 30%

Luteni,

Wewe unaionaje hiyo 30%? Inamtosha? Au ameonewa na 'perfomance appraisal' inabidi irudiwe:)?

Lakini, on a serious note tunavyoelekea October kama wapiga kura na pengine watu ambao tunaweza/wanaweza kuwa mbadala wa utawala uliopo ni vema kuanza kuyatizama mambo haya kwa karibu zaidi. Si ajabu kusikia ameshinda kwa kishindo kuliko ilivyokuwa 2005.
 
umejitaidi kumtafutia vya kumsifia lakini jambo moja tu hujalitaja na ndio la msingi, hakuna nchi yoyote duniani iliyoendelea bila strong MANUFACTURING INDUSTRY, tiger ecenomies, china zote zimeendelea kwa strong manufacturing industry, na hapo ndio capitalist powers wame hold their advantage na hawatakubali waingilie, tunataka rais wa kuendeleza manufacturing industry badala ya kua taifa la wachuuzi, dream ya kila kijana nchi hii nowdays ni kupata frem pale kariakoo akalete makorokoro kule dubai aje auze, hatutaendelea milele, wala sio average, this guy is the worst of all kwani anayoyafanya ndio yanaumiza majority ya watanzania, kwa mfano he couldnt find new source of revenue instead when the budget reach deficit he rush to print more money( you need know someone in the inner circle to know this) as a result wananchi suffer from inflation of basic need e.g food prices are almost three times that when at the time he took office! democracy, freedom of press, road construction etc are vocabulalry not familiar to majority of tanzanian as they do not touch their daily lives, foods touch people daily lives!

Strong points.
 
Luteni,

Wewe unaionaje hiyo 30%? Inamtosha? Au ameonewa na 'perfomance appraisal' inabidi irudiwe:)?

Lakini, on a serious note tunavyoelekea October kama wapiga kura na pengine watu ambao tunaweza/wanaweza kuwa mbadala wa utawala uliopo ni vema kuanza kuyatizama mambo haya kwa karibu zaidi. Si ajabu kusikia ameshinda kwa kishindo kuliko ilivyokuwa 2005.

Hiyo 30% nimei grade kutokana na mtazamo wako ila kwa mtazamo wangu nafikiri hata hiyo 30% asingefikisha lakini sina shaka pamoja na kuonyesha poor performance kama zilivyo shule zetu nyingi baada ya uchaguzi utasikia ka pass mtihani kwa flying colours
 
Mambo makubwa yaliyotokea wakati wa awamu ya kwanza ya JK yameimpact mfumo mzima wa kijamii na hivyo inakuwa vigumu kuona wapi tumegain kwasababu ofcourse Socially politically na pia economically,we have been loosers na sijui lini we have turned to be the gainers,coz sioni how wakati bajeti yetu ni tegemezi kwa asilimia kubwa na Taifa linaendeshwa "Kimatonya matonya" huku umasikini ukikithiri!

Kama tunakubali kuwa Taifa letu ni masikini,then cha kupima ni kwa kiasi gani tumepiga hatua tukiongozwa na mh rais kwenye kuutokomeza umasikini ambao unapelekea matatizo mengi kama magonjwa,ujinga nk.

Nimegunduwa kuwa viongozi wetu wakuu hususan mh rais mwenyewe huwa kimawazo wanaishi tofauti na matarajio na matakwa ya wananchi.....Hivyo basi Rais apimwe rather for how he has fought to eradicate poverty na si kwa jinsi gani jiji linafanana na majuu ama arabuni nk kwa majengo,fly overs ect....Viongozi wameloose touch na hivyo kutoka kwenye basics za kutuongoza ili tuweze kutoka kwenye dimbwi la umasikini....Badala yake wanatumia udhaifu uliopo ku implement siasa za danganya toto huku Taifa likiangamia.

Kuna namna siasa zinachezewa vibaya na wanasiasa wetu,namna ambayo inajeorpodize well being na stability ya taifa letu kwa kizazi kilichopo na hata kijacho kwasababu hakuna dalili kuwa mabadiliko ya kweli yatatoka from within.
 
Amemleta Drogba..
Amemleta Etoo...
Amemleta Bush...
Amemleta Maximo...
Ameleta kombe la dunia na tukapiga nalo picha..
Rais wa kwanza toka Africa kumtembelea Obama
Amewakaribisha wasanii wa bongo flava ikulu kupiga nao stori
Ameendesha mahojiano ya ana kwa ana live kupitia luninga....
Mhudhuriaji mzuri kwenye misiba,graduations na birthdays..(hata walalahoi tulipata nafasi ya kumshika mkono).
Kuna mwaka Miss Utalii ilitaka kushindikana kufanyika kwa kukosekana fedha ,akaiokoa na ikafanyika
Sasa watz wenzangu hapo nyumbani mngeyaona wapi yote hayo ???asili ya binadamu ..akiondoka ndiyo mtamkumbuka kwa 'mema'...
 
jmushi
Mimi naona the opposite is true kwamba mambo makubwa ambayo hayajafanyika ndiyo inatufanya tusione kama tume gain au tume lose sijaona jambo kubwa lolote la maendeleo limefanyika katika awamu hii kwa hiyo hatuwezi kupima kitu kama hatuna cha kupima

well wakati wa awamu ya pili liona mambo makubwa yalifanyika kama kuruhusu mfumo huria wa biashara kuruhusu mfumo wa vyama vingi hayo ndiyo tunaweza kusema ni mambo makubwa hata hivyo huwezi kuyapima kwa muda mfupi

naweza kusema katika awamu ya tatu pia kuna mambo makubwa talitokea mfano kukua kwa ukusanyaji wa kodi kuliosababisha kukua kwa pato la taifa vile vile kuingia mikataba mingi fake ambayo JK amekuja kuirithi

Jambo kubwa ambalo JK angeweka historia ni kuivunjilia mbali hiyo mikataba fake in contrary yeye ndiyo anaendelea kuikumbatia labda naweza kusema jambo kubwa ambalo JK amefanikiwa ni kutokuchukua maamuzi magumu yanayoweza kusambaratisha wanamtandao
 
Amemleta Drogba..
Amemleta Etoo...
Amemleta Bush...
Amemleta Maximo...
Ameleta kombe la dunia na tukapiga nalo picha..
Rais wa kwanza toka Africa kumtembelea Obama
Amewakaribisha wasanii wa bongo flava ikulu kupiga nao stori
Ameendesha mahojiano ya ana kwa ana live kupitia luninga....
Mhudhuriaji mzuri kwenye misiba,graduations na birthdays..(hata walalahoi tulipata nafasi ya kumshika mkono).
Kuna mwaka Miss Utalii ilitaka kushindikana kufanyika kwa kukosekana fedha ,akaiokoa na ikafanyika
Sasa watz wenzangu hapo nyumbani mngeyaona wapi yote hayo ???asili ya binadamu ..akiondoka ndiyo mtamkumbuka kwa 'mema'...

Hizi ni kama decorations tu katika nyumba mtu atakayekuja ku evaluate thamani ya nyumba huwa haviangalii na sisi hapa sidhani kama hivyo vitatusaidia kum evaluate JK hata nyumba za makuti ndani huwa na mapambo lakini hayawezi kuongeza thamani ya nyumba
 
Back
Top Bottom