Rais Kikwete asema siasa basi, sasa tuendeshe nchi kisayansi

Kwa maoni yangu, huu ujumbe wa Rais ni kwa kina Slaa, Sitta, Kilango, Mwakyembe, Zitto, Mpendazoe na kwamba huenda anamuunga mkono Kingunge ambaye upo uwezekano pia alimtuma ama walizungumza.

Kauli kama hiyo aliwahi kuitoa Mkapa siku chache kabla ya Januari 21, 2001 na baada ya hapo kilichofuatia kisiasa tunakifahamu. Hapa anakoelekea Rais ni kubaya zaidi ila anatafuta njia. Alianza katika hotuba yake kwa kusema demokrasia lazima iwe na mipaka na sasa anasema "siasa basi tuendeshe nchi" na Mkapa alisema "siasa sasa basi, uchaguzi umekwisha tujenge nchi" ndipo maandamano yakazuiwa na hali ya kisiasa ikawa nzito akatimua zake nje (kama Kikwete aivyotimua juzi) huku nyuma mzee wa watu (Marehemu Dk. Omar) huku akipokea maagizo na maelekezo kutoka kwa Ben, akafanya Press Conf sambamba na Press Conf nyingine kama hiyo kwa serikali moja na baadaye mambo yakawa mazito.

MUNGU AEPUSHIE MBALI, lakini eweee JK na watu wako, tuepusheni na machafuko, Watanzania wamechangamka musiwachokoze, endeleeni tu kuwazuga hadi muda wenu wa kutawala uishe kwa amani.
 
Ni nzuri, ila serikali yake ianze kwanza kuwajali hawa wachache tulionao. Tatizo la nchi yetu, si kwamba ni uchache tu wa wanasayansi, isipokuwa hata hawa wachache waliopo hawathaminiwi kabisa. Ndo maana wengi wanakimbilia nje ya nchi kutafuta maslahi zaidi. So, ishu si kuwa na wanasayansi wengi peke yake, je Watathaminiwa na kutumiwa?
 
Hivi Afrika kuna nini? pamoja na kuwa EPA zipo hata ulaya na asia lakini wenzetu bado wanatuacha.Ili tuendelee tunahitaji siasa SAFI, sera MUAFAKA, uongozi MAKINI + BORA, TEKNOLOJIA + ELIMU, watu makini na waliondaliwa vizuri, Aridhi + mali asili nk...Hakuna msomi asiyejua hilo, Baraza la mawaziri la Mkapa lilijaa maprof na madaktari na Most of makatibu wakuu wa wizara na wakurugenzi walikuwa wasomi wazuri tu. Hata baraza la serikali ya sasa wapo masomi wazuri...bajeti na mipango hupangwa na hao wasomi kupitia wizara zao..Kama JK ametoa changamoto kwa hao makandalasi, wao walitoa changamoto gani zaidi ya kulilia kupewa tenda zaidi kwa wazawa...harafu mpe tenda mzawa mwenyewe utasikia hadithi....hiyo ndiyo ilikuwa nafasi muafaka kwa wao kueleza mengi, sasa JK atafuata mawazo yao au ya kwenye JF? lakini pia Lowasa aliwahi kutana na wahandisi na wasomi na akawanataka watoe mapendekezo yao ama kuishauri na wangehitaji serikali ifanye kipi...hayo majibu yao pekee yalikuwa ya kukatisha tamaa...Kwa mtazamo wangu kumponda JK pekee,it will never move us forward, because there alot of factors zinazotukwamisha hata vyama vya upinzani wapo kwa msilahi yao tu,tumejifunza toka kenya.... Wambieni na hao mawaziri wake wanao subiri JK ashindwe ili wao waje wagombee, kuwa na wao ni part of our problems....
 
Na Peter Edson

...Alisema kuna haja ya ERB kuhakikisha kuwa inawapa usajili wahandisi wote nchini, ili kuhakikisha wanafuata misingi, kanuni na sheria katika kutekeleza majukumu yao ya kihandishi.

"Nawaagiza ninyi ERB kuhakikisha kuwa mnawasajili wahandisi wenye sifa zinazotakiwa kimataifa, ili wimbi hili la kuanguka kwa majengo liishe kabisa nchini,"alisisitiza Rais Kikwete.


Ni Kikwete kachanganya data, mwandishi, au mimi ambae nina tatizo la kuelewa kilichoandikwa hapo?

Nadhani tatizo ni gazeti.
 
Kikwete anaelewa maana ya siasa? Popote penye organization kuna siasa.Katika high councils za sayansi za nchi zilizoendelea huko magharibi kuna siasa, katika kuchapisha papers, kupata nishani za Nobel nk, kuna siasa.Sasa anataka watu waishi bila siasa kivipi?

Kikwete anaongelea nchi kuongozwa kisayansi na si kisiasa halafu hapo hapo yeye mwenyewe ambaye si mwanasayansi ila ni mwanasiasa anataka kuwapa pressure ya jinsi gani waandikishe wanachama wao, anafanya kile kile anachokikataa, kuendesha mambo ya kisayansi kisiasa.Kikwete is a walking contradiction.
 
sio siasa tu na udini tuache ndio tutaendelea

10rkfes.jpg
 
Siasa basi na tuachane na political economy baada ya uchaguzi. Propaganda hazitakiwi wakati huu. Nchi kama Kenya, Rwanda, Angola, na nyinginezo tunazozijua zinapata maendeleo katika kasi ya ajabu. Nchi hizo wala angalau hazitukaribii Tanzania kwa Maliasili hata kwa robo.

Sisi tumelaaniwa au nini? Siasa nyingi majukwaani, utekelezaji Hakuna. Hata Maofisa wengi serikalini ni wazito kutoa maamuzi au kujibu mahitaji ya wananchi. Hata kujibu barua au barua pepe ni ngumu. Ukiandika barua nje ya nchi unajibiwa mapema while hapa Tanzania itajibiwa baada ya miezi au isijibiwe. Waziri Mkuu amesema hili Bungeni mara nyingi. Bunge la budget.

Sasa inabidi wasaidizi wa rais kuanzia Mawaziri, mpaka makamishna wawe na kasi mpya ya utendaji. Tuepukane na Siasa kwa wakati huu.
 
After the 1998 twin bombing of USA Embassies in Tanzania and Kenya; CIA and FBI made assessment of security situation of Tanzania. Jokingly, one of the FBI agent pointed that a country like ours is only protected by God! Meaning that as a country we have no security! (But you may refute this by pointing to the WTC attack).
Now our president comes again saying that we should stop studying politics and lead our country by science.

Mie naona Mr. President ungesema Siasa za Uongo na kudanganyana sasa Basi; we have to shape our politics through science.
Surprizingly; Mr. President kwa nini ushangae kuwa tuna engineers 8000 tu? Je unajua tuna lawyers wangapi? Daktari wangapi, Economist wangapi? Even business people wangapi kwa sababu hata business people lazima waqualify kuwa business people!

Simple, our President, our planners and all in the government do not know what they are doing; we must have real statistics of how many people we need in every sector and we have to invest on that; in other words Mr. President by having population censors you can plan the needs for your people and the country at large!

Achana na SIASA za Uongo na kudanganya, shape your politics in scientific methods and good governance!
Is too long you have been talking too much!
 
Jamani mmefikiria hili?.... tokeni ndani ya kabati na sayansi na Teknologia kwanza...

1. Ni jambo la aibu kubwa Tanzania nzima kuwa na Wahandisi 8,000 tu...
sababu ya umaskini wetu sio kuendesha nchi kisiasa isipokuwa kutokuwa na wahandisi wa kutosha, kutowekea mkazo ELIMU kama ndio chimbuko la hao wahandisi na hizo Technologia..Tuna wahandisi wachache nchini kuliko idadi ya Wanasiasa si aibu hii!..

