Rais hakosei?

lutemi

JF-Expert Member
Dec 24, 2013
1,743
1,379
Naomba kuuliza katika utawala je Rais huwa HAKOSEI?

Je, Rais anaweza kuwa na ushawishi wowote wenye nguvu kuingiza nchi kwenye mikataba isiyo na tija Kwa nchi?

Je, Rais anaweza kuamua Jambo lolote kwenye mihimili mingine na asifanywe chochote?

Je, Rais anaweza kuisigina katiba na chama chake kisimsimamie?

Naomba kuuliza tu je Rais anaweza kukosea katika utawala wake?

Nini Kazi ya washauri?

Nini Kazi ya katiba?

Nini Kazi ya mihimili mingine Kwa Rais.

Je, neno la Rais ni SHERIA?

Nawasilisha.
 
Huu Ujinga wa Kiongozi/Mkubwa wako hakosei.

Ni utamaduni wa kishenzi Kwa nchi za Afrika ,hasa Tanzania.

Angalia hata kwenye mazingira yetu ya kazi... BOSS hataki kukosolewa Wala kurekebishwa yaan yeye anajiona Yuko sahihi muda wote.

Ni Ujinga !!.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Kwa katiba yetu rais ni Mungu anayetembea (Mungu mtu). Hakosei na hata akikosea hahojiwi wala kushitakiwa na chombo chochote

Anaweza kuamuru eneo lote la Kanda ya ziwa wauziwe Rwanda ama Burundi.........na asifanywe kitu.

Anaweza kuamuru wapinzani wote auawe .....na asifanywe kitu.

Anaweza kuamuru wanaccm wote wanaopinga wauawe ....na asifanywe kitu.

Anaweza kuuza bandari zetu kwa waarabu na asifanywe kitu
 
Kwa katiba yetu rais ni Mungu anayetembea (Mungu mtu). Hakosei na hata alikosea hahojiwi wala kushitakiwa na chombo chochote

Anaweza kuamuru eneo lote la Kanda ya ziwa wauziwe Rwanda ama Burundi.........na asifanywe kitu.

Anaweza kuamuru wapinzani wote auawe .....na asifanywe kitu.

Anaweza kuamuru wanaccm wote wanaopinga wauawe ....na asifanywe kitu.

Anaweza kuuza bandari zetu kwa waarabu na asifanywe kitu
Nimeogopa Sana. Hii ni hatari Sana
Hivi hakuna kiongozi yeyote au vyombo vya ulinzi na usalama wanao weza kuitazama nchi na kusimamia Kwa mashauri mazuri?
 
vyombo vya ulinzi na usalama wanao weza kuitazama nchi na kusimamia Kwa mashauri mazuri?
Vyombo vya ulinzi na usalama vipo Niger, Mali, Senegal na Burkina Faso. Hapa kwetu tuna wanachama wa ccm wanaovaa magwanda ya kijeshi huku wakivizia teuzi wanapostaafu.
 
Watawala wengi wa kiafrika niwa wapumbavu wakubwa.Hulewa madaraka kama wanywa mvinjo,hufanya nchi kama mali Yao binafsi.
 
Back
Top Bottom