Rais Joe Biden kuchunguzwa baada ya kukutwa na Nyaraka za Siri Nyumbani kwake

GREAT INVESTOR

Senior Member
Nov 13, 2018
128
295
Tutafika lini walipo wenzetu.

Kwema wa kuu, Niko nimetulia kazini nafuatilia habari.Kwa wafuatiluaji wa habari za kimataifa watakumbuka siku si nyingi, Rais aliemaliza muda wake Donald Trump alivamiwa katika hoteli yake ya kifahari zilipo ofisi zake binafsi na FBI.

FBI walivamia izo ofisi baada ya kupata taarifa kuwa jamaa aliondoka na documents ambazo hakupaswa kuzichukua kutoka white house (CLASSIFIED DOCUMENTS) na walipofanya uchunguzi walibaini kua jamaa alikua nazo.

Mchezo umegeuka kwa rais wa sasa Biden ambae nae kakutwa na izo documents nyumbani kwake, mbaya zaidi yeye zimekutwa garage kwake(sehemu ya kupaki magari yake) waliozikuta ni ofisi/ Maktaba ya taifa ya kutunza nyaraka au kumbukumbu, FBI walitumwa kuhakikisha zinachukuliwa kwa usalama bila kuvuja.

Punde mwanasheria mkuu (AG) ametoka kufanya press hapa na waandishi wa habari na ameunda tume ya kumfanyia uchunguzi Biden.

Kwa upande wa Biden akiulizwa maswali hana majibu ya kueleweka sana sana anasema aliondoka na izo CLASSIFIED DOCUMENTS wakati akiwa makamu wa rais msimu Obama akiwa Rais.

Siasa za hawa jamaa ni za uwazi na uwajibikaji kwa makosa utakayo yafanya.

Je, ni lini sisi kama Nchi tutafika hatua hii.

------

Mwanasheria mkuu wa serikali nchini Marekani Merrick Garland amemteua mchunguzi maalumu Robert Hur kuchunguza tukio la kupatikana kwa nyaraka za siri katika makazi ya rais Joe Biden yaliyoko Wilmington, Delaware.

Aidha mchunguzi huyoi atachunguza tukio la awali la kukutwa kwa nyaraka kama hizo za siri katika ofisi ya rais Joe Biden isiyokuwa na ulinzi iliyoko mjini Washington. Nyaraka hizo zinasadikika zilikuwepo kwenye ofisi hiyo tangu Biden alipokuwa makamu wa rais.

Katika tukio la kwanza, nyaraka hizo za siri zilipatikana wiki moja kabla ya uchaguzi wa katikati ya muhula wa mwaka uliopita, ambalo liliripotiwa na ikulu ya White House Jumatatu hii, hatua iliyoibua shutuma kutoka chama cha Republican, wakihoji sababu za kufichwa kwa taarifa hizo.

Kwenye ufichuzi huu wa karibuni, nyaraka hizo zimepatikana kwenye gereji ya nyumbani kwa Biden mjini Wilmington, Delaware, ambako mara nyingi huwa anakwenda kupumzika mwishoni mwa wiki, hii ikiwa ni kulingana na ikulu ya White House.

Mwanasheria huyo mkuu Garland amemteua Hur ambaye atachunguza iwapo kuwapo kwa nyaraka hizo kwenye makazi binafsi kunaweza kuwa kumekiuka utaratibu wowote wa kisheria. Garland anayeongoza wizara ya sheria, amesema anaamini kwa dhati kwamba mchakato huo wa kawaida unaoendeshwa na wizara yake utaifanya kazi hiyo kwa uadilifu.
 
Hiyo tume haijaundwa na Russia wala China au UN.
Nakukumbusha mada ina zungumzia U.S.A sio Russia, China wala UN.
Imeundwa na mifumo imara ya the US.
Mifumo imara ni nini ? Na hiyo mifumo imara kwa US ni ipi ?
Jengeni mifumo imara badala ya kujenga wendawazimu ambao kesho na keshokutwa wanaweza kuibadilisha nchi na watu wake kuwa their subjects.
Hiyo mifumo imara ina jengwaje ? Na nini kinacho ongoza hio mifumo imara ?
 
Screenshot_20230112-234113.png
 
Mwanasheria mkuu wa serikali nchini Marekani Merrick Garland amemteua mchunguzi maalumu Robert Hur kuchunguza tukio la kupatikana kwa nyaraka za siri katika makazi ya rais Joe Biden yaliyoko Wilmington, Delaware.

Aidha mchunguzi huyoi atachunguza tukio la awali la kukutwa kwa nyaraka kama hizo za siri katika ofisi ya rais Joe Biden isiyokuwa na ulinzi iliyoko mjini Washington. Nyaraka hizo zinasadikika zilikuwepo kwenye ofisi hiyo tangu Biden alipokuwa makamu wa rais.

Katika tukio la kwanza, nyaraka hizo za siri zilipatikana wiki moja kabla ya uchaguzi wa katikati ya muhula wa mwaka uliopita, ambalo liliripotiwa na ikulu ya White House Jumatatu hii, hatua iliyoibua shutuma kutoka chama cha Republican, wakihoji sababu za kufichwa kwa taarifa hizo.

Kwenye ufichuzi huu wa karibuni, nyaraka hizo zimepatikana kwenye gereji ya nyumbani kwa Biden mjini Wilmington, Delaware, ambako mara nyingi huwa anakwenda kupumzika mwishoni mwa wiki, hii ikiwa ni kulingana na ikulu ya White House.

Mwanasheria huyo mkuu Garland amemteua Hur ambaye atachunguza iwapo kuwapo kwa nyaraka hizo kwenye makazi binafsi kunaweza kuwa kumekiuka utaratibu wowote wa kisheria. Garland anayeongoza wizara ya sheria, amesema anaamini kwa dhati kwamba mchakato huo wa kawaida unaoendeshwa na wizara yake utaifanya kazi hiyo kwa uadilifu.
 
Ingekuwa ajamhuri ya watu wadanganyika chawa wangesema aachie madaraka kwa kwenda kinyume na baba au angepotea au angepata kesi moja matata.
 
Checks and balances ni muhimu ukiamua kuchagua demokrasia ama uamue kabisa hatwendi na demokrasia kuliko kuwa hujulikani upo upande upi
Ones gotta pick a side or die in the middle, bongo ni kama China tu, ubeberu kidogo, ujamaa kidogo, ubepari kidogo, unyang’au kidogo, no wonder we always landing in the midst of nowhere…
 
Back
Top Bottom