2. Huwezi kubadilisha mfumo wa nchi kiungozi kwa raia wako kwa sababu ya Technologia..yaani unaendesha nchi kisayansi ikiwa na maana tuko mwezini au?..Siasa ina nafasi yake, huwezi kuendesha nchi kwa teknologia isipokuwa unaihititaji Teknologia pale inapotakiwa ktk utendaji... Policy ambazo ndizo zinaongoza nchi hazitokani na teknologia hata kidogo.
Hakuna solution ya kitoknologia inayoweza kusolve issue za Haki na hasa hawa Mafisadi ambao sasa hivi wameturudisha nyuma..Hiyo Teknologia itawazuia nini kina Mkapa, Lowassa na Rostam kuendelea Ufisadi!... au mkuu JK alikuwa akiepusha kujibu maswali (hotuba yake) ambayo yangeandamana na issue za kisiasa. kawahi kuzizima!

Teknologia haiwezi kupima haki na Usawa wa binadamu, mdumo bora wa kiutawala, sera, ilani na kadhalika kisha kutoa hitimisho kiufundi isipokuwa Teknologia na Sayansi inakuwepo pale inapostahili baada ya siasa kufanya maamuzi. JK hakutumia Teknologia kumsafisha Lowassa ama Mkapa ila katumia siasa za kutupaka mafuta na hivyo tutaendelea kutafuta ufumbuzi kisiasa.

3. Leo hii tunaona Kikwete akiwapeleka wanajeshi na makachero kuwa mabalozi nchi za nje hali hawa watu hawana elimu kabisa ya fani hiyo!. Tumewahi shuhudia Mawaziri wakiongoza wizara bila elimu na uzoefu wakutosha, hao kina Meghji ambao wamefikia kuitumia vibaya wizara kubwa ya FEDHA kisha Waziri mzima anaweka madai kuwa nilidanganywa!.

Jamani, tusiwe wepesi sana kuamini vitu kama hivi maanake kama kweli Kikwete angekuwa anataka kuzungumza haya kwa nia safi ingekuwa wakati akifungua vyuo na vitengo zaidi vya Uhandisi, kuonyesha umuhimu wa sera hiyo ya kuongeza wataaalam toka kutegemea Wahandisi 8,000 kwa wananchi zaidi ya millioni 40..

Mkandara naweza kuungana na wewe, lakini kwa upande fulani naona nii ni danganya toto nyingine kama zilivyo nyingine. Tatizo letu sio uhaba wa wahandisi na dunia haina uhaba wa wahandisi, tatizo letu ni ufisadi uliokithiri. Ukiangalia nchi zilizoendelea utagudua kuwa kuna wahandisi wachache sana lakini wanatumiwa vizuri na wanaheshimiwa. Uhandisi sio sawa na udaktari ambao unaweza kuangalia idadi ya madaktari kwa wagonjwa. Uhandisi unaangaliwa kwa njia nyingine, mhandisi anaweza kufanya kazi mia moja bila tatizo, bora aheshimiwe na asihujumiwe. Sisi hapa tanzania wanaoheshimiwa ni wanasiasa mafisadi, madaktari, walimu, wahandisi hawaheshimiwi hata kidogo. Kwa hiyo hapa unaweza kuona kabisa kuwa mheshimiwa rais anafaya ule ule usanii, kama sio yeye basi maneno hayo amewekewa na Salva, yeye ana akili na anajua ukweli huu.
 
Kwa maoni yangu, huu ujumbe wa Rais ni kwa kina Slaa, Sitta, Kilango, Mwakyembe, Zitto, Mpendazoe na kwamba huenda anamuunga mkono Kingunge ambaye upo uwezekano pia alimtuma ama walizungumza.

