Rais Kikwete kwenye ziara ya kiserikali nchini Ufaransa

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


Telephone: 255-22-2114512,2116898
E-mail:
ikulumawasiliano@yahoo.com / press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT'S OFFICE, THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,DAR ES SALAAM
Tanzania


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

RAIS wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete anaanza ziara rasmi ya Kiserikali nchini Ufaransa leo, Jumamosi, Januari 19, 2013, kwa mwaliko wa Rais wa Ufaransa, Mheshimiwa Francois Hollande.

Rais Kikwete na ujumbe wake aliondoka nchini usiku wa kuamkia leo, Jumamosi, kwa ndege ya Shirika la Ndege la Uswisi kuelekea Ulayakwa ajili ya ziara hiyo.

Mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Charles DeGaul mjini Paris leo jioni, Rais Kikwete ambaye anafuatana na Mama Salma Kikwete atapokelewa rasmi katika Ufaransa kwa gwaride nakupokelewa na Waziri wa Misaada ya Maendeleo wa Ufaransa, Mheshimiwa Paschal Canfin.

Kwa mujibu wa ratiba, kesho, Rais Kikwete atakutana na kufanya mazungumzo na Mama Frannie Leautiera mbaye ni Mtendaji Mkuu wa Mfuko Private Fund na baadaye atakutana na Mama Marie Christine Saragosse, Mtendaji Mkuu wa Redio France International (RFI).

Mkutano huo utafuatiwa na kikao kati ya Rais Kikwete na Jumuiya yaWatanzania wanaoishi nchini Ufaransa.

Keshokutwa, Jumatatu, Rais Kikwete atakutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Francois Hollande, Rais wa Ufaransa kwenye Kasri ya nchi hiyo ya Elysee Palace.

Mazungumzo kati ya Rais Kikwete na Rais Hollande yatafuatiwana chakula cha mchana ambako Rais Kikwete atakaribishwa na Waziriwa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Mheshimiwa Laurent Fabius. Baada ya chakula hicho cha mchana, Rais Kikwete atakutana na kuzungumza na Bwana Yves Louis Darricarere, Rais wa Kampuni ya Mafuta yaKimataifa ya Total.

Mazungumzo hayo yatafuatiwa na mazungumzo mengine kati yaRais Kikwete na Kiongozi wa Madhehebu ya Ismailia Duniani H.H TheAga Khan na baada ya hapo, Rais Kikwete atakwenda Kasri la Luxemburg kukutana na kuzungumza na Rais wa Bunge la Seneti la Ufaransa, Mheshimiwa Jean Pierre Bel.

Usiku wa Jumatatu, RaisKikwete atakula chakula cha usiku naRais wa zamani wa Ufaransa, Mheshimiwa Valery Giscard d'Estaingambaye ni Mwenyekiti waTanzania Wildlife Conservation Foundation. Jumanne, Rais Kikwete atakuwa na siku nyingine yenye shughuli nyingi ambako miongoni mwa mambo mengine atakutana nakufanya mazungumzo na mabalozi wa Afrika wanaowakilisha nchi zaokatika Ufaransa, na atakutana na Mheshimiwa Abdou Diouf, KatibuMkuu wa Umoja wa Kimataifa wa Nchi Zinazongumza Lugha yaKifaransa na Rais wa zamani wa Senegal.

Rais Kikwete pia atashiriki majadiliano kuhusu masuala yakimataifa yaliyoandaliwa na Taasisi ya Mahusiano ya Kimataifa yaUfaransa – Institute Francais Des Relations International (IFRI) naatakutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika laMaendeleo ya Kimataifa la Ufaransa (AFD).

Rais Kikwete ataondoka nchini Ufaransa Jumatano, Januari 23,2013, kwenda Uswisi ambako atatembelea Makao Makuu ya Shirikishola Soka Duniani (FIFA) mjini Zurich na baadaye kwenda Davoskuhudhuria mkutano wa mwaka huu wa Shirika la Uchumi Duniani – World Economic Forum (WEF).

