Kabembe
JF-Expert Member
- Feb 11, 2009
- 2,548
- 1,741
Ni moja ya mbinu za CCM kuwapumbaza wabunge wao wenye misimamo mikali ingawa kwetu sisi wanainchi haina maana na ni kubana nafasi kwa watanzania wengine wenye uwezo.Leo Mh. Raisi wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania ameteua waku wa mikoa na kuwapandisha hadhi baadhi ya wakuu wa wilaya kuwa wakuu wa Mikoa. Mmoja wa wateule hao ni Mh. Eng. Stela Manyanya (MB). Mimi hapa ndipo ninapo hitaji ufafanuzi, hivi ni kwa nini Mbunge ateuliwe tena kuwa Mkuu wa Mkoa?? Najua huyu si wa kwanza kuna wengi walisha wahi kuwa wabunge na wakuu wa mikoa. Hapa tatizo ni nini? Je hatuna watendaji wakutosha serikalini au popote pale wasio kuwa wabunge au tatizo ni nini?? Tafadhali naomba kusaidiwa.
Nawasilisha,