Rahma Al Kharoos anatafuta Ubunge?

Mchokonozi

Member
Nov 17, 2009
15
0
Waungwana, mtaniwia radhi kwa kutoonekana ukumbini kwa muda mrefu. Nimekuwa nikisoma alama za nyakati ili niweze kuja hapa na mada iliyosheheni hoja za nguvu, si nguvu za hoja.

Naanza kwa hili la Mke Mdogo wa Mkuu wa Kaya – nadhani wote mnamtambua, sihitaji kumtaja jina lake – ambaye hivi karibuni ameanza kampeni za wazi wazi, ikionekana dhahiri kwamba si kwamba anajinadi ili kuweza kupata umaarufu wa haraka haraka, lakini lengo lake haswa likiwa kuupata Ubunge wa Viti Maalum kupitia Chama Tawala.

Habari za ndani kutoka kwa wadau walio karibu naye zinadai kwamba mwanamama huyu machachari na mkorodi, ambaye inasemekana kwamba “haambiliki” hata kwa Mkuu wa Kaya mwenyewe, amepania naye kuukwaa Ubunge huo ili naye aingie “mjengoni” mwaka 2010, lakini kisichojulikana ni kwa malengo gani haswa yanayomsukuma kufanya hivyo. Licha ya kwamba mwanamama huyu ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa kifedha – jambo ambalo amelidhihirisha wazi wazi – haieleweki ni kipi haswa anachokifuata “mjengoni” humo.

Duru za kisiasa zinasema harakati za mwanamama huyu zinaweza kuleta athari hasi kwa Mkuu wa Kaya, kwani zitasomeka kuwa harakati za kuigeuza hali ya kisiasa nchini hapa kuwa ya “kisultani”, kwani, minong’ono inasikikika kwamba mwana wa Mkuu wa Kaya, ambaye ni Mjumbe wa NEC kupitia Wilaya ya Bagamoyo, naye pia yumo mbioni kujiandaa kugombea kuingia “mjengoni”, ingawa hajatangaza rasmi nia yake hiyo.

Mwanamama huyu alianza kishindo cha kampeni zake siku chache zilizopita baada ya kumwaga kitita cha fedha taslim shilingi milioni 10, ambazo alihakikisha zinaonekana kwenye taarifa ya habari ya kituo cha luninga cha Channel Ten, ambacho ndicho kimekuwa karibu naye kwa wakati wote huu. Kitita hicho kilimwagwa kama “msaada” kwa timu ya soka ya wanawake, Twiga Stars, RK akitambulishwa kama “mdau wa soka ya wanawake”, na kutambulishwa kwamba amekuwa akiichangia timu hiyo mara kwa mara. Jambo la kushangaza ni kwamba, ni zaidi ya mara moja timu hiyo imekuwa ikitembeza bakuli kwa wafadhili mbalimbali, lakini haikuwahi kusikika hata mara moja kwa mwanamama huyo – ambaye anaishi nchini Oman – kujitokeza kuisaidia, licha ya uwezo wake mkubwa wa kifedha.

Jitihada za mwanamama huyu kujinadi wazi wazi hazikuishia hapo, kwani, ni Jumapili ya wiki iliyoisha, alijitokeza kufadhili kinyanganyiro cha kuwasaka walimbwende wanaoshiriki kupitia shindano la Miss Inter College, ambao washindi wake watapata nafasi ya kuingia moja kwa moja kwenye shindano la Miss Tanzania 2010. Safari hii, dau la mwanamama huyu limeongezeka kufikia Shilingi milioni 12, akijinadi kupitia kampuni ya RBS Oil and Technology.

Tathmini yangu ni kama ifuatavyo.

