asante kwa kujitolea rais wetu ubarikiwe sana maana unachoka sana na hizo safari lakini kwa kuwa uliahidi kututumikia watanzania kwa moyo mmoja unafanya hayo maana mwingine angejifungia ikulu na kula bata hongera mkuu kikwetw ubarikiwe tena
Tena anakutana na boss wa TOTAL hapo lazima waongelee gas ya MTWARAkimpango wakee,na hizo safari za ajabu ajabu zisizo na tija wala maana yoyote kwetu sisi lazima zije zimtokee puani,waziri wa mambo ya nje anafanya nini??na sikun hizi anakuja na janja kwamba kaalikwa nani amwalike yeye??aliikwe ana nini??
Na huko uswisw anakokwenda haendi kutembelea shirikisho la soka wala nini??anaenda kuzidi kuweka 10 percent za gsei yetu tuu,tulaani dhulma kama hizi
Pro-Chadema JF vipi vikwazo vya UN vimeisha.
Rais Kikwete ataondoka nchini Ufaransa Jumatano, Januari 23,2013, kwenda Uswisi ambako atatembelea Makao Makuu ya Shirikishola Soka Duniani (FIFA) mjini Zurich
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
RAIS wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa JakayaMrisho Kikwete anaanza ziara rasmi ya Kiserikali nchini Ufaransa leo, Jumamosi, Januari 19, 2013, kwa mwaliko wa Rais wa Ufaransa,Mheshimiwa Francois Hollande.Rais Kikwete na ujumbe wake aliondoka nchini usiku wa kuamkia leo, Jumamosi, kwa ndege ya Shirika la Ndege la Uswisi kuelekea Ulaya kwa ajili ya ziara hiyo.Mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Charles DeGaul mjini Paris leo jioni, Rais Kikwete ambaye anafuatana na Mama Salma Kikwete atapokelewa rasmi katika Ufaransa kwa gwaride nakupokelewa na Waziri wa Misaada ya Maendeleo wa Ufaransa,Mheshimiwa Paschal Canfin.
Kwa mujibu wa ratiba, kesho, Rais Kikwete atakutana na kufanyamazungumzo na Mama Frannie Leautiera mbaye ni Mtendaji Mkuu waMfuko Private Fund na baadaye atakutana na Mama Marie Christine Saragosse, Mtendaji Mkuu wa Redio France International (RFI).
Mkutano huo utafuatiwa na kikao kati ya Rais Kikwete na Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini Ufaransa.
Kesho kutwa, Jumatatu, Rais Kikwete atakutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Francois Hollande, Rais wa Ufaransa kwenye Kasri ya nchi hiyo ya Elysee Palace.Mazungumzo kati ya Rais Kikwete na Rais Hollande yatafuatiwana chakula cha mchana ambako Rais Kikwete atakaribishwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Mheshimiwa Laurent Fabius.
Baada yachakula hicho cha mchana, Rais Kikwete atakutana na kuzungumza na Bwana Yves Louis Darricarere, Rais wa Kampuni ya Mafuta yaKimataifa ya Total.
Mazungumzo hayo yatafuatiwa na mazungumzo mengine kati ya Rais Kikwete na Kiongozi wa Madhehebu ya Ismailia Duniani H.H The Aga Khan na baada ya hapo, Rais Kikwete atakwenda Kasri la Luxemburg kukutana na kuzungumza na Rais wa Bunge la Seneti laUfaransa, Mheshimiwa Jean Pierre Bel.Usiku wa Jumatatu, RaisKikwete atakula chakula cha usiku naRais wa zamani wa Ufaransa, Mheshimiwa Valery Giscard d'Estaingambaye ni Mwenyekiti wa Tanzania Wildlife Conservation Foundation.
Jumanne, Rais Kikwete atakuwa na siku nyingine yenye shughulinyingi ambako miongoni mwa mambo mengine atakutana na kufanya mazungumzo na mabalozi wa Afrika wanaowakilisha nchi zao katika Ufaransa, na atakutana na Mheshimiwa Abdou Diouf, Katibu Mkuu wa Umoja wa Kimataifa wa Nchi Zinazongumza Lugha ya Kifaransa na Rais wa zamani wa Senegal.
Rais Kikwete pia atashiriki majadiliano kuhusu masuala yakimataifa yaliyoandaliwa na Taasisi ya Mahusiano ya Kimataifa yaUfaransa – Institute Francais Des Relations International (IFRI) naatakutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Ufaransa (AFD).