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu
Dar es Salaam.
19 Januari, 2013
attachment.php


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu, kesho Rais Jakaya Kikwete atakutana na kufanya mazungumzo na MAMA FRANNIE LEAUTIERA,anayetajwa kuwa ni Mtendaji Mkuu wa MFUKO PRIVATE FUND.

Nimejaribu kufanya utafiti mtandaoni lakini jina la karibu linaloshabihiana na la mwanamama huyo ni FRANNIE LEAUTIER (pichani juu)

Lakini jitihada zangu za kutafuta MFUKO PRIVATE FUND (taasisi ambayo taarifa hiyo ya Ikulu inaeleza kuwa Mama Leautiera ni Mtendaji Mkuu) hazijazaa matunda.

Je, Ikulu walimaanisha Frannie Leautier lakini wakaongeza herufi 'A' kimakosa, hivyo kusomeka LEAUTIERA badala ya LEAUTIER?

Tukiamini hilo ni kosa dogo tu la kiuandishi, je MFUKO PRIVATE FUND ni taasisi gani? Na kwanini Rais akutane na Mtendaji Mkuu wake?

Unaweza kudhani maswali haya hayana umuhimu lakini kwa vile taarifa zimeshasambaa duniani kuwa tuna utajiri 'mpya' wa gesi, basi ni vema kufahamu viongozi wetu wanakutana na watu wa aina gani wanapokuwa ziarani huko nje.

Kama mnavyojua, kabla na wakati wa ukoloni akina Karl Peters walipita huko na kule kusaini mikataba ya kilaghai ya kuchukua ardhi na raslimali zetu. Siku hizi, baadhi ya viongozi wa Afrika ndio wamegeuka akina Karl Peters kwa aidha kukaribisha 'wakoloni wapya' au kuwafuata huko makwao kusaini mikataba ya kuuza nchi yetu.

Ni matarajio yangu kuwa Ikulu itajitahidi kutoa ufafanuzi kuhusu suala hili.

Mama Frannie Leautiera Atakayekutana na Kikwete Ufaransa ni Nani? Na MFUKO PRIVATE FUND ni nini? ~ Kulikoni Ughaibuni

 
Kumbe kwenda FIFA ni moja ya majukumu ya raisi wa nchi,duh au ndo kaenda kucheki ule mgao wa uswis,naombeni kuuliza ivi wewe ukiwa na nyumba ya kupangisha ni wewe ndo unaenda kuonana na huyo unaetegemea kumpangisha sehemu anayoishi au ni yule anayetafuta nyumba ya kupanga ndo anatakiwa aje?????
 
Vasco da gama again? Sjui kwanini TZ ni maskini

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Annaenda kuumuuzia pande la nchi ya ngara huko akachimbe Nikel au Platinum huko namtumbo na ludewa mpaka anaondoka atamalizia kwa kutuuza sisi wenyewe IKULU bila aibu wanasema atapokelewa kwa gwaride kwa nini asipokelewe kwa gwaride wakijua atatoa mapande ya nchi wajinome kuvuna rasirimali ha ha nchi hii ni kichwa cha mwenda wazimu akirudi viongozi 100 watakuwa airport kumpokea
 
kimpango wakee,na hizo safari za ajabu ajabu zisizo na tija wala maana yoyote kwetu sisi lazima zije zimtokee puani,waziri wa mambo ya nje anafanya nini??na sikun hizi anakuja na janja kwamba kaalikwa nani amwalike yeye??aliikwe ana nini??

Na huko uswisw anakokwenda haendi kutembelea shirikisho la soka wala nini??anaenda kuzidi kuweka 10 percent za gsei yetu tuu,tulaani dhulma kama hizi
 
Aibu gani hii watanzania tunayotwikwa ameshindwa kushughulikia sakata la mtwara huyoooooo kiguu na njia.
 
asante kwa kujitolea rais wetu ubarikiwe sana maana unachoka sana na hizo safari lakini kwa kuwa uliahidi kututumikia watanzania kwa moyo mmoja unafanya hayo maana mwingine angejifungia ikulu na kula bata hongera mkuu kikwetw ubarikiwe tena
 
Back
Top Bottom