baharia Ar
JF-Expert Member
- Dec 1, 2013
- 837
- 314
Wakuu nashindwa kuelewa nini mantiki ya rais wangu kuto kulivunja baraza la mawaziri, tunamaliza wiki sasa tangu kampen ianze mawaziri wanatumia nafasi za uwaziri wao kuomba ubunge na wengine wanatumia uwaziri wao kuombea u rais. Na bunge halijavunjwa mpaka sasa licha ya ahadi Kuwa litavunjwa tarehe 20/8/2015 lakin mpaka sasa wabunge wanautumia ubunge wao kuusaka ubunge hivi nchi hii ninani katurogaaa
1) Muda wa kushika madaraka ya Waziri na Naibu waziri utaanza tarehe atakapoteuliwa kushika madaraka hayo.
(2) Kiti cha waziri au Naibu Waziri kitakuwa wazi litokeapo lo lote kati ya mambo yafuatayo:-
(a) Endapo mwenye madaraka atajiuzulu au kufariki dunia;
(b) Ikiwa mwenye madaraka hayo atakoma kuwa Mbunge kwa sababu yoyote isiyohusika na kuvunjwa kwa Bunge;
(c) Ikiwa Rais atafuta uteuzi na kumuondoa kazini mwenye madaraka hayo;
(d) Iwapo atachaguliwa kuwa Spika;
(e) Iwapo Waziri Mkuu atajiuzulu au kiti chake kikiwa wazi kwa sababu nyingine yoyote;
(f) Ukiwadia wakati wa Rais mteule kushika madaraka ya rais basi mara tu kabla rais mteule hajashika madaraka hayo;
(g) Iwapo Baraza la Maadili linatoa uamuzi unaothibitisha kwamba amevunja Sheria ya maadili ya viongozi wa Umma.