Rais Kikwete ataondoka nchini Ufaransa Jumatano, Januari 23,2013, kwenda Uswisi ambako atatembelea Makao Makuu ya Shirikishola Soka Duniani (FIFA) mjini Zurich na baadaye kwenda Davos kuhudhuria mkutano wa mwaka huu wa Shirika la Uchumi Duniani –World Economic Forum (WEF).
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONSRAIS wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete anaanza ziara rasmi ya Kiserikali nchini Ufaransa leo, Jumamosi, Januari 19, 2013, kwa mwaliko wa Rais wa Ufaransa, Mheshimiwa Francois Hollande.
Telephone: 255-22-2114512,2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com / press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENTS OFFICE, THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,DAR ES SALAAM
Tanzania
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Kikwete na ujumbe wake aliondoka nchini usiku wa kuamkia leo, Jumamosi, kwa ndege ya Shirika la Ndege la Uswisi kuelekea Ulayakwa ajili ya ziara hiyo.
Mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Charles DeGaul mjini Paris leo jioni, Rais Kikwete ambaye anafuatana na Mama Salma Kikwete atapokelewa rasmi katika Ufaransa kwa gwaride nakupokelewa na Waziri wa Misaada ya Maendeleo wa Ufaransa, Mheshimiwa Paschal Canfin.
Kwa mujibu wa ratiba, kesho, Rais Kikwete atakutana na kufanya mazungumzo na Mama Frannie Leautiera mbaye ni Mtendaji Mkuu wa Mfuko Private Fund na baadaye atakutana na Mama Marie Christine Saragosse, Mtendaji Mkuu wa Redio France International (RFI).
Mkutano huo utafuatiwa na kikao kati ya Rais Kikwete na Jumuiya yaWatanzania wanaoishi nchini Ufaransa.
Keshokutwa, Jumatatu, Rais Kikwete atakutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Francois Hollande, Rais wa Ufaransa kwenye Kasri ya nchi hiyo ya Elysee Palace.
Mazungumzo kati ya Rais Kikwete na Rais Hollande yatafuatiwana chakula cha mchana ambako Rais Kikwete atakaribishwa na Waziriwa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Mheshimiwa Laurent Fabius. Baada ya chakula hicho cha mchana, Rais Kikwete atakutana na kuzungumza na Bwana Yves Louis Darricarere, Rais wa Kampuni ya Mafuta yaKimataifa ya Total.
Mazungumzo hayo yatafuatiwa na mazungumzo mengine kati yaRais Kikwete na Kiongozi wa Madhehebu ya Ismailia Duniani H.H TheAga Khan na baada ya hapo, Rais Kikwete atakwenda Kasri la Luxemburg kukutana na kuzungumza na Rais wa Bunge la Seneti la Ufaransa, Mheshimiwa Jean Pierre Bel.
Usiku wa Jumatatu, RaisKikwete atakula chakula cha usiku naRais wa zamani wa Ufaransa, Mheshimiwa Valery Giscard dEstaingambaye ni Mwenyekiti waTanzania Wildlife Conservation Foundation. Jumanne, Rais Kikwete atakuwa na siku nyingine yenye shughuli nyingi ambako miongoni mwa mambo mengine atakutana nakufanya mazungumzo na mabalozi wa Afrika wanaowakilisha nchi zaokatika Ufaransa, na atakutana na Mheshimiwa Abdou Diouf, KatibuMkuu wa Umoja wa Kimataifa wa Nchi Zinazongumza Lugha yaKifaransa na Rais wa zamani wa Senegal.
Rais Kikwete pia atashiriki majadiliano kuhusu masuala yakimataifa yaliyoandaliwa na Taasisi ya Mahusiano ya Kimataifa yaUfaransa Institute Francais Des Relations International (IFRI) naatakutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika laMaendeleo ya Kimataifa la Ufaransa (AFD).
Rais Kikwete ataondoka nchini Ufaransa Jumatano, Januari 23,2013, kwenda Uswisi ambako atatembelea Makao Makuu ya Shirikishola Soka Duniani (FIFA) mjini Zurich na baadaye kwenda Davoskuhudhuria mkutano wa mwaka huu wa Shirika la Uchumi Duniani World Economic Forum (WEF).
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu
Dar es Salaam.