Kauli kama hiyo aliwahi kuitoa Mkapa siku chache kabla ya Januari 21, 2001 na baada ya hapo kilichofuatia kisiasa tunakifahamu. Hapa anakoelekea Rais ni kubaya zaidi ila anatafuta njia. Alianza katika hotuba yake kwa kusema demokrasia lazima iwe na mipaka na sasa anasema "siasa basi tuendeshe nchi" na Mkapa alisema "siasa sasa basi, uchaguzi umekwisha tujenge nchi" ndipo maandamano yakazuiwa na hali ya kisiasa ikawa nzito akatimua zake nje (kama Kikwete aivyotimua juzi) huku nyuma mzee wa watu (Marehemu Dk. Omar) huku akipokea maagizo na maelekezo kutoka kwa Ben, akafanya Press Conf sambamba na Press Conf nyingine kama hiyo kwa serikali moja na baadaye mambo yakawa mazito.




MUNGU AEPUSHIE MBALI, lakini eweee JK na watu wako, tuepusheni na machafuko, Watanzania wamechangamka musiwachokoze, endeleeni tu kuwazuga hadi muda wenu wa kutawala uishe kwa amani.


hivi ninyi mnataka Kikwete aongee nini ili mfurahi??

aliyosema JK ndio ukweli wenyewe nchi hiyo imeharibika inatakiwa tu wakabidhiwe ma engineer wairekebishe.
 
Kwanini JK asitume wawakilishi wanaojua cha kuongea kwenye hadhira za wasomi kuliko kuongea as if yuko kijiweni?Tunahitaji as many lawyres,doctors,journalist,etc as possible just like tunavyohitaji wanataaluma ktk teknolojia.Wanaobishana kila kukicha ni wanasiasa na si wataalam wa siasa in the sense of political analysts,researchers,scientists,etc.This presidaa cant be serious kudai tukijaza wanasheria wataishia kutufunga tu....by the way watamfunga nani kama state inalinda mafisadi kwa kutowapeleka mahakamani?



Rais mzima anaongea utumbo kila kukicha. Inatia kinyaa sana kumsikiliza raisi wa nchi anaongea kienyeji kama yuko kilabuni.

Huyu ni mtu ambaye amepata exposure akiwa waziri wa mambo ya nje; kauli zake zingefananaje ikiwa hakupata nafasi hii?


.
 
Wakuu, tunapochambua wasifu wa viongozi watakaokuja, ni vyema tukawaangalia pia wake zao wakoje. I am fade up!



.
 
RAIS Jakaya Kikwete, ameonya kwamba kama nchi ikiendelea kuzalisha wanasiasa kwa wingi itaishia kwenye malumbano na migogoro isiyo na tija, badala yake amewataka Watanzania kuijenga katika misingi ya sayansi na teknolojia.

Akizungumza kwenye mkutano wa sita wa Siku ya Wahandisi nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, Rais Kikwete alisema njia pekee ya kuiletea nchi maandeleo ni kuzingatia sayansi na teknoliji badala ya siasa ambayo huishia kwenye porojo na malumbano.

Alisema umefika wakati kwa kutumia wataalam hasa wanasayansi kufanisha utendaji badala ya wanasiasa katika mambo yanatakiwa watu waliobobea kwenye fani hizo.

"Tukijaza wataalamu wa siasa tutaendele kubishana tu na tukiwajaza wanasheria tutaishia kufungana, kinachotakiwa sasa ni wataalamu wa sayansi na teknolojia, ili nchi yetu iweze kusonga mbele kimaendeleo," alisisitiza Rais.

Rais alisema pamoja na kazi nzuri ya kufundisha wahandisi inayofanywa na UDSM, bado kuna changamoto nyingi za kuboresha fani hiyo, kama vile ubora wa ufundishaji unaoweza kukidhi mahitaji ya sokoni pamoja na upatikanaji wa vitendea kazi vyote muhimu.

