Rais Kikwete, baba mbakaji na utata wa mtoto aliyezaliwa

Mkuu mbona ueleweki utaka kusema nini unachosema, mfano wako ni dhaifu sana.

Kuhusu Dk Slaa na mtazamo wako ni hadithi za Abunuasi na mke wake Elizabeti, eti angetangaza watu waingie barabarani saizi angekuwa Makamu wa Rais.

Mtazamo na muelekeo wako kisiasa na wasiwasi nao

Umechukua sehemu ndogo story na kujenga hoja hasi. Kijumla nilimaanisha kwamba angekuwa na uroho wa madaraka angeleta machafuko kama kenya. Ingefuata mwafaka, halafu kama zilivyo nchi nyingi za afrika, angekuwa serikalini. Sasa hiyo ina uhusiano gani na mtazamo wangu kisiasa? Kwa ufupi mimi nilipenda jinsi alivyoweka taifa mbele bila kujali mimi ni Chadema au sina chama.
 
Hata kama dr slaa aliamua kuwa mvumilivu lakini bado anawajibika kwetu watanzania kuweka ukweli wazi wa alivyoibiwa kura na takwimu sahihi badala ya kila siku kutaja waliowaibia. Kutaja hata mimi naweza kutaja ni jambo jepesi

Unajua kwamba baadhi ya ushahidi alionao Dr Slaa (siyo wote) zinafifia kadri siku zinavyokwenda - yaani zile copy za karatasi za kurekodi idadi ya kura vituoni. CCM wanatumia akili nyingi sana kuiba kura. Laiti wangetumia akili hiyo kuendeleza Tanzania tungekuwa mbali sana. Kwa hiyo, ushahidi tulio nao unatutosha kutulinda kama CCM wataenda mahakamani kutushtaki. Najua hawaendi.
 
baba huwezi kumkana lakini unaweza kuvunja mawasiliano na mahusiano naye hadi kaburi

Really?
Tunaweza kuvunja mahusiano na serikali jumla? Kwa katiba iliyopo haiwezekani - labda uhame nchi.
Unataka kusema viongozi wote wa Chadema ambao wanafanya kazi serikalini wajiuzulu? Tugome kutumia pesa zote za Tanzania kwa sababu ni mali ya benki ya serikali ya ccm? Inawezekana?
Tuache kwenda kutibiwa ktk hospitali za serikali? Tusiende ktk shule za serikali? Haiwezekani. Tasisi zote hizo pia zinaendeshwa kwa kodi za watanzania wote wakiwepo wanachadema. Hatuwezi kumsusia mlevi pombe - atakunywa na kufurahia.
 
tatizo lako hutaki kukubali kwamba Dr slaa alishindwa kwa sababu wewe ni chadema unajenga hoja dhaifu badala ya kumwaga ushahidi hapa unaosema unao. Haitoshi tu kusema tume na Usalama wa taifa waliiba lete hapa takwimu za majimbo yote ya tanzania na eleza jinsi ccm walivyoiba. tumechoka na wimbo huu

Badala ya kutaka mimi nifanye kazi hiyo ngumu, mimi nadhani ungeungana na mimi na kuwauliza tume ya Taifa ambao tumewaajiri kwa kodi zetu, kwanini hawakuweka matokeo yote hadharani? Kwanini wanamtangaza rais kutokana data za mifukoni mwao? Kwa nini mawakala wa Chadema na waangalizi wa kimataifa hawakuruhusiwa kuwepo wakati wa kujumlisha kura za Rais?
 
Mkuu salama?
Usipoteze nguvu zako nyingi kumjibu huyo mdau, si kwamba hakuelewi, hasha anakuelewa sana.
Anachokifanya hapa ni kujaribu kuipuuza hoja yako ambayo ni ya kweli na wenye ufahamu wao na kuchanganya na zao wanajua ukweli.
 
Mkuu mbona ueleweki utaka kusema nini unachosema, mfano wako ni dhaifu sana.

Kuhusu Dk Slaa na mtazamo wako ni hadithi za Abunuasi na mke wake Elizabeti, eti angetangaza watu waingie barabarani saizi angekuwa Makamu wa Rais.

Mtazamo na muelekeo wako kisiasa na wasiwasi nao

Abunuwasi hajawahi kuwa na mke aitwaye elizabeti, bali bulicheka amewahi, kwa ukweli niliokupangia jua kuwa wewe ni muongo!!!!!! na bandiko lako ni uongo mtupu.
 
Mkuu Wab,

Mbaya zaidi badala ya kwenda maeneo ambayo CDM hawajawafikia wapiga kura wamekazana kila siku Arusha !.Pwana na kusini ndiyo maeneo yakutembelewa ianzishwe operesheni nyingine kama Sangara.Tazama uchaguzi wa mwaka 2010 Igunga hawakuweka mgombea kama kusingekuwa na uchaguzi wangesubiri mwaka 2015.

Mheshimiwa sana Ngongo,
Mwaka huu Dr Slaa alikuwa Pwani, alianzia Kisarawe mjini mkoa wa Pwani na alizunguka huko kata kwa kata. Sikumbuki idadi ya kata alizokwenda na wilaya alizokwenda. Mwezi uliopita kulikuwa na uzinduzi wa ofisi mpya ya Chadema chalinze Pwani. Dr Slaa alikuwa awe Mgeni Rasmi, akawakilishwa na Erasto Tumbo. Huo si ndo ujezi wa chama pwani? Worry not my friend.
 
Ninyi nyote wawili ni "Manzi ga nyanja", chadema hate preachers, tushawafahamu na kuwazoea!!:photo:

umekuwa addicted na uchadema hata kufikiria unashindwa.......unamfananisha slaa na odinga?

chadema vituo vingine hamkuweka wagombea na vituo vingine hamkuwa na mawakala, kusini hamkupiga campaign yet mlishinda urais.....utatukanwa siku nyingine!

Mkuu Wab,

Mbaya zaidi badala ya kwenda maeneo ambayo CDM hawajawafikia wapiga kura wamekazana kila siku Arusha !.Pwana na kusini ndiyo maeneo yakutembelewa ianzishwe operesheni nyingine kama Sangara.Tazama uchaguzi wa mwaka 2010 Igunga hawakuweka mgombea kama kusingekuwa na uchaguzi wangesubiri mwaka 2015.
 
Hii tuhuma "Chadema hajawahi kusema hawamtambui rais, na hawawezi kufanya hivyo kikatiba, ila waliwahi kulalamika baba yao ( Rais) kubaka demokrasia akisaidiwa na tume ya Uchaguzi na usalama wa ccm (Taifa?) na kuzaliwa mtoto( Rais). Mtoto hana utata ila njia iliyotumika ndio tatizo ( ubakaji wa demokarasia)" ilikuwa nzito sana ilitakiwa kama ni uongo Dr. atiwe ndani, kulikoni hapa kwa hiki kimya kuna harufu ya ukweli.....

aluta continua!

Wanajf,

Hivi mama yako akikuambia kuwa baba yako alinibaka, nikapata mimba, ndo ukazaliwa wewe mwanangu X. utamkana baba yako hata kama ubakaji ni kosa la jinai? Huwezi kumkana baba yako kwa sababu huo ndio ukweli ambao huwezi kuubadili. Baba yako ni baba yako bila kujali alimtongoza mama au alimbaka. Hakuna mahakama ya kubadili ubaba wa baba yako.

Nimekuwa nikijibu shutuma na propaganda nyingi zinazoelekezwa kwa makusudi au kwa kutojua kuhusu Chadema kumtambua au kutomtambua Rais. Propaganda hizi zimekuja hasa baada ya Chadema kwenda ikulu kuongea na Rais na kujadili mstakabali wa Taifa na kuepusha mgawanyiko wakati huu tunapotunga sheria itakayoongoza uundaji wa tume na uandikaji wa Rasimu ya katiba mpya. Nimekuwa nikijibu thread za namna hii, lakini nimeona niiweke ktk thread inayojitegemea ili nijibu once and for all.

