Rais Kikwete akiwa ziarani mkoani Mwanza pamoja na Wabunge wa CHADEMA

Kikwete ni raisi wa mfano katika taifa hili kuwahi kutokea. Ni mtu anaewasikiliza watanzania wanataka nini na kuact accordingly.
 
Acha wivu wa kike wewe, kwani mara ngapi tunawashuhudia mawaziri na wabunge wa ccm wanavaa mavazi ya kichama katika shughuli za kiserikali? ni mara ngapi wakuu wa mikoa na wilaya wanatumia rasilimali za serikali katika mikutano ya ccm kwakuwa tu yupo Kinana, Nape au Kikwete katika shughuli za kiccm?

Wenje amevaa t shirt safi kabisa ya M4C ambayo imempendeza na kwahakika hajafanya kosa lolte ama kumkwaza mtu yeyote kwa mavazi yake. Hata alipopewa nafasi na Raisi Kikwete kusalimia wananchi alifanya hivyo kwa salamu ya Chadema na uwanja mzima ukazizima. Hatahivyo hapo ni uwanja wake wa nyumbani na Chadema ndio habari ya mujini.
Mkuu Mwita Maranya , Nianze kwa kuuliza, kama huu niliofanya ni wivu wa kike, Je, upi ndiyo wivu wa kiume, kama hakuna wivu wa kiume, huoni maneno yako yana mtazamo wa dharau and victimization kwa wanawake.

Sijui unachoongea hapa nini na point yako inasimama wapi kwenye siasa zinazohubiriwa kila siku na CHADEMA ndani na nje kwenye majukwaa ya siasa.

Kwa hiyo unataka kusema CHADEMA wanafanya na wataendelea kufanya kama wanavyofanya CCM. Sasa tofauti ya CHADEMA na viongozi wake iko wapi kama na wao wanafanya kama CCM wanavyofanya?. Kwa maelezo yako haya, unamaanisha kuwa hata CHADEMA ikiingia madarakani itaendelea kufanya kama CCM wanavyofanya!. Kauli yako niya kushangaza na hasa ikichukuliwa kuwa na wewe ni mmoja wa watu wanao quest for something in CHADEMA come 2014 and 2015.

Wananchi wenye mitazamo na fikra pana wanataka siasa na utendaji kutoka vyama vya upinzani ambao ni tofauti na CCM ili wapate choices katika maamuzi kwenye sanduku la kura. Huwezi kuwa wale wale ukategemea wananchi wakuchague kwa utofauti wako wakati kiuhalisia haupo.

Huwezi pia kama chama kinachopenda na kinataka kupewa nchi kwa kutegemea kura kutoka kwa wananchi ziwe kama bahati nasibu kwa sababu wananchi wamekosa tofauti yoyote kimtazamo na kiutendaji kati ya CCM na CHADEMA.

Badilisheni mitazamo na utendaji.
 
>Leo kwenye uzinduzi wa maji kule kwimba wakijaa watoto! Ni kutokana na kutokuwepo kwa wabunge wa CHADEMA!!
 
Hii ni sawa kabisa, unapokuwa rais ni rais wa watanzania sio rais wa chama.
Huu ni ukomavu wa kisiasa wa rais Kikwete.
Nadhani alifanya kazi kubwa sana kuwashawishi watu wa usalama wasiwafukuze viongozi wa vyama vya upinzani ndani ya protokali.
Nawaomba viongozi wengine wa CCM Na Wa usalama waige hili Na wajue kuwa chama cha upinzani si Uhaini!
 
Rais Kikwete alishasoma alama za nyakati. Kwa sasa ametulia. Vazi la Wenje ni la kawaida tu! Hapakuwa na mavazi maalum! Kwa akili za Ndugai hata huu mfano alioonyesha Bosi wake atashindwa kujifunza chochote! Big up Prezda!
 
Kweli masisiem hamuoni masabur..i yenu,antonia dialo na likofia lake kama anaokota chupa za uhai huoni,soseji pita muongo na t shirt yake ya magamba ndani ya koti nayo hujaona?acheni unaa nyie magamba!!!
mkuu kijome :yield: Hahaha hahaha hahaha maccm aka magamba huwaza kwa kutumia masabur
 
kama si chadema jk asingepata hao watu.

Kwani aliwaandikia barua kuwaomba wahudhurie? wamejipendekeza wenyewe kwa kuwa wanajua hawatarudi mwanza tena ndio Omega yao 2015, hao wabunge wawili walifanya maandamano juzi watu waliohudhuria ni wapiga debe, vijana wakiume na wanywa viroba, wakaishia kupigwa mabomu
Hakuna wanawake au wazee waliohudhuria kama unavyojionea kwa macho kwa ziara hii ya Rais wetu ambaye kwasasa mumemtambua kuwa ndie aliyewashinda 2010 na mkajifanya kujifaragua kutafuta huruma ya wananchi mwisho baba zako akina slaa wakaishia kwenda kuomba chai Ikulu, Aibu hii ndio Omega yenu.
 
