Ringo Edmund
JF-Expert Member
- May 10, 2010
- 4,879
- 1,125
Rais umekuwa mwepesi kuliko marais wote niliowahi kuwasikia hapa duniani. Kwanza nijuavyo Rais ni kiongozi na kiongozi ni lazima akae mbele ili aliongoze kundi mahali pa kuelekea.
Na kauli ya Rais najua ni ya mwisho, hatakiwi kukurupuka kuzungumza kwani ana washauri wa kutosha.
Kauli za Kikwete zenye utata.
1. Mimi ni mmoja wa wasiotaka DOWANS isilipwe, wewe kama rais unaungana na wananchi kulia nani wa kutusaidia?
Je unataka tufunge na kuomba ili Mungu atuondolee DOWANS?
Kwani ulikaa kimya muda mrefu tukawa tunakusubiri labda utatuokoa na hiki kikombe kichungu lakini kumbe na wewe huna msaada.
2. Uzio uliojengwa jangwani ubomolewe, ulipotoa hilo agizo nikawa nasubiri utekelezaji, lakini wapi, halmashauri nimesikia imegoma.
Sasa najiuliza je unajua uzito wa kauli yako kwa sasa kama rais na si kama Jakaya? Ni bora usiwe unazungumza rais wangu kwani sauti yako walio chini yako wameizoea mpaka sidhani kama wanakusikiliza tena.
3.Sijui kwa nini Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali zote zilizopo, hapo ndipo ulinichosha sana rais wangu. Uliomba kuwa rais wa Tanzania ili kiwe nini?
Nakuombea umalize miaka yako minne iliyobaki kwa amani ili tujipange upya ila kwa hayo sikusamehi.