Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,162
Kwa kweli huwa najiuliza, lakini nakosa majibu, hivi inakuwaje Kwa Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan, aingie na walinzi wake na huku akichukua hadi kiti chake Cha Ikulu, ili akalie kwenye nyumba za ibada, Huku akilindwa na walinzi wake zaidi ya wawili?
Hivi hatuoni kuwa hatuishi na maneno tunayojidai nayo kuwa hii nchi ni kisiwa Cha amani?
Huu ulinzi wa viongozi wetu nauchukulia kama viongozi wetu, wanachukulia kama nchi yetu ipo vitani!
Nimeshuhudia Jana katika tukio la kusimikwa Kwa Askofu Malasusa, kuwa Mkuu wa KKKT, katika ibada iliyofanyika katika kanisa la Azania Front
Binadamu wote tunaamini kuwa, kwenye nyumba za ibada, wanaingia watu watakatifu na wenye kumwamini na kumhofia Mungu wetu
Katika maandiko kwenye vitabu vyetu vya dini, inaandikwa kuwa hairuhusiwi Kwa binadamu kupanga njama yoyote ya kumdhuru binadamu mwenzake na tukiamini pia wale waumini wa dini hizo, wanaokwenda makanisani na misikitini, ndiyo wanaopaswa kuyafuata Kwa umakini mkubwa wa maandiko hayo.
Ukitafakari Kwa makini, huu "woga" wa kutowaamini wananchi wake, upo katika nchi yetu pekee!
Katika nchi za wenzetu, unaweza kumkuta kiongozi kama Rais wa nchi, anajichanganya na wananchi wake, bila ya kulindwa na ulinzi wowote!
Najiuliza, hivi Hawa viongozi wetu, mbona Wana hofu kubwa na wananchi wake hadi "wajirundikie" na msururu wa walinzi?
Hivi Hawa watawala wetu, hawaoni kuwa "kuwarundika" walinzi kibao, ili wawalinde ni kuwaongezea gharama wananchi wao, Kwa kuwa hizo gharama za walinzi wanaowalinda, ni mzigo mkubwa Kwa wananchi wanaokamuliwa Kodi wa nchi hii??