Raila Odinga atua Dar es salaam kumtembelea Magufuli kwa kificho kikali

Mahebe

JF-Expert Member
Feb 7, 2009
319
63
Wana JF katika kuonyesha Dr.Magufuli na Odinga lao ni moja kwa taarifa nilizozinyaka na ni za uhakika ni kuwa Mh. Raila Odinga yupo Tanzania kumtembelea rafiki yake kipenzi Mh.Dr John P.Magufuli ambapo nimebahatika kupata baadhi ya picha kama mtakavyoziona hapo chini.Na inavyoonyesha ziara hii ni ya kificho kikubwa sana au ni umafia wa Dr.Magufuli kumkaribisha rafiki yake Raila ili wapange mikakati yao wanayojua wao wenyewe au wamepanga washerekee pamoja katika kuaga mwaka.

Wana JF naomba tizameni hizo picha wakati Raila Odinga akikaribishwa na mwenyeji wake Dr Magufuli katika uwanja wa ndege terminal one Dar es salaam siku mbili zilizopita.Nawasilisha! DSC00020.JPG DSC00021.JPG DSC00041.JPG DSC00042.JPG DSC00057.JPG
 
ana agenda gani huyu mjaluo! na kwa nini sasa na sio kabla au baada ya uchaguz wa kenya
 
Kama ni kwa heri hakuna shida. Kwani mbona wakubwa wengi wanaruka kifichoficho to abroad kwa mambo binafsi au kwa kuwa hawaanikwi root zao!! No problem with this alimradi tu wasije wakawa na mikakati ya kimafia (as u pinpointed).
 
Mi hata sioni hicho kificho ulichokipa kichwa cha habari.

Mkuu kama Si kificho hope media wangekuwa wametujuza leo siku ya tatu yupo TZ je ulijua yupo???

Ningefurahi kama ungeniunga mkono kupata nyeti hizi!
 
Mkuu kama Si kificho hope media wangekuwa wametujuza leo siku ya tatu yupo TZ je ulijua yupo???

Ningefurahi kama ungeniunga mkono kupata nyeti hizi!

Ninavyofikiri mimi hii ni private visit sio official visit kwahiyo sio lazima watu wa media waiandike.
 
Magufuli ana uzoefu gani katika siasa za nchi hii, kiasi mbaka raila aje kumconsult,mtu ambaye hajawahi hata kugombea urais?

...Huu urafiki utamsukuma Magufuli kuchukua form ya urais 2015...

...Na endapo Chadema itakuwa na nguvu zaidi kuelekea 2015,mashine za dharura kama Magufuli ndizo zitakazokuwa kimbilio la CCM,na hili likitokea kuna uwezekano wa upinzani kurudia tena pale zilipokuwepo 2005...
 
Magufuli ana uzoefu gani katika siasa za nchi hii, kiasi mbaka raila aje kumconsult,mtu ambaye hajawahi hata kugombea urais?

Ninacho amin mim ni kwamba huyu jamaa hajaja kutembea bongo apa, kaja na jambo ambalo kwake ni critical sana na ana imani kwamba Mzee wa Ujenzi atamsaidia....! kile alichofata kwa Magufuli ndo ujuzi ninao uongelea!!
 
...Huu urafiki utamsukuma Magufuli kuchukua form ya urais 2015...

...Na endapo Chadema itakuwa na nguvu zaidi kuelekea 2015,mashine za dharura kama Magufuli ndizo zitakazokuwa kimbilio la CCM,na hili likitokea kuna uwezekano wa upinzani kurudia tena pale zilipokuwepo 2005...
Mkuu usitarajie tena siasa za 2005,za ushindi wa kishindi,mtanzania wa leo ni tofauti na wa miaka hiyo!
 
Back
Top Bottom