Pwani: Askari Wawili wa Usalama Barabarani wauawa kwa kupigwa risasi Kibiti

Mkuu unawakumbuka wale "majambazi" waliouliwa na polisi kule Mkapa Bridge? Mauaji ya kibiti yana SIRI KUBWA!
Nawakumbuka tpaul..... so how tunashindwa wap tunakwama? Hd ifikie hatua jwtz wapelekwe nihali amby aibu kwa jeshi la police na vikos vingine visivyokuwa jwtz. Kuwapeleka jwtz kwaupande wangu ninaona police wetu hawa hawana uhodari na ujuzi ikiwa wao wameshindwa. Jaman tunajua sote kaz ya jwtz ni ipi. Ndugu zetu pwani haswa kibit,tufiji na mkuranga wanaishi ktk hali mbaya hawana hakika yao yakesho ama jion ijapokuwa mungu ndie mpangaji wakifo lkn isiwe kwahali km hii. Narudia tena busara na hekma vinapaswa vitumike sana. Km nguvu tulitumia lkn bado haikuzaa matokeo mazr na mbaya zaid kila linapotolewa kauli wakuu hawa watu ama majini whatever nawezawaita wao ndio wanafanyakusudi.

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
nakumbuka swali la history ..the colonialists sowed the seed of their own destruction...discuss...tuna vijana tuwapeleka jkt hivi wanajulikana ni wangapi na wanafanya nn...je hawa migambo vipi? hilo halitoshi kama hawa watu hawaogopi kuuwa askari je tunajua hatua inayofata? kujitoa mhanga kutaanza ktk maeneo ya raia na ndipo washangiliaji wote watakapojuta...siku muhimbili ikiliuliwa ndio tutajua hawa sio watu wa kushangilia

Mkuu mambo mengine hatutaki kuyafikiria tunayawaza kimya kimya kwamba labda Mungu atayahepushia mbali, tukio la leo ndiyo limenifanya nifikirie mambo mengi mengi sana labda niko overly paranoid hata sijui - sisi hapa kwetu sijui tukoje kwa nini hatujifunzi kutoka kwa wenzetu - juzi hapa kwa mfano magaidi/waarifu walivamia Teherani Iran ndani ya masaa 36 wote walishabainika wako wapi na wakashughurikiwa kikamirifu, Uingereza, Urusi, China, Ujerumani, Spain na huko Marekani mijamaa imekuwa trained kwa ku-deal na situation fasta fasta kwa kuwa wanaelewa wakilaza damu sleeper cells watakuwa activated na kuleta balaa juu ya balaa, wanatumia vyombo vyao vya habari kikamilifu, if need be matangazo yote yanakatizwa wanajikita kutangaza tukio hilo moja masaa 24, Taifa zima linakuwa kitu kimoja watu wanatoa taarifa, maoni na mbinu za kusaidia Dola.

Msifikiri Askari na wapelelezi ndiyo wenye akili tu za kujua wapi pa kuanzia, kumbuka hata watu ambao hawajaenda shule wana akili sana, wenzetu Ulaya na Marekani hawadharau maoni ya wananchi - utawasikia wana waomba raia wao watoe hata clue moja however insignificant lakini hiyo inaweza kuwa ni nyenzo muhimu ya kusaidia askari/afisa aliye kuwa trained kuzitafasiri na kuplan next move ya ku-deal na crime, sisi hapa kwetu hilo huwa alipewi umuhimu wowote, jaribu kufungulia channels zote utakatua zinazungumzia zaidi masuala ya mpira wa Ulaya na Wanamiziki wa Marekani basi, chukulia tukio la ugaidi huko London mwezi uliopita - CNN na MSM za huko Uingereza zilikatisha matangazo ya kawaidi wakatangaza tukio hilo zaidi ya masaa 12 wana hoji raia kuhusu maoni yao nini kifanyike, kama wana information za kusaidia Dola nk - sisi hapa kwetu hilo halipo kabisa, hakuna hata kipindi cha kila wiki cha "CRIME WATCH" Watanzania hasa Wizara ya mambo ya ndani wanakosa ubunifu wa ku-deal na majambazi na magaidi, nendeni mkajifunze kwa wenzetu - we need a flying squad.
 