19 Januari, 2013
who wrote this statement from Ikulu? Salva or Premi???....ingekuwa vizuri wawe wanaandika majina yao tuwajue.....Wanaandika kumfagilia JK...lakini wanaonyesha ujuha wao pia...Hii statement haiko detailed hata kidogo...zaidi ya kuonyesha maeneo atakayokwenda JK....Atazungumzia nini....na kwa maslahi gani kwa taifa hawasemi.....what mediocres eh!!THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONSRAIS wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete anaanza ziara rasmi ya Kiserikali nchini Ufaransa leo, Jumamosi, Januari 19, 2013, kwa mwaliko wa Rais wa Ufaransa, Mheshimiwa Francois Hollande.
Telephone: 255-22-2114512,2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com / press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT'S OFFICE, THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,DAR ES SALAAM
Tanzania
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Kikwete na ujumbe wake aliondoka nchini usiku wa kuamkia leo, Jumamosi, kwa ndege ya Shirika la Ndege la Uswisi kuelekea Ulayakwa ajili ya ziara hiyo.
Mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Charles DeGaul mjini Paris leo jioni, Rais Kikwete ambaye anafuatana na Mama Salma Kikwete atapokelewa rasmi katika Ufaransa kwa gwaride nakupokelewa na Waziri wa Misaada ya Maendeleo wa Ufaransa, Mheshimiwa Paschal Canfin.
Kwa mujibu wa ratiba, kesho, Rais Kikwete atakutana na kufanya mazungumzo na Mama Frannie Leautiera mbaye ni Mtendaji Mkuu wa Mfuko Private Fund na baadaye atakutana na Mama Marie Christine Saragosse, Mtendaji Mkuu wa Redio France International (RFI).
Mkutano huo utafuatiwa na kikao kati ya Rais Kikwete na Jumuiya yaWatanzania wanaoishi nchini Ufaransa.
Keshokutwa, Jumatatu, Rais Kikwete atakutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Francois Hollande, Rais wa Ufaransa kwenye Kasri ya nchi hiyo ya Elysee Palace.
Mazungumzo kati ya Rais Kikwete na Rais Hollande yatafuatiwana chakula cha mchana ambako Rais Kikwete atakaribishwa na Waziriwa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Mheshimiwa Laurent Fabius. Baada ya chakula hicho cha mchana, Rais Kikwete atakutana na kuzungumza na Bwana Yves Louis Darricarere, Rais wa Kampuni ya Mafuta yaKimataifa ya Total.
Mazungumzo hayo yatafuatiwa na mazungumzo mengine kati yaRais Kikwete na Kiongozi wa Madhehebu ya Ismailia Duniani H.H TheAga Khan na baada ya hapo, Rais Kikwete atakwenda Kasri la Luxemburg kukutana na kuzungumza na Rais wa Bunge la Seneti la Ufaransa, Mheshimiwa Jean Pierre Bel.
Usiku wa Jumatatu, RaisKikwete atakula chakula cha usiku naRais wa zamani wa Ufaransa, Mheshimiwa Valery Giscard d'Estaingambaye ni Mwenyekiti waTanzania Wildlife Conservation Foundation. Jumanne, Rais Kikwete atakuwa na siku nyingine yenye shughuli nyingi ambako miongoni mwa mambo mengine atakutana nakufanya mazungumzo na mabalozi wa Afrika wanaowakilisha nchi zaokatika Ufaransa, na atakutana na Mheshimiwa Abdou Diouf, KatibuMkuu wa Umoja wa Kimataifa wa Nchi Zinazongumza Lugha yaKifaransa na Rais wa zamani wa Senegal.
Rais Kikwete pia atashiriki majadiliano kuhusu masuala yakimataifa yaliyoandaliwa na Taasisi ya Mahusiano ya Kimataifa yaUfaransa – Institute Francais Des Relations International (IFRI) naatakutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika laMaendeleo ya Kimataifa la Ufaransa (AFD).
Rais Kikwete ataondoka nchini Ufaransa Jumatano, Januari 23,2013, kwenda Uswisi ambako atatembelea MakaoMakuu ya Shirikishola Soka Duniani (FIFA) mjini Zurich na baadaye kwenda Davoskuhudhuria mkutano wa mwaka huu wa Shirika la Uchumi Duniani – World Economic Forum (WEF).
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu
Dar es Salaam.
19 Januari, 2013