eliesikia
JF-Expert Member
- Oct 29, 2010
- 787
- 755
Mimi nilishiriki katika kuwashawishi Dowans kuja nchini. Nitaendelea kushawishi wawekezaji waje nchini ili nchi iendelee, ajira ipatikane na kodi ziongezeke.
Juzi tu nimetoka Singapore, Malaysia na UAE (Falme za Kiarabu) kuwashawishi wawekezaji kuwekeza kwenye usafiri wa anga, alisema Rostam.
Alipotakiwa kueleza iwapo yeye ni mmoja wa watu wanaotarajia kufaidika na malipo ya shilingi bilioni 185 ambazo TANESCO inatakiwa kuilipa fidia Dowans, mfanyabiashara huyo alikana kuimiliki kampuni hiyo.
Mbali ya kukanusha hilo, Rostam aliyabeza madai ya baadhi ya wanasiasa wanaohusisha fedha hizo na yeye akisema katika mkusanyiko wa biashara zake anazofanya ndani na nje ya nchi kiasi hicho cha fedha wanazotarajiwa kulipwa Dowans ni sawa na mapato yake ya miezi minne tu.