Na bahati nzuri nina open ID ambayo ukitaka waweza kunipigia simu au kuniandikia email kwa maelezo zaidi.

Je, baada ya Chadema kuwa na uhakika kuwa kura zao zimeibiwa (mimi nina ushahidi wa jimbo la ubungo) na baada ya Rais kutangazwa na tume ya Taifa (ambao mpaka leo wameshindwa kuweka vizuri ktk website yao ya Tume) Chadema wangefanya nini?

Kwa mujibu wa katiba hii mbovu, kikwete ni Rais mara tu baada ya kutangazwa na tume ya uchaguzi Mbowe na Slaa watake, wasitake. Hakuna mahakama ya kupinga kutangazwa kwake na sijasema ushindi wake. Ieleweke hivyo. Kwangu mimi mshindi ni Dr Slaa, japo huu ndio ukweli mchungu.

Chadema hajawahi kusema hawamtambui rais, na hawawezi kufanya hivyo kikatiba, ila waliwahi kulalamika baba yao ( Rais) kubaka demokrasia akisaidiwa na tume ya Uchaguzi na usalama wa ccm (Taifa?) na kuzaliwa mtoto( Rais). Mtoto hana utata ila njia iliyotumika ndio tatizo ( ubakaji wa demokarasia)

Tuache ushabiki, nchi yetu iko ktk hali tete sana kuliko wakati mwingine wo wote. Tunahitaji hekima na uvumilivu wa hali ya juu.

Niliwahi kusema na narudia.

Kama Dr Slaa angetangaza kuwa nina taarifa za uhakika kuwa kura za Chadema zinaibiwa kwa hiyo watu waingie barabarani, hivi leo huyo Kikwete angekuwa ikulu? Kama jibu ni ndiyo, basi makamu wake angekuwa Dr Slaa siyo Gharib Bilal. Hii ni baada ya damu nyingi za watanzaniakumwagika sana.

Ifahamike tofauti kati ya Raila Odinga wa Kenya na Dr W Slaa ni uvumilivu. Raila aliwaambia watu waingie barabarani, Dr Slaa alivumilia akaweka Tanzania mbele kuliko urais. Wagombea urais wangapi Tanzania na Afrika ambao anapewa ushahidi wa jinsi kura zao zinavyoibiwa, halafu akakubali yaishe kama Dr Slaa?

Inasikitisha viongozi wa dini zote waliokuwa wanamshauri akubali matokeo hayo tata, leo wako kimya na wengine wako busy wanajenga ccm makanisani na misikitini.

TIME WILL TELL
 
Dr slaa hakuibiwa kura na kama angeibiwa kweli asingekubali kirahisi hivyo ni propaganda tu za kisiasa kutafuta umaarufu

Hapo penye Red,
Unapimaje kukubali au kukataa kwa Dr Slaa? Unapimaji kama alikubali kirahisi au kinguvu?
 
Mkuu salama?
Usipoteze nguvu zako nyingi kumjibu huyo mdau, si kwamba hakuelewi, hasha anakuelewa sana.
Anachokifanya hapa ni kujaribu kuipuuza hoja yako ambayo ni ya kweli na wenye ufahamu wao na kuchanganya na zao wanajua ukweli.
Mwita wa Maranya nakupata sana,
Watz wa leo siyo wa 1961. Wanajua kuchambua mchele na pumba.
 
Mkuu MM bahati mbaya umeshindwa kunisoma vizuri.Mimi napenda mageuzi yakiletwa na CDM sawa,yakiletwa na CUF sawa,yakiletwa na NCCR Mageuzi sawa,yakiletwa na TLP sawa,yakiletwa na UDP sawa,yakiletwa na CCM sawa duh bahati mbaya magamba hawawezi kufanya maamuzi magumu nimewarule out !.

