Rais amedhalilishwa au amujithalilisha?

kibajaj

Senior Member
Apr 12, 2011
106
26
Ni muda usiozidi miezi miwili pale Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya muungani aliposimama na kutangaza hadharani kuwa uzio wa mabati uliozungushwa katika eneo la jangwani ubomolewe mara moja na ujenzi wa aina yeyote usiendelee katika eneo lile kwani ni eneo la wazi.Wakati anaongea hayo waziri mwenye dhamana ya mambo ya ujenzi na makazi Prof Anna Tibaijuka alikuwepo pamoja na viongozi wengine wenye dhamana kubwa katika serikali ya jamuhuri ya muungano.Nusu saa iliyopita nimebahatika kupita eneo lile na kuona liko vile vile nilishangaa sana kuona kauli ya muheshimiwa haijatimizwa. Kwa hili nilijiuliza maswali mengi sana bila jibu la haraka.
Hebu sikia haya!

Ni kwamb watendaji wa serekali hawakumsikia rais?
Au hawmtii?
Ni kwamba rais hajui kuwa uzio ule haujabomolewa hadi leo?
Rais atakuwa amejiwekea heshma gani kama uzio usipobomomlewa na ujenzi uaendelea?
Au muda uliotolewa tena kwa sharti kuwa hata kama anayajenga amelipa arudishiwe pesa zake haujaisha?
Watendaji wa muheshimiwa wasiposimamia kuona agizo la muheshimiwa linatekelezwa watakuwa wamemdhalilisha sana
N a Raisi mwenyewe asiposimamia na kutuonyesha kwamba ana mamlaka ya kiutendaji na kiutawala atakuwa amejidhallilisha sana.
Mimi nilitegemea kesho yake tungepaona pale kweupeeee! Lo! ila hadi leo Hapa Rais kajidhalilisha kadhalilishwa?

" IT BEING A HOLISTIC DEMOCRACY,BUT THERE MUST BE THINGS TO STATE AND THINGS TO DISCUSS"
 
Amejidhalilisha!! Wasiotekeleza ni watu wake na wajnaomoliki ni watu wake. Anaongeaga tu ni kawaida yake. Inasikitisha sana kwa kweli.
 
Back
Top Bottom