Inaonekana hiki ni kisasi baina ya watu flani na polis haiwezekani iwe na askali tu,ombi vyombo vya dola vifatilie vizur swala hili wap pamekosewa itabainika tu
 
Hawa jamaa wakiendekezwa ipo siku wataua basi zima la wanachama wa CCM endapo watapita maeneo hayo ya kibiti. Kama hapo wanamiliki silaha za kawaida kama smg, vp wakipata LMG, RPG, Heavy Machine Gun cartridge 12.7 × 99mm NATO hapo si tutapoteana hapa town.
 
Kwanini hawa jamaa hawatoi sababu....shida yao nini..

Mbona wenzao al shaabab na boko haram madai yao yanajulikana..
Hawa kenge wanaua tu..
Wapuuzi sana.
sababu zitakua zinajulikana ndo mana hawazitaji by the way nadhani sio magaidi maana serikali bado haijasema kama nimagaidi bali ni majambazi
 
Mimi binafsi nilishangaa Kupeleka kule jeshi la wananchi wanaenda kupigana na nani coz wale ni hit man sasa jeshi linaenda kufanya nini zaidi kukamata Raia wasio na atia
 
Hivi kweli serikali inashindwa kupambana na hao wauaji ona askar walivyo uawa bila hatia inatia uchungu sana,maeneo ni hayohayo kila siku mauaj kwa nn ulinzi usiwe maalumu askar wanapotea
 
Kwanini hawa jamaa hawatoi sababu....shida yao nini..

Mbona wenzao al shaabab na boko haram madai yao yanajulikana..
Hawa kenge wanaua tu..
Wapuuzi sana.
Kuna tatizo kubwa sana huko......watu wanateketea mno......hasa askari....
Linahitaji mkakati wa nguvu sana..
 
Muda mfupi uliopita askari polisi wawili wa kikosi cha usalama Barabarani Bungu, Kibiti wamepigwa risasi na kufa papo hapo wakiwa kazini eneo kati ya Bungu na Jaribu! Walikuwa watatu, mmoja wa kike kasalimika!

.Tutaendelea kukujuza jina la askari huyo na namna mauaji hayo yalivyotokea hivi punde.

Tunashukuru kwa taarifa lakini tusiwe tuna attach picha ambazo ni horror!! Wengine hatupendi kuona damu damu.
 
Amejibu vizuri, kuna sehemu tumekosea kama serikali lazima ikiri kuwa wamefeli na sababu ni nyingi sana. Tatizo la kibiti ni dogo sanaa kwa viongozi ambao wanatumia akili, wapo focused determined na wanajali maisha ya watu wao. Mwisho: hatuwezi linganisha hali ya kibiti na yanayotokea Uingereza au America that's a different case scenarios. Kibiti pale ukimpeleka kiongozi mmoja hata angekuwa mkapa au kikwete wangeweza handle vizuri tu
Mkuu watu hawataki kusikia ukweli, wanataka kusikia yatakayofurahisha nafsi zao

Tatizo la Kibiti ni kubwa kwa eneo la kibiti kwa sasa, halikuanzia hapo.
Tatizo lilianza askari walipoanza kuvamiwa kule Ikwiriri na kisha Bungu kama sikosei.

Huko mauaji yalifanyika na silaha zilibwa kutoka vituoni. Matukio hayo yalikuwa tu kiashirio kuwa hali ya mauaji ya wananchi iliyokuwepo katika 'low profile' kama uhalifu wa kawaida

Hayo yametokea mwaka mzima, kiasi kwamba yalitosha kabisa kuwa 'warning' hali si shwari

Leo tumefika mahali tusipojua kwanini wananchi wanaendelea kuawawa, askari wanauawa na hainonekani kama kuna ushirikiano katika ya vyombo na Raia

Hatuwezi kukwepa ukweli kuwa laiti ingalikuwa tukio la kisiasa tungeona viongozi wakiwa katika foleni za vyombo vya habari kwa matamko makali, '' tumejiandaa kukabiliana nao, tuna taarifa za hali mbaya usalama, atakayejaribu ataona cha mtema kuni, lazima kila mtu atii sheria, msicheze na dola' na kila aina ya vitisho. Hili halihitaji kufikiri ni la kila mara tunalijua

Hoja inakuja, hawa majambazi waliofikia kuua askari wetu wa usalama na usalama barabarani ni wengi kiasi gani kwamba hawawezi kukabiliwa?
Wana nguvu kiasi gani kiasi wanakuwa tishio?

Jibu lake tungelipata kupitia intelejensia zile zile zinazoweza kuona au kubashiri 'hali ya usalama tata au si nzuri kwa matukio ya kisiasa'' , Je nini kinakwamisha?

Hatuwezi kufanikiwa kwa kusingizia eti ni Acacia au mabeberu wanataka kutuyumbisha kwasababu za uchumi. Mauaji Mkuranga, Kibiti, Bungu hadi Ikwiriri yameanza wakati kontena za mchanga zinapita raha mustarehe, haiwezi kuwa sababu hata kidogo

Kibaya zaidi tunaamini 'drones' zinaweza kuwa na majibu, bila kujiuliza azma ya haya majambazi ni kitu gani? Kuua askari wa usalama na kutokomea, au kuua askari vituoni na kutokomea haionekani kama ujambazi wa kupora. Je, nini hasa azma ya hawa waovu?

Pili, wamefanya kitu gani kiasi kwamba wananchi wa maeneo hayo hawatoi ushirikiano?

Je, kuna watu wanofuatilia mauji hayo na kuunga dots ili kupata motive behind?

Haiwezekani leo mwenyekiti, kesho mjumbe, keshokutwa mzee wa mtaa siku nyingine kiongozi wa nyumba kumi, tukabaki kudhani ni mauji ya majambazi ya kawaida yenye mwenendo 'pattern' fulani. Kwanini kuna walengwa?

Tukishapata majibu, tunaweza kusema nini kifanyike.

Tulikuwa na tatizo hilo Ngorongoro ambapo Wasomali walifanya sehemu ya nchi yetu kama Somalia, wakiwa na amri hata za kuua OCD. Utafiti ukafanyika kwa intelejensia makini na haraka, suluhu ikapatikana hadi kesho Wasomali hawataki kusikia Ngorongoro! Heshima mbele

Haya ndiyo tunataka kuona yakifanyika,kinyume chake tunasikia intelejensia ikiwa kali kuita watuhumiwa waliotajwa kwa madawa na yule bwana. Je, watuhumiwa hao ni hatari kuliko haya majambazi ya Rufiji yanayoua tu kwa unyama kiasi hicho?

Je, kuna priority za nini cha dharura na hatari na kipi kifuate kwa intelejensia?

Kosa kubwa tunalofanya na lisilotupatia majibu ni kutojadiliana kwa dhati, ukweli na weledi

Hili ni tatizo la Kitaifa si la chama wala mtu. Mauaji ya askari wetu yanatisha katika eneo dogo kama la Rufiji. Hatutaki kuona askari wetu wakiwa katika hali ya kuumia kisaikolojia kila wanapotoka kwenda kazini ikiwa watarudi salama.

Hatupendi kuona askari ambao wana ndugu na ni ndugu zetu wakifanyiwa unyama wa kutisha na majambazi yanayopaswa kutokomezwa kwa silaha zozote kali zilizopo yakibainika

Tutafute ukweli, tutafute majibu , tusitafute njia za mkato za visingizio au teknolojia zisizowekana. Tunaweza kutumia akili zetu kwa usahihi tukapata majibu

RIP askari wetu, Poleni sana ndugu. Inatuuma sana
 
Hawa jamaa wakiendekezwa ipo siku wataua basi zima la wanachama wa CCM endapo watapita maeneo hayo ya kibiti. Kama hapo wanamiliki silaha za kawaida kama smg, vp wakipata LMG, RPG, Heavy Machine Gun cartridge 12.7 × 99mm NATO hapo si tutapoteana hapa town.
wewe umejuaje kama wanamiliki smg?
 
Back
Top Bottom