Alisema kazi ya uhandisi inahitaji kujiendeleza kimasomo, hivyo aliwataka wahandisi na makandarasi nchini kutotosheka na kiwango cha elimu walicho nacho badala yake watafute nafasi za kujiendeleza kimasomo.

"Heshima ya uhandisi inategemea ubora wa kazi mnayofanya, acheni mambo ya ujanja ujanja," alisonya Rais Kikwete.

Rais Kikwete alitoa wito kwa bodi hiyo kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kwa umoja ili kuondoa tofauti dhana iliyojengeka miongoni mwa watu wengi kwamba wazawa hawawezi kufanya vizuri isipokuwa wanaotoka nje ya nchi.

Alisema kama wahandisi na makandarasi wakifuata maadili ya kazi, shughuli nyingi zinazohusiana na fani hiyo zitafanyika kwa ubora unaotakiwa na kuipunguzia hasara taifa kutokana majengo kuporomoka. .

NIliposoma hii habari, nilijibu kwa kebehi Bwa ha ha ha ha. Lakini katika kujibu hoja ya mtu siku kadhaa baadaye, nikasema kuwa miaka 30 tangu kauli hii ya kuendesha nchi kisayansi itoke, tutaitafakari na kusema kuwa Kikwete alikuwa sahihi.

Naomba nijirudi kwa kuondoa kebehi hii na kuona kauli ya Kikwete kama changamoto. Ikiwezekana, MODS naomba muirudishe hii hoja kule Jukwaa la Siasa!

Mwalimu Nyerere alisema tulipopata uhuru, "wenzetu wanapaa, sisi tunatambaa, inabidi tukimbie tuwafikie" (sina nukuu kamili, lakini huu ni uelewa wangu wa alichokisema Nyerere).

Rais Kennedy wa Marekani aliposema kuwa ni muhimu kwa Marekani kufikisha mtu mwezini, alitoa changamoto ambayo katika miaka kumi, ikawa kweli. Alitoa changamoto kwa wananchi wake na wakaitikia wito Special Message to the Congress on Urgent National Needs Page 4 - John F. Kennedy Presidential Library & Museum

NImetafakari sana hii changamoto pamoja na kuwa Mkwere huwa anaweka maneno mengi na kuchanganya vitu kama upishi wa mseto, nimeamua nichambue yaliyo ya maana na niyajengee hoja.

Ni kweli hakuna ambalo Kikwete atalisema ambalo tutaliona la maana au umuhimu kwa kuwa tumejipofusha kuona lolote bora kutoka kwake kutokana na udhaifu wa Uongozi wake kuwa makini, fanisi na hasa kushughulikia Uhujumu, Uzembe na Ufisadi.

Nitapokea makonzi yenu kwa unyenyekevu kwa kutamka kuwa Kikwete ni Rais mzuri, katika nyakati mbovu na hata nchi isiyomfaa. Right President at rong country and time!

Nimesema hivi na nitaomba nitumie kilugha cha Pundit kujieleza.

Think of a CEO or Manager who has Macro Management style, always delegating and looks at reports. Most of times, this kind of Manager has a strong competent team and does not require to Micro Manage everyproject and every penny, as long as this Manager and Leader trusts the people supporting him.

Sasa hapa kuna mawili, Management na Leadership.

Kwenye Management, yeye ni Macro Manager, yule ambaye anafaa kuongoza shirika au mradi ambao tayari una ufanisi wa hali ya juu na hahitaji kuchafuka sana au kutoka jasho. Kama Leader, anaruhusu walioko chini yake kujitutumua na kuonyesha ujuzi na utaalamu wao, hivyo ni kuwa-empower wafuasi wake kwa kuwapa nafasi ya kuonyesha kazi zao na kujieleza.

Lakini pamoja na sifa hizi, Kikwete alichoshindwa kubaini ni kuwa Tanzania inahitaji Micro Manager na Close directive ya Leadership!

