Rafiki yangu anamuoa ex wangu daaah!!!

Nobrain

JF-Expert Member
Feb 26, 2020
248
691
Yaani mwezi uliopita nimepigwa na Mshangao mkubwa Sana. Iko hivi kipindi nasoma chuo flani hapa Dar, nilikuwa na Jamaa yangu (Tuseme anaitwa JAMES), lakini pia darasani kulikuwa na demu mmoja hivi (tumwite Rose) alikuwa ni mtu wa Dini sana.

Mimi pia kipindi hicho kwenye maswala ya Ibada na maombi nilikuwa naenda kishikaji vile, nazuga zuga Tu. Siku moja yule demu alinifata na Kusema angepebda tuwe na Company ya Kusoma Pamoja na Maombi.

Mara nyingi alikuwa anakuja sana Getto kwangu, so kuna Siku nilitest mitambo Tu, kumchezea Tukiwa getto, dem akanipatia mbususu. Hapo ndo kulizaliwa mapenzi, na Kwa kweli alinipenda yule manzi.

Muda huu wote James alikuwa hajui chochote kama ninamla ROSE. Lakini pia James na Rose pia walikuwa na urafiki wa kawaida na kwenye maombi walikuwa wanaenda pamoja mkmi nikiwa sipo.

Tulipomaliz chuo, zile harakati ngumu za kutafuta maisha zikanifanya nitengane na Rose, na mara ya mwisho nakumbuka nilimcheki miaka 7 ilopita hakupokea simu. Nikaamua kumpotezea.

Lakini kwa muda wote huu, nilikuwa nawasiliana na James ile kishikaji Tu. Siku moja nikaelekea mkoa X, na kwa bahati nzuri nikakutana na James, mwamba alifurahi sana na tulipiga stori nyingi.

Nakumbuka jioni moja, aliniomba niende kwake nikamsalimie Shemeji maana Katoka Kujifungua mtoto wa Pili siku si nyingi. Kwa kweli nilikubari kwends, sikuwa na hiyana yoyote kwani alikuwa ni mshikaji wangu kitambo!!

Nilifika nyumbani kwa James na kumkuta Mwanamke amekaa sabreni majira ya Usiku. Nikainama kuvua vuatu. "Karibu Shemeji, ingia bila kuvua viatu" ilisikika sauti ya Yule mwanamke, nikamwambia hakuna Shida nishavua na kuinuka.

Alahaula!!!!!!! Kumtazama yule mwanamke kumbe ni ROSE aisee....!! Nilishituka sana na hata yeye kama alipata kigugumizi, ikabidi nikaze tu, na kumsalimia mtoto wao mkubwa aliyekuja kusimama pembeni yangu.

Nilikaa pale ndani, na rose alipika chakula kitamu, tukala huku tunapiga stori za Hapa na Pale. Wakaniuliza kuhusu familia yangu nikawaambia iko poa.

Baada ya stori Jamea alinidokeza swala lao la kufunga ndoa. Na akaniomba mimi ndo niwe Best-man wake.

Kiukweli pale nilishindwa kukataa wala kukubari. Nikawaomba wanipe muda ili niangalie mambo yangu yanaendaje, kwani hata hivyo ndoa ni mwakani mwezi wa kwanza.

Baada ya wiki nilimchangia Rafiki yangu kama 500k. Na kumpongeza sana kwa Hatua aliyochukua.

Sasa hapa nilipo nimekwama kuelewa nini nifanye, nikubari kuwa Best-man wa rafiki yangu ilhari anamuoa mwanamke niliyekuwa nampenda au niwakatae?

Kwako mwana JF. Nipe mawazo
 
Yaani mwezi uliopita nimepigwa na Mshangao mkubwa Sana. Iko hivi kipindi nasoma chuo flani hapa Dar, nilikuwa na Jamaa yangu (Tuseme anaitwa JUMA), lakini pia darasani kulikuwa na demu mmoja hivi (tumwite Rose) alikuwa ni mtu wa Dini sana.
Wape support then endelea na maisha Yako,Wala usifikirie kuleta uhuni.

Na kama unajiona haupo comfortable na ubest man, basi mchango uliowapa unatosha.
 
Yaani mwezi uliopita nimepigwa na Mshangao mkubwa Sana. Iko hivi kipindi nasoma chuo flani hapa Dar, nilikuwa na Jamaa yangu (Tuseme anaitwa JUMA), lakini pia darasani kulikuwa na demu mmoja hivi (tumwite Rose) alikuwa ni mtu wa Dini sana.
Acha ujinga huyo sasa ni shemeji yako. Endeleeni na urafiki wa kawaida isitoshe huyo jamaa yako hajui usije leta taharuki ambayo itaharibu ndoa ya rafiki yako. Kuwa bestman mwenye hekima.
 
Back
Top Bottom