Raia Mwema limepigwa ban?

Vyamavingi

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
5,745
5,446
Gazeti la Raia Mwema hutoka mara mbili kwa wiki; Jumatatu na Jumatano. Lkn nimeaambiwa na muuza magazeti kuwa Raia Mwema halikuwa mtaani Jumatatu, na leo Jumatano pia halijatoka! !

Sijasikia lolote kutoka ama upande wa wachapishaji au serikali (kama limefungiwa ) , kwangu gazeti hilo ndio pekee linalochapisha uchambuzi bila kuegemea upande.

Ikumbukwe wiki iliyopita likisababisha mzozo kati yake na Bunge kufuatia makala ya GT mmojawapo- Pascal Makala kiasi kwamba Spika wa Bunge Mh. Ndugai kuitaka kamati ya Haki na Madaraka ya Bunge kumuita Pascal Dodoma mbele ya Kamati hiyo. Spika alukaririwa pia akiwaonya Wahariri wa Gazeti hilo kufuatia makala hiyo ya uchambuzi.

Mtiririko huo wa matukio na kutoonekana mtaani kwa matoleo mawili mfululizo linafanya nijiulize kulikoni. Gazeti hilo limewahi kuingia kwenye mgogoro na serikali kiasi cha kuzuiwa kuchapishwa kwa miezi mitatu.

Vv
 
Cyo kweli!
 
Back
Top Bottom