Hao anaowaamini kuwa watafanya kazi vizuri, kawapa madaraka makubwa sana na wanajifanyia kazi hovyo hovyo, na yeye Kikwete anafeli kuwa Kiongozi na Mtawala mzuri kwa kuendelea kung'ang'ania kuwa yeye ni Macro Manager, hivyo aachie Uhuru wa watu kujifanyia mambo.

Sasa tukiangalia kufanya kazi kwa kutumia Sayansi na Teknolojia, suala la Macro au Micro Management si la kisiasa tuu, bali ni la kutumia sayansi na teknolojia.

Naipokea changamoto ya Kikwete kwa mtazamo wa kusema ili Tanzania tuendelee, tunabidi turudia kauli ya Nyerere na Kennedy kuwa sasa hivi, siasa basi, tuendeshe nchi kwa kutumia Sayansi na Teknolojia.

Hii si kwa masuala ya Utawala na Uongozi pekee, bali ni kila kitu tunachokifanya. Iwe ni Kilimo, Ufugaji, Biashara, Viwanda, Uvuvi, Michezo, Sanaa na shughuli nyingine za uzalishaji mali.

Alichokosea Kikwete ni kuchanganya mambo ya kutaka wahitimu wengi wa Uhandisi na hata kutoa uwiano dhaifu wa wahandisi na kuachana na siasa kukimbilia Teknolojia na Sayansi.

Kauli ya kutaka nchi iendeshwe Kisayansi na Kiteknolojia ingetolewa katika mandhari tofauti na hii aliyokuwapo. Ni kweli inabidi tuachane na kuendesha nchi kwa kutumia siasa pekee na tuoanishe itikadi na sera ambazo ni siasa na matumizi ya Sayansi na Teknolojia katika kuendesha nchi, ikiwa ni pamoja na Utawala, Uongozi, Uzalishaji mali na Huduma za jamii.

Laiti kama angeanzia kujitathmini kwa kuangalia anachofanya yeye kama Kiongozi na Mtawala kwa darubini ya Sayansi na Teknolojia, angegundua kuwa Tanzania inahitaji Micro Manager na si Macro Manager!

Tanzania bado inatumia zana na hata mawazo na fikra za kiutendaji za kijima.

Leo hii wenzetu wanakaribia kuachana na Nano Technology na kwenda kwenye technology mpya,sisi bado hata Computer inatushinda.

TUnashindwa kuwa na central database ya Serikali kuweka Nyaraka au kumbukumbu. Hatuna hata vitambulisho vinavyoaminika, hatuna anuani au makazi ambayo yanaweza aminika na benki hata kupata mkopo, kila kitu ni kutafuta faili au yale ma-black book, kupata kumbukumbu. Tunatumia muda mwingi kufanya vitu kutumia analog methods huku tungeweza kuwa kwenye digital age.

Mfano, unakwenda Uhamiaji au Leseni ya Gari kubadilisha picha au kupata leseni na paspoti mpya, kama huna nakala ya pasipoti na leseni yako, ni vigumu kwa wanaotoa huduma kukusaidia. Si hivyo tu, kila kumbukumbu iko kwenye karatasi, moto ukikamata ni kilio na kusaga meno.

Sasa tafakari muda utakotumika kwenda litafuta hili faili la Rev. Kishoka pale Uhamiaji. Kama wangekuwa na Database, na kutumia Computer ningeweza wasilisha ombi la kupatiwa pasi mpya kwa kutumia internet, au kutuma fax fomu zangu na siku ya kwenda ichukua, nitokee nakitambulisho changu na fedha kulipia kama sijalipia nimalizane nao. Zaidi kama tungekuwa na mfumo wa anuanizakuaminika na hata posta kufanya kazi vizuri, wala nisingepoteza muda kwenda uhamiaji kupigishwa gumba na picha upya au kutoa chai nipate pasipoti yangu wiki nne baada ya kuwasilisha maombi. Uhamiaji wangenitumia kwa posta Pasipoti yangu na mchezo ungekweisha.

