Aliyosema yote ni kweli kwani hata humu JF kuna watu kazi yao ni kutukana tuu kama mtu atatoa hoja ya kuipinga chadema na wahusika wala hawachukui hatua za dhati kwa watu hao(wengi waliofungiwa ni wale walioisema vibaya chadema au wanaochafuana wao kwa wao)na utaona hata post zinazohusu kupiga debe chadema zinashabikiwa sana kuliko zile zinazoipinga chadema.Kwakweli hapa sasa pamekuwa ni kijiwe cha baadhi ya watu wasio na utaifa ambao kazi yao ni kubomoa tuu.
Pamoja na yote hayo wakae wakijua mwenye mbili havai moja hivyo ccm ushindi kama kazi kwa njia yoyote ile,narudia kwa njia yoyote ile huyo mtu wao wanaomtakasa hatapata hata 13% ya kura zote,kaeni mkisubiri ila mjue Utaifa kwanza na utashi wa vyama baadae kwani baada ya uchaguzi tunarudi wote pamoja.
Elimikeni jamani!
Mimi nashindwa kuelewa huyo mwana diplomasia, kwake ukweli ni nini? je mtu akisema JK ameshindwa kazi, kwa nini yeye hafafanui jinsi jk alivyofanikiwa? Badala ya kujadili hoja anajadili watu. Mwana diplomasia gani huyo? tutajie jina lake