Q-Chillah ft Patoranking - KOKU

Nyimbo nzuri ndio ila sio kwa maskio mengi ya wabongo, jamaa alitakiwa kupigilia verse yake kwa kiswahili. Tatizo la chila amekuwa akidhania kuimba ngeli basi ndo kuonekana anajua au ndo atapata urahisi wa kutoboa, kuna kipindi aliachiaga ngoma kama 2 kaimba ngeli tupu na zote zikabuma then akawa kimya muda mrefu then akarudi na ngoma ya lugha ya taifa inaitwa "mdogo mdogo" ngoma ikafanya poa sana

Hatukatai jamaa kweli ngeli yuko vizuri sana tena kwenye pronunciation ya maneno ila hicho sio ambacho wabongo wengi tunapenda, ndomana mtu kama Diamond siku hizi anaongea ngeli safi kabisa lakini hajitii ujuaji wa kuimba nyimbo kwa kingereza anajaribu kuwa unique kwakuwa lugha yetu kwa sasa inakuwa sana na watu wengi wanajifunzia kupitia nyimbo za wasanii wetu sasa karibia nchi zote zilizoendelea Africa zinaimba kwa lugha ya kingereza sasa wewe mbongo utawapa radha gani tofauti unadhani,

Lugha ya kiswahili kwa sasa inapendwa sana Africa inabidi wasanii wetu hili walijue, na ata ukiimba kisukuma mtu ambae haelewi atapenda tu the unavyo sound, vionjo na ulivyotembea na beat, ndomana wabongo wengi unakuta tunapenda nyimbo za kidhuru, kihispania, kiarabu na ilhali hatuelewi kinachoimbwa ila kwakuwa ni mziki mzuri lazima utaenjoy tu. So chilla aachane na hii dhana ya kudhani lugha ya kigeni itambeba kwenye soko la nje ataishia humu humu mchangani

Kitu kingine alichobugi ni kushindwa kufanya timing nzuri, yani kipindi kipi aachie ngoma yake, kaja kuiachia kipindi kibaya sana kuna ngoma ya darasa ambayo imeficha ngoma kibao kwa sasa so ngoma yake imekosa tension kabia kwa sasa ndomana anakuja na excuse kama kusema eti nyimbo imevuja mara hv mara vile baada ya kuona hajapata kile alichokitegemea, ye alitegemea kwa kumshirikisha patoraking basi ngoma ita trend sana alafu imekuwa tofauti
 
Ngoma ni kali kwakweli,, nnavyozidi isikia nazidi kuielewa. Q Chilla karibu WCB uone Nuru.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom