Rais Kikwete aongea na Wazee wa Dar: Adai pesa za Escrow ni za IPTL. Uteuzi wa Tibaijuka watenguliwa

Usilete maneno ya mkoloni mwingereza na vi-debit na vi-credit vyenu hizo hela si za Tanesco zingetafuta nini kwenye vitabu vya Tanesco wakati si zake.

Kweli wewe ni kilaza ya lumumbu.. Hiyo pesa si imelipwa na Tanesco sasa itakusekanaje kuwa kwenye vitabu vya tanesco??
 
Kesho ningekuwa mwandishi wa habari kwenye gazeti ningeweka heading TANZANIA YAPOTEZA MWELEKEO KWA SASA HAINA RAIS YABAKI YATIMA.
 
Anajichanganya sana unajua unapojitahidi kutetea uongo ni lazima uwe na kumbukumbu. Tutaonana Oktoba 2015. Chadema Na Ukawa msilale watanzania yupo pamoja Na nyinyi kuwatoa wezi hawa.
 
Huyu mzee hatumuelewi hata huyo jamaa aliyekaa hapo nyuma yake anasinzia mbaya na kama sijakose ni Usalama wa Taifa!!!
 
Baaaasi watanzania tu mbumbumbu sana...
Kwann uongee na wazee mambo mazito hivi? Kwann usituite wanazuoni? Aaaa rais umeniangusha mno

ukitaka kuaminisha watu huwezi kuongea na wazee wasio na changamoto . ongea na vijana pia wataalam angeumbuliwa
 
Yaliyoongelewa na mheshimiwa JK leo yalitazamiwa.
Kimsingi wale waliokuwa wakituhumiwa , wamesafishwa mchana kweupe pepe!!

Sasa miye najiuliza kwa mtaji wa watuhumiwa wengine kubeba bulungutu kwa maboksi,rambo, lumbesa na visulfeti, wafadhili watarudisha misaada waliyokata?

Sijui kama hili limejibiwa.
 
ndio maana kachagua wazee maana hawajarifuatilia sana ilo swala la escrow bado anababaika, wangekua vijana sijui kama angeweza kuliongelea kabisa au angeongea uku anafumba macho

mpaka unastukiwa na wacheza bao basi ujue umechemsha vibaya mno !
 
Kwa wa-TZ mnaosubiria JK aseme tofauti, pole za dhati, kwani huyu bwana anajua kinachoendelea na hakisemeki, kutokana na uhusika wake.

Tanzania kuna makampuni mangapi?mbona kila kampuni haigawi fedha kama chizi kwa mafisa wa ikulu na viongozi waandamizi wa serikali, pamoja na wadini, kwa siri?
 
Walikwepa kulipa kodi? Hakuna adhabu kwa mkwepa kodi? Au hilo nalo halikuwa na umuhimu wa kuongelewa? Hapa Nasubiri mwisho tu wa hotuba hii, ila msimamo wa mkuu wa kaya unatoa dalili za kwamba 'Muhongo na Tibaijuka kama wangejiuzulu angewashangaa!'
Ova

Amesema wamekubali kulipa kodi...kwa hio hakuna shida watalipa kodi
 
Mada ya leo itawafanya wazee wasiudhurie tene mkutano wa mkuu. Mtoa mada anafikia point anakiri kwamba mada hii inachanganyanya. Ukiangalia wazee ni usingizi na miayo tu anaendelea. Kungekuwa na paper mwishoni ingekuwa vizuri zaidi kupima kama wameelewa. Ila ninachokiana hapa sitegemea kipya toka kwa mkuu.
 
Naunga mkono.
UKAWA waongee na vijana ili vijana wawe tayari kurithi taifa hili toka CCM inayojiandaa kustaafu mwaka 2015 na wazee wake wastaafu.
 
Back
Top Bottom