Rais amespend karibu miaka 3 ya kipindi chake akiwa nje ya nchi, hii imekaaje?

Bundewe

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
400
141
Takwimu zinaonesha kwamba Rais wetu ameshafanya safari 322 katika kipindi cha miaka 6 ya utawala wake. Hii ni wastani wa Safari 53.6 kwa mwaka. endapo tutachukulia wastani wa kuspend siku 3 tu kwa kila safari moja, kiongozi wetu atakua ameishi nje ya nchi yake kwa kipindi cha jumla ya siku 966 tangu aingie madarakani. Huu ni wastani tu ingawa natambua kwamba zipo safari ambayo amespend zaidi ya wiki nzima hasa zile za Marekani na Ulaya. Kipindi cha siku 966 ni sawa na miaka 2 na kama miezi nane hivi kipindi ambacho kinakaribia nusu ya kipindi chake alichokwishakaa madarakani.

Endapo kila safari moja ambayo huambatana na ujumbe mzito, itagharimu Tshs. 300,000,000/- Mpaka sasa tayari kiasi cha Tshs. 98.8 Bilioni zimekwishatumika kugharamia safari hizo.

Endapo gharama za ujenzi wa barabara kiwango cha lami ni wastani wa Tshs. 700,000,000/- kwa kilomita, fedha hizo zingejenga kilomita 141 za lami, Hivyo kwa mfano barabara ya Nzega - Tabora (Km 116) ingekamilika kiwango cha lami na chenji ingebaki, nk. Endapo gharama za kujenga chumba kimoja cha darasa ni Tshs. 12,000,000/-, fedha hizi zingetosha kujenga vyumba 8233 vya madarasa, nakadhalika.

Sina maana kwamba Rais asisafiri, isipokuwa angeweza kupunguza safari hizo, hali ya kifedha ya serikali ingeboreka bila shaka. Hatuoni wimbi la viongozi wenzie wakitutembelea kwa kasi ambayo yeye anawatembelea. Vilevile ujumbe anaoambatana nao ni mzigo mkubwa kwa Taifa. Jambo hili limepigiwa kelele mara nyingi lakini tunaambiwa kwamba Rais anakwenda kuhemea, mpaka sasa hatujaambiwa ni kiasi gani kimepatikana kutokana na kuhemea kwake badala yake tunaona Serikali ikizidi kudhoofika kifedha kiasi cha kushindwa hata kulipa mishahara kwa watumishi wake.

Nawasilisha.
 
Mfano mdogo amekwenda uingereza mara ngapi na waziri mkuu wa uingereza ametua hapa kwetu mara ngapi?

Hapo ndo utajua kuwa rais wetu anapenda sana sifa za wakubwa kwenda kwao
 
Hebu soma hapo takwimu sahihi za hapahapa jf

https://www.jamiiforums.com/search.php?do=getnew
 
Mfano mdogo amekwenda uingereza mara ngapi na waziri mkuu wa uingereza ametua hapa kwetu mara ngapi?

Hapo ndo utajua kuwa rais wetu anapenda sana sifa za wakubwa kwenda kwao

jamaa lazima mkumbuke ni lazima asafiri mara kwa mara ili akabadili blad, si unajua ana mambo yetu yale!
 
kwa hiyo ni nusu ya muda wake tangu aingie ofisini!?

Lakini naona anaanza kuelewa kuwa knowledge yake ya mambo yanayoendelea hapa nyumbani sio kubwa kutokana na kukaa nje sana na ndio maana hata suala la mgomo wa madaktari hajajihusisha nalo kabisa.

Lakini siku hizi kuna kamsemo ambapo wanasema msimlaumu/msimpongeze yeye bali washauri wake!
 
Dah!baba mwanaasha anapenda kwenda kuruka disco na kina 50 cent ss km kuna matamasha si lazima aende kuwacheki G UNIT hapa bongo akitinga tu Msondo ngoma kesho magazeti yote yatakua na picha yake ss huko Las Vegas,New york, anatinga kwenye kumbi za disco bila tatizo,hii picha yenyewe aliyopiga na 50 cent ni baada ya tamasha kwisha la G UNIT
 
Sisi tutaendelea kuilaumu NEC maana ndio iliyompa urais, sisi watanzania tulio wengi hutukumchagua.
 
Dah!baba mwanaasha anapenda kwenda kuruka disco na kina 50 cent ss km kuna matamasha si lazima aende kuwacheki G UNIT hapa bongo akitinga tu Msondo ngoma kesho magazeti yote yatakua na picha yake ss huko Las Vegas,New york, anatinga kwenye kumbi za disco bila tatizo,hii picha yenyewe aliyopiga na 50 cent ni baada ya tamasha kwisha la G UNIT

Mkuu hapo sasa umezidisha chumvi!
 
jamaa lazima mkumbuke ni lazima asafiri mara kwa mara ili akabadili blad, si unajua ana mambo yetu yale!

alah! Kumbe hii ndo logic ya safari zake??? I didnt know. Angekuwa mkweli tu, maana hakuna kunyanyapaana siku hizi.
 
Dah!baba mwanaasha anapenda kwenda kuruka disco na kina 50 cent ss km kuna matamasha si lazima aende kuwacheki G UNIT hapa bongo akitinga tu Msondo ngoma kesho magazeti yote yatakua na picha yake ss huko Las Vegas,New york, anatinga kwenye kumbi za disco bila tatizo,hii picha yenyewe aliyopiga na 50 cent ni baada ya tamasha kwisha la G UNIT

Du! Satelite na hiyo avatar yako! Hapo mkulu alikuwa wapi vile?
 
mwacheni rais wetu kipenzi chetu amalize muda wake akapumzike kafanya mambo makubwa sana katika nchi yetu wewe huwezi kujua na wala hutaki kujua
 
Back
Top Bottom