Iwapo mwanamama huyu ataachwa kuendelea kufanya ayatakayo, huenda kambi ya Mkuu wa Kaya ikapata athari hasi, kwani harakati hizi zitaweza kuwa “mtaji wa kisiasa” (political capital) kwa kambi ya upinzani, wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2010, jambo ambalo linaweza kuathiri vibaya matokeo ya kura zitakazovunwa na Mkuu wa Kaya
Duru za kisiasa zimezidi kudodosa na kusema kwamba, harakati za mwanamama huyu zinaweza kutafsiriwa kuwa ukandamizaji kwa wanawake kutokana na nafasi kubwa aliyonayo kama Mke Mdogo wa Mkuu wa Kaya, nafasi ambayo anaweza kuitumia ipasavyo kwani hakuna atakayeweza kumpinga wakati wa kinyang’anyiro hicho cha Ubunge kupitia Viti Maalum. Kampeni ya kusaka umaarufu kwa kutoa michango lukuki inasadikiwa kuwa ni kutaka kumwiga Mke wa Rais, ambaye tayari amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na mchango wake mkubwa kwa maendeleo ya wanawake na watoto, japokuwa Mke huyo hajaonesha nia ya kutaka kugombea nafasi ya kuingia “mjengoni”


Wadau wa masuala ya kisiasa wamemshauri Mkuu wa Kaya kumwita mwanamama huyo na kumkalisha, kasha kumpa karipio kali na amri ya kusitisha mara moja harakati zake hizo, kwani harakati hizo za kuutaka umaarufu zinaelekea kumwaga “mtama” na kuweka wazi mambo ya ndani ya “familia” yasiyopaswa kujulikana, jambo ambalo litaweza kuiweka kambi ya Mkuu wa Kaya kwenye wakati mgumu mara tu kipenga cha kampeni za Uchaguzi Mkuu kitakapopulizwa rasmi.

“Sio kwamba Mkuu wa Kaya anapendwa sana na wananchi wake, la hasha; sio kwamba wananchi wake wote watafurahi akirejea ulingoni, la hasha; itakuwa ni aibu akishindwa kurejea kwa sababu ya kukuru-kakara za mke wake mdogo”, alishauri mdau mmoja wa kisiasa.

Nimepewa ujumbe niufikishe kwa Mkuu wa Kaya. Natumai utafika.



>>> Mchokonozi, Shujaa wa Kuchokonoa!

 
Mkuu hoja yako inaeleweka na karibu kambini kwa mara nyingine tena. Remember one thing, at Jamii Forum we dare to talk openely. Ni vema ukamtaja mwana mama huyo maana ni wazi si watu wote tunamafahamu kama unavyofikiri. Na sidhani sana kama kapeni zake zitakuwa sahihi sana, kama anachotaka ni viti maalum tuu ingawa nina uhakika mkuu akishinda anamchagua amtakae kwa maslahi yake binafsi.

kwamba mwanamama huyo ataathiri mchakato wa mkuu, sina hakika sana. Hii ni kwa sababu CCM haishindi kwa sababu watu hawajawapigia kura. Wanashinda kwa sababu wameamua kushinda. Kwamba kwa kuiba au kutoo rushwa( maana wanatafuta bilioni 50 za uchaguzi lakini hawawezi kuongeza mishahara ya wafanyakazi hata kwa miaka 8), yote hayo yanawezekana. Nakuhakikishia wapo wapinzani na wabunge machachari hawatarudi bungeni,si kwa sababu wananchi hawatawachagua, bali CCM watakuwa wameamua hivyo)

Nashauri mwanamama huyo aongeze kasi, na kama wapo 'wake wengine wadogo' au hata mama salma mwenyewe wajitokeze kwa wingi kutafuta nafasi hizo, maana kama kweli watasababisha mkuu asirudi madarakani, inawezekana, na nasema inawezekana, ikawa ndo ukombozi wa Tanzania
 
Mchokonozi,

Mimi simfahamu huyu mama na kwa kushindwa kumtaja, hujanitendea haki yangu hapa JF ambapo we dare to speak openly!

Lete jina mshikaji ili hata sisi vilaza tujue.
 
