Rais Kikwete amteua George Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Hii sio sahihi kabisa. Huyu mtu alikuwa mtu wa karibu kabisa na yule aliyeboronga. Je kama alishirikiana nae kufikia maamuzi au pengine alipata kumshauri bosi wake kufikia uamuzi mbovu, si ni wote wale wale tu. Hii sio sahihi kabisa.
 
Hongera Mheshimiwa Masaju.

Umekabidhiwa kiti cha moto, Mungu akupe busara ulitumikie taifa lako
 
huyo wa katikati

Naibu+Mwanasheria+Mkuu+wa+Serikali%252CBw+George+Masaju%2528katikati%2529+Mkurugenzi+wa+Mipango%2528Kushoto%2529+na+Mkurugenzi+wa+Rasilimali+watu+m.jpg
 
Wale wadini wenzangu karibuni hapa tumseme kikwete kwa UDINI wake;
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana George Mcheche Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Uteuzi wa Bwana Masaju ulianza jana, Ijumaa, Januari 2, 2015 na ataapishwa keshokutwa, Jumatatu, Januari 5, 2015, Ikulu, Dar Es Salaam. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Masaju alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Bwana Masaju pia amepata kuwa Mshauri wa Sheria wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Ataweza kumtia kitanzini bosi wake wa zamani ikiwa sakata la escrow litaelekezwa huko?
 
Hii sio sahihi kabisa. Huyu mtu alikuwa mtu wa karibu kabisa na yule aliyeboronga. Je kama alishirikiana nae kufikia maamuzi au pengine alipata kumshauri bosi wake kufikia uamuzi mbovu, si ni wote wale wale tu. Hii sio sahihi kabisa.
Mkuu kwan kateuliwa na nani na msimamo wa huyo mteuzi juu ya escrow ukoje?Je unadhani anaweza kuteua mtu mwenye msimamo tofauti na yeye?
 
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana George Mcheche Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Uteuzi wa Bwana Masaju ulianza jana, Ijumaa, Januari 2, 2015 na ataapishwa keshokutwa, Jumatatu, Januari 5, 2015, Ikulu, Dar Es Salaam. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Masaju alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Bwana Masaju pia amepata kuwa Mshauri wa Sheria wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

naamini H.E. Prof.Dr. JK alikuwa anaufanyia kazi ushauri huo kwa umahiri mkubwa, bila kusahau '.....za mbayuwayu .....changanya na za kwako'
 
Kama alikuwa naibu wa Tumbili basi huyu atakuwa ngedere, wote tabia zao moja, hawalimi, kazi yao ni wizi tu!
 
Back
Top Bottom