Rais Kikwete aanza ziara ya kidola Afrika Kusini; Ni ziara ya kwanza ya kidola kufanya na Rais wa TZ

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Na Rachel Balama

RAIS Jakaya Kikwete, jana ameanza ziara ya kidola siku nne nchini Afrika Kusini ambayo ni ya kwanza kufanywa na Rais wa Tanzania nchini humo.Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, inasema ziara hiyo ya kihistoria imetokana na mwaliko wa Rais Jacob Zuma wa nchi hiyo ambaye utawala wake umekuwa na uhusiano mzuri na Tanzania tangu aliposhika madaraka ya kuongoza Taifa hilo.

Rais Kikwete ambaye ameongozana na ujumbe wake akiwemo mkewe Mama Salma, waliondoka nchini jana mchana kwenda nchini humo katika Jiji la Pretoria.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, pamoja na marais waliotangulia nchini Tanzania, waliwahi kutembelea nchini humo kwa shughuli mbalimbali lakini hakuna Rais wa Tanzania ambaye aliwahi kualikwa kwa ziara rasmi ya kiserikali au ya kidola tangu nchi hiyo iingie katika mfumo wa demokrasia mwaka 1994.

Rais Kikwete pia atafanya mazungumzo ya kiserikali Rais Zuma, kutiliana saini mikataba ya makubaliano katika nyanja mbalimbali, kufanya mkutano na waandishi wa habari na kutembelea Uwanja wa Uhuru akiwa na mwenyeji wake.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa, viongozi hao pia watakula chakula cha mchana na wafanyabiashara wa Tanzania, Afrika Kusini na kufanya mazungumzo ya pamoja ili kuimarisha uhusiano wa kibiashara na kiuchumi kati ya nchi hizo.

Rais Zuma ataandaa dhima ya kitaifa kwa ajili ya Rais Kikwete na ujumbe wake kwatika nyumba ya wageni nchini humo.

Julai 20 mwaka huu, Rais Kikwete na ujumbe wake watakwenda Cape Town nchini humo ambapo watatembelea kisiwa cha wapigania uhuru wa Afrika Kusini ambao walifungwa kwa miaka mingi na Makaburu akiwemo Rais mstaafu Bw. Nelson Mandela kinachoitwa Robben.

Rais Kikwete na ujumbe wake, watarejea nchini Julai 21 mwaka huu
 
So trip zote alizokwenda SA ni sio za kidola ina maana waziri angeweza kuiwakilisha Nchi

Hii ni Ziara kweli anatakiwa kwenda SA laikini ukicheki Boarding Pass yake amekwenda South African mara 5 toka Jan 2011 Utamu huo wa Urais...
 
nyambaaffffff...!!!!! Halafu waache uwongo....Afrika Kusini imekuwa na uhusiano mzuri na Tizii toka walipopata majority rule na siyo toka utawala wa Vasco da Gama II...waache sifa za kijinga....halafu eti ziara ya kidola...hivi wanatufanya sisi mabweeeegeeee sana!
 
Aende tuu manake awalete makaburu wengi waje kukamua Tanzanite dhahabu uranium makaa ya mawe hongere Mh Jakaya kwa kuuza nchi yetu kwa makaburu
 
Sijui anaenda kuuza kipande gani tena yarabi! Term iliyopita tuliona trips za Marekani matekeo yake Uranium imekwenda in exchange for mosquito nets! Sasa Zuma in not your average shower-gel user, atapiga deal ya nguvu. Tusubiri makaburu weusi! Wa-south wanajuwa tunalainika tukiona weusi wenzetu lakini ukweli hawana tofauti sana na weupe, angalieni kule Merereni kama kuna tofauti wakati CEO akiwa mzungu na wakati walipoleta mweusi. Neglible difference!
 
So trip zote alizokwenda SA ni sio za kidola ina maana waziri angeweza kuiwakilisha Nchi

Hii ni Ziara kweli anatakiwa kwenda SA laikini ukicheki Boarding Pass yake amekwenda South African mara 5 toka Jan 2011 Utamu huo wa Urais...

zuma na kikwete ni watu wa Gadaffi kuna kitu wanapika kwa visingizio kibao
wanafanana kwa mengi hata chamani wako sawa
 
tunaibiwa sana na waafrika kusini kupitia makampuni yao ya kikaburu
sito shangaa kuona leo ZUMA anajifanya kusema kikwete kaongeza ushirikiano mzuri wakati tulishiriki kuwakomboa
na DAKAWA je?
dirty politics za kikwete bana sasa na ili ni sifa?
 
Back
Top Bottom