DSC09813.JPG


Rais wa kampuni ya RBP OIL & INDUSTRIAL TECHNOLOGY (T) LIMITED,Mama Rahma Al Kharoos akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari waliofika leo katika Hoteli ya Movenpic wakati wa akitangaza udhamini wake wa Mil. 12 kwa ajili ya shindano la Miss Dar Inter College

DSC09823.JPG


Rais wa kampuni ya RBP OIL & INDUSTRIAL TECHNOLOGY (T) LIMITED,Mama Rahma Al Kharoos akikabidhi Hundi yenye Thamani ya shilingi Mil. 12
 
.....Interesting! Nilizion hizi picha kwenye blogu......Nikawa najiuliza maswali mengi, halafu leo nasoma hili la nyumba ndogo!......
 
Mh kwa vidokezo hapo je una maanisha mama Rahma Al Kharoos? Eka wazi bana ebo!
 
Salma kikwete......anatokea Rufiji....nyamisati na ndipo alipojenga shule yake ambayo inasomesha wanafunzi bure. Mchakato Wa kuwapata hao OVC haujulikani.
 
357q3pw.jpg


Toka kushoto ni balozi wa Palestina nchini, Mh Yusuf Habab, Balozi wa Saudi Arabia nchini mh Al-Jarbuo Ali,Mwenyekiti wa kampuni ya mafuta ya Noor Oil-Industrial technology,Mama Rahma Al kharoos al kharoos, Najey Al Haram pamoja na Bw.Ali

Source: Michuzijr
 
Sasa kila Mtu akitaka ainngie mjengoni, kwa staili hii nani tena atakuwa pembeni??

26870_116830848335861_100000268407034_219550_6693419_n.jpg






HAWA WATU WAPO VERE VERE STRATEGIC...


27ymg8.jpg



shy+2.jpg
 
Rais wa kampuni ya RBP OIL & INDUSTRIAL TECHNOLOGY (T) LIMITED,Mama Rahma Al Kharoos akikabidhi Hundi yenye Thamani ya shilingi Mil. 12

Ahsante sana Masanilo aka Msukuma wa mjini kwa kutufungua macho...we mtu!
 
Nadhani hakuna haja ya kufanya uchaguzi Tanzania, tumsimike Mh JMK awe ni Mfalme na viongozi watokee kwenye ukoo huo huo wa kifalme
 
Tutawakoma Vikwete.
Jakaya Kikwete ni rais na Mwenyekiti wa CCM (Chama tawala kwa sasa)
Salma Kikwete ni mjumbe wa Mkutano Mkuu (kwa kugombea)
Wadogo wa Mzee Jakaya, Mohamed Kikwete na Yusuf Kikwete ni wajumbe wa Mkutano mkuu wa CCM,
Ridhiwani Kikwete ni 'king-maker' wa UVCCM na kiongozi wa kitengo cha 'ukaji hapo UVCCM,
Khalfani Kikwete (11 yrs old) ni mjumbe wa mkutano wa Chipukizi wa CCM
Na sasa tena huyu Rahma Al Kharoos?
Na zile nyinginezo......???

Baba wa Taifa alisema kama unampenda mtu kwa sura yake, kuchekacheka kwake na mizaha yake, basi mualike nyumbani, mpikie chai, kisha mtazame anavyoinywa na kuchekacheka, ila SIYO KUMFANYA AWE RAIS WAKO!
WaTz sasa wanayakumbuka maneno hayo ya Mwalimu...
 
Contacts za huyu mama basi. Nimsaidie kupiga kampeni japo kwa hali (mali sina), kama itasaidia kuiangusha CCM ya mafisadi! :angry:
 
Ahsante sana Masanilo aka Msukuma wa mjini kwa kutufungua macho...we mtu!

Ahhhhh bwana kwenye week 2 Mh Rahma Al kharoos al kharoos ametumia Mil 22 kwenye publicity ...10 mil netball na Ridhiwani akiwepo na tena 12 Mil kwa Wazuri (Miss) intercolllege...Hizi pesa zina nunua madawati mangapi.....hawa wanasiasa hawajuai sehemu za kupeleka pesa zao. Mimi hapo ningejenga Dispensary kule anakotekea Balatanda ama kwa kina Manyoya wa Ngoswe

The Following User Says Thank You to Masanilo For This Useful Post:
Bubu Ataka Kusema (Today)



 
Back
Top Bottom