Mfano mwingine, Wastaafu wengi walioko mikoani, hawawezi kupata penshieni zao bila kufunga safari kwenda Dar kupata mafao yao. Kama NSSF, PPF au wengine wangekuwa na mfumo mzuri wa computer na Mstaafu huyu ana kitambulisho chaTaifa,angebakia kwao Malampaka pesa aendezichukua benki au atumiwe cheki yake kila mwezi!

Tuje kwenye uzalishaji mali kama kilimo, uvuvi, ufugaji na hata uchimbaji madini. Ukiondoa wazawa wachache wenye uwezo, asilimia kubwa ya Watanzainia wanatumia zana za kijima kuzalisha mali katika nyanja hizi. Ndio tunaelewa ni umasikini, lakini ni mpaka lini tuendelee kusubiri kutumia Trekta au mbegu bora kuweza kuzalisha kwakutumia Sayansi na Teknolojia hivyo tuweze jitosheleza?

Tanzania imezungukwa na maziwa makubwa matatu na mito mingi ndani ya nchi, lakini tunakabiliwa na njaa kila baada ya miaka miwili kisa hakuna mvua, je umwagiliaji uko wapi?

Hata kama leo tutasema kuwa mkulima wa Tanzania anaweza kupata mavuno mengi, je ni mbegu bora, kilimo cha kisasa au kitu gani kinatumika kumzindua Mtanzania?

Je tunashindwa nini kutumia Sayansi na Teknolojia vizuri kuhakikisha kuwa tuna umeme na nishati za kutosha? Mabwawa ya Umeme yanajaa tope, tunashindwa nini kuyasafisha na hata kutoa kinga yasipate tope? kwa nini hakuna mkazo kutoka taasisi za Sayansi au mamlaka husika kulisukuma Taifa kwenda kwenye matumizi ya Umeme wa Upepo na Jua?

Sasa pamoja na kuwa kauli ya Kikwete inaelekea kumsuta nikitumia vigezo nilivyoweka hapo juu, lakini si dhani ni haki tukimbebesha mzigo huu yeye pekee bila sisi wote kuubeba mzigo huo.

Nakubaliana naye kuwa tatizo la Tanzania kuendelea ni siasa nyingi. Wanasema Wamarekani "too many chiefs and not enough Indians"! Ndilo tatizo la Tanzania, kila kitu ni siasa nyingi ambazu huua ufanisi na tija kwa kuwa kila mtu mtazamo wake ni wa kisiasa na si kisayansi au teknolojia.

Mitazamo ya kisiasa na hata kufanya mambo kwa kuegemea siasa kumetufanya tupoteze muda mwingi katika safari yetu ya kusukuma gurudumu la maendeleo na ujenzi wa Taifa.

Mfano mwingine mzuri wa porojo za siasa ni ile website ya Ikulu. badala ya kufanya mambo kwa kutumia Sayansi ambayo anaihubiri, wasaidizi wake wamekaa wakivutana kisiasa na kubishana ni nini kitokee, ni rangi gani itumike!

Nakubali kuna mengi ambayo yangefanikiwa kama tungekuwa na Uongozi mahiri na makini na hilo Kikwete ni wa kulaumiwa, lakini tusipuuzie changamoto hii.

Tutumie fursa hii kuleta maendeleo kwa kumtaka Kikwete afanye kweli kama Kennedy alivyofanya kuwa kusema tunahitaji kujifunga mikanda na kuingia gharama kama tunataka kwenda mwezini (soma hiyo link hapo juu).

Tunachotakiwa kumuasa na kumuomba Kikwete ni kuwa inabidi awe Micro Manager na awe mkali sana na si mkali kidogo kama Mwinyi alivyoombwa na Nyerere!
 
Back
Top Bottom