Rafael Mgaya: Mnadanganywa, wafanyabiashara hawafichi mafuta ila uagizaji umepungua kwa 28% tangu January wakati matumizi yamepanda kwa 10%

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,503
2,046
Akizungumza kwenye kipindi cha asubuhi katibu wa waagizaji wa mafuta anasema hao wanaosema mafuta yamefichwa hawasemi ukweli.

Anasema waliishauri serikali tangu January kwamba iongeze dollar ili kuongeza kiwango cha mafuta kinachoagizwa kutokana na kupanda kwa thamani ya Dola dhidi ya shilingi na kupanda kwa bei ya mafuta duniani, lakini serikali haikusikiliza badala yake wafanya biashara wakaanza kushusha kiwango cha kuagiza mafuta.

Mbali ya kushusha kiwango cha mafuta yanayoagizwa hali ya matumizi nchini imeongezeka Kwa zaidi ya 10% amedai Rafael.

Amesema aliyesema mafuta yapo ya kutosha siku 18 anahesabia hata mafuta yaliyo kwenye meli ambayo kimsingi bado ni ya supplier.

Tatizo la kukosekana Kwa mafuta linatokana na serikali kupuuza ushauri wa waagizaji walioitaka serikali iongeze dollar kwaajili ya kuagiza mafuta.

Zingine zote ni porojo tu.
 
MWALIMU NYERERE ANAMALIZA KWA USHAIRI KWENYE KITABU CHAKE.

UONGOZI WETU NA HATMA YA TANZANIA.

Ole wake Tanzania Tusipoisaidia, Niwezalo nimelifanya kushauri na kuonya nimeonya.

tahadhali nimetoa ushauri na kuonya nimeshatoka kitini zaidi nifanye nini.

Namlilia Jaalia atumulikie njia Tanzania ailinde WAOVU wasiishinde.

Amina Tena Amina Amina Tena amina

UONGOZI WETU NA HATMA YA TANZANIA.

MWALIMU JK NYERERE
 
Mbna bei ikipanda yanaanza kupatikana?
Hawa wauzaji nao kuna mchezo wanaucheza,
 
Wakija kujitetea dollar imeadimika sababu ya Vita n.k
Muwaulize yule Yohane (John) aliyenguruma toka nyikani alitoa wapi dollar wakati wa Covid 19 shughuli nyingi za uzalishaji zimesimama?

Wakirudikujitetea wafanyabiashara wa mafuta wameficha mafuta.
Muwaulize nani ana vyombo vya Dola vya kusimamia sheria na vya uchunguzi? Kwanini viongozi wakose nguvu ya kuwashawishi wasifiche mafuta wanahujumu uchumi?
 
Mambo ya ajabu kama haya hutokea awamu za waswahili sababu ya kubembelezana kwingi kuliko kazi.
 
Kakaa kimya Tanganyika inapuyanga kama gari bovu, tunaweza kusema kama hatuna rais vile
 
Back
Top Bottom