Kwani aliwaandikia barua kuwaomba wahudhurie? wamejipendekeza wenyewe kwa kuwa wanajua hawatarudi mwanza tena ndio Omega yao 2015, hao wabunge wawili walifanya maandamano juzi watu waliohudhuria ni wapiga debe, vijana wakiume na wanywa viroba, wakaishia kupigwa mabomu
Hakuna wanawake au wazee waliohudhuria kama unavyojionea kwa macho kwa ziara hii ya Rais wetu ambaye kwasasa mumemtambua kuwa ndie aliyewashinda 2010 na mkajifanya kujifaragua kutafuta huruma ya wananchi mwisho baba zako akina slaa wakaishia kwenda kuomba chai Ikulu, Aibu hii ndio Omega yenu.
2015 sio mbali,tutaujua ukweli!kama umeandika ukweli au propaganda tutajua!
 
Umekuwa Mtetezi mkubwa sana wa JK pale anapofanya vizuri na hata apofanya vibaya
mfano kuweka mchagoni majina ya wauza sembe bila Shaka likiwemo na jina lako. Hebu tuambie wewe na JK mkoje?
mbali na hili la Kuwa Rais wa watanzania wote.

usipate tabu na huyo ritz mkuu,hana uhusiano wowote na jk,ni mdini flani na mmatumbi wa kilwa anayemkubali sana dr.slaa ila kimoyomoyo.
 
Siku zote siasa zingekuwa za upendo namna hii nchi ingepiga hatua za kimaendeleo kwa haraka sana.
 
Rais Kikwete, ni rais wa wote wenye vyama na wasiyo na vyama, waliomchagua na wale ambao hawakumchagua.

Anafanya hivi kwenye majimbo yote ambayo kuna wabunge wa upinzani aangalii Chadema, CUF, NCCR Mageuzi wala CCM.

Sijui umeipata wapi hiyo kuwa JK kaamua kuwashirikisha Chadema.
ukifanya ziara ya kiserikali kanda ya ziwa ukawabagua CDM kwa namna yoyote ile basi ziara hiyo lazima ikudodee - JK ni mjanja ndiyo maana kaagiza wabunge wa CDM wawepo.
 
Kikwete ni raisi wa mfano katika taifa hili kuwahi kutokea. Ni mtu anaewasikiliza watanzania wanataka nini na kuact accordingly.

Duh kazi kweli hiyo ni kazi yake wala haitaji kupewa sifa huu ni uchiz
 
mkuu kijome :yield: Hahaha hahaha hahaha maccm aka magamba huwaza kwa kutumia masabur
Ndipo akili zao zilipohamia mkuu concord nh hata nepi anajua zipo kwenye masabur ,karume akaua zaidi eti wana akili za kambale hahahaaaa
1234550_418893724881859_1383862369_n.jpg

cc Ritz , ZeMarcopolo , Simiyu yetu , MwanaDiwani
 
Huu ni ukomavu kisiasa na pia ni taswira nzuri kwa Taifa.

Siasa za vyama vingi siyo ugonvi bali ni njia mojawapo inayotumika kuharakisha na kusukuma maendeleo mbele zaidi katika nchi.

Nimelipenda vazi la mbunge Kiwia ambalo haliwagawi wananchi katika hafla hiyo kwa misingi ya kiitikadi na mitazamo kwa sababu halina alama au nembo yoyote inayomtambulisha kama ni tofauti na baadhi ya wananchi na viongozi wengine. Mh. Kiwia yuko kitaifa zaidi kama ilivyo kwa Rais Kikwete na hasa ukichukulia kuwa Mwanza ni epic centre ya mapambano ya kisiasa kati ya CCM na CHADEMA kwa kanda ya ziwa.

Mbunge Wenje anatakiwa afahamu ni wapi anatakiwa kuvaa mavazi aliyovaa na wapi hapaswi kuvaa. Lazima ajitambulishe kama ni mbunge wa wananchi wote kwenye hafla ya kitaifa na siyo mbunge wa CHADEMA.

Big up Mh. Kiwia kwa kuliona hilo.

Mbona Kiwia naye amevaa gwanda? Mimi sioni tatizo kwa Wenje kwa hilo la kuhusu alichovaa, labda ni hivi tulivyozoea kukosoa kila jambo, hivyo kuwa tunasaka cha kukosoa kwa udi na uvumba.
 
Back
Top Bottom