Nucky Thompson
JF-Expert Member
- Sep 20, 2016
- 1,817
- 4,058
Msanii wa Bongo fleva wa kitambo Q Chief amedai ana uwezo mkubwa sana kimuziki na hili limethibitishwa alipoomba kolabo na msanii wa Nigeria Patoranking
Anadai alipoomba kolabo na msanii huyo yeye hakutaka fedha aliomba apewe demo na alipopewa demo akapigwa na butwaa juu ya uwezo wa msanii huyo na kushangaa alikuwa wapi kipindi chote hicho
Amesema wasanii wa size yake ambao anatakiwa kukaa nao meza moja ni Patoranking na sio hawa wengine tunaowajua
Ametolea mfano wa mume au mke kuwa na mwenza mzuri ndani na hagundui kuwa ni mzuri bali watu wa nje ndio humuona mzuri