Mkuu wngu tofauti yangu na wewe ni moja tu !.Wewe huna uwezo wa kukosoa upuuzi unaofanywa au utakaofanywa na viongozi wa CDM.Mimi wakikosea nawakosoa wakifanya mambo ya maana nawasifia kwangu mimi CDM ni chama kinachoongozwa na binadamu wenye madhaifu mengi hivyo kukosolewa na kusahihishwa ni jambo la kawaida.CDM wanavuna na kufyonza zaidi toka kwangu mambo ya maana ikilinganishwa na wewe unaiisifia hata kwenye mambo ya kijinga.

Ninyi nyote wawili ni "Manzi ga nyanja", chadema hate preachers, tushawafahamu na kuwazoea!!:photo:
 
Mkuu MM bahati mbaya umeshindwa kunisoma vizuri.Mimi napenda mageuzi yakiletwa na CDM sawa,yakiletwa na CUF sawa,yakiletwa na NCCR Mageuzi sawa,yakiletwa na TLP sawa,yakiletwa na UDP sawa,yakiletwa na CCM sawa duh bahati mbaya magamba hawawezi kufanya maamuzi magumu nimewarule out !.

Mkuu wngu tofauti yangu na wewe ni moja tu !.Wewe huna uwezo wa kukosoa upuuzi unaofanywa au utakaofanywa na viongozi wa CDM.Mimi wakikosea nawakosoa wakifanya mambo ya maana nawasifia kwangu mimi CDM ni chama kinachoongozwa na binadamu wenye madhaifu mengi hivyo kukosolewa na kusahihishwa ni jambo la kawaida.CDM wanavuna na kufyonza zaidi toka kwangu mambo ya maana ikilinganishwa na wewe unaiisifia hata kwenye mambo ya kijinga.

Yaani Slaa anaweza kumwambia chochote huyu jamaa na akasema sawa!

hawatuelewi wala hawatatuelewa wakija kutuelewa itakuwa too late....

Tunataka CCM itoke, lakini watoaji wa CCM hatutaki wawe na vi-element vya CCM!
 
Kwa hiyo waberoya,
Unaipa nguvu hoja yangu kwa ccm ni wezi wa kura. Kwa sababu una maanisha kuwa kila mahali ambapo chadema hawajaweka wakala chadema hawapati kura kwa sababu mawakala wa ccm na wasimamizi wa serikali ya ccm kila kituo waliiba kura ya chadema. My goodness. Kwa hiyo, na kila kituo ambapo wakala alipata udhuru au aliugua kura zote zimekombwa na ccm. Kama ndivyo, tuna serikali au tuna wezi?

kama ulijua sio wezi kwa nini mliweka mawakala sehemu zingine....??
kama ulijua ni wezi kwanini sehemu zingine hamkuweka mawakala?

Lengo la mawakala ni nini?

Kubali kosa, kaeni chini, jipangeni wote tuko pamoja. Kutetea uozo huu kwa hoja dhaifu za namna hii, nitaku-discredit na nitakufanya ujione huna hadhi hata ya kuwa balozi wa nyumba kumi kumi!

you guys kila chalenji mnajitetea utumbo tu......take that chalenji ebo!!
 
Mkuu MM bahati mbaya umeshindwa kunisoma vizuri.Mimi napenda mageuzi yakiletwa na CDM sawa,yakiletwa na CUF sawa,yakiletwa na NCCR Mageuzi sawa,yakiletwa na TLP sawa,yakiletwa na UDP sawa,yakiletwa na CCM sawa duh bahati mbaya magamba hawawezi kufanya maamuzi magumu nimewarule out !.

Mkuu wngu tofauti yangu na wewe ni moja tu !.Wewe huna uwezo wa kukosoa upuuzi unaofanywa au utakaofanywa na viongozi wa CDM.Mimi wakikosea nawakosoa wakifanya mambo ya maana nawasifia kwangu mimi CDM ni chama kinachoongozwa na binadamu wenye madhaifu mengi hivyo kukosolewa na kusahihishwa ni jambo la kawaida.CDM wanavuna na kufyonza zaidi toka kwangu mambo ya maana ikilinganishwa na wewe unaiisifia hata kwenye mambo ya kijinga.

Ha ha haaa Ngongoooo,

Mbona unajikweza hivyo? kiongozi gani wa chadema anayefyonza na kuvuna ushauri wako? wewe si ulikuja hapa kulalamika kwamba Lema ameshindwa kutekeleza ushauri wako kwenye lile saga la madiwani, ama ulikuwa umelewa siku hiyo hata hukumbuki ulichoandika!? sasa kama tunayo maandiko yako unalalamika chadema kutokubali ushauri wako na kutoshaurika ni nani huyo tena anayefyonza na kuvuna ushauri wako ambao kwa kipimo cha kawaida ni mbovu.

Ngongo ni kweli mimi na wewe tuna tofauti kubwa sana kimtazamo na kiuwezo. Mimi niko mstari wa mbele katika kupigania mageuzi ya kweli ndani ya nchi hii wakati wewe umesimama kando unatutupia mawe na kulalamika tu. Mimi nikiwa mwanachama hai wa chadema na ni kiongozi ninatumia nafasi yangu ya vikao ndani ya chama kutoa ushauri na mapendekezo mbalimbali namna ya kukiimarisha chama, kama una mashaka na hilo karibu sana ukonga ndipo utajua kwamba tunafanya nini, sio nyie mnaojua kuchonga tu kwenye mitandao lakini kwenye ground hamuonekani.

Ni kweli chadema inaongozwa na binadamu na kwahiyo kutenda makosa si jambo la ajabu lakini katika hili hawajatenda kosa, hao unaowashabikia wa vyama vingine wanafanya makosa ya makusudi na huwasemi ama unawaona wa maana!? Ukweli uko dhahiri kwamba chadema ndicho chama pekee cha kisiasa chenye vision ya kweli kwa watanzania, na ndio maana tunazidi kupata uungwaji mkono kwa kasi na kwa wingi sana, tena na vijana wasomi wa vyuo vikuu, hivi karibuni tunafungua tawi la chadema Kampala International University (KIU) gongo la mboto karibu ushuhudie jinsi chadema inavyokumbatiwa na watanzania wenye mapenzi mema na nchi yao.
 
Yaani Slaa anaweza kumwambia chochote huyu jamaa na akasema sawa!

hawatuelewi wala hawatatuelewa wakija kutuelewa itakuwa too late....

Tunataka CCM itoke, lakini watoaji wa CCM hatutaki wawe na vi-element vya CCM!

Huna hoja siku hizi mkuu, umejaribu hata kutumia multiple IDs kuishambulia chadema bila mafanikio.

Siku tukikamata uongozi tutakukaribisha chai, tunajua unatumika bila kujua!
 
Mkuu wangu MM.

Yaani unataka nisifu viongozi wanaowaambia watu wakeshe uwanja wa NMC kisa Lema kagomea dhamana ?.

Mkuu ukiniambia nikishe NMC kwaajili ya katiba mpya nitakuelewa.

Mkuu ukiniambia niandamane kwaajili ya kupinga ongezeko la posho za wabunge nitakuelewa.

Mkuu ukiniambia niandamane kwaajili ya kupinga malipo ya Dowans nitafanya hivyo bila kulazimishwa.

Mkuu ukiniambia niende mahakamani kwania ya kumsindikiza mbunge anayelipwa mamilioni ya kodi nitakataa hajalishi mbunge huyo anatoka chama gani kwangu mimi wabunge wote ni wezi na wanyonyaji lazima katiba mpya iweke kipengele cha kudhibiti posho za wabunge,mawaziri,mabalozi na nk.

Mkuu CDM si Mungu ndiyo maana sioni taabu kukikosoa umeniambia wewe ni kiongozi sawa ebu pita makao makuu uliza Ngongo amefanya nini kwa mbunge wa Arusha kuhusiana na sakata la General Tyre.Pamoja na kumsaidia hainizuii kumkosoa Lema ninapoona anakwenda ndivyo sivyo